Pacome vs Simba SCPacome vs Simba SC
  • Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP namna ambavyo imemalizwa msimu wa 2024/25.
  • Jean Ahoua wa Simba SC mwenye mabao 16 na Pacome wa Yanga SC mwenye mabao 12 kitaumana.
  • Aziz Ki alitwaa tuzo msimu wa 2023/24 akiwa na uzi wa Yanga SC mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25.

Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP imemalizwa kwa vitendo uwanjani. Ni wachezaji wawili ambao wanatajwa kuwania tuzo hiyo kubwa ndani ya ligi 2024/25, NBC Premier League. Pacome Zouzoua  wa Yanga SC na Jean Ahoua wa Simba SC wanapewa chapuo kutwaa tuzo.

Mamilioni haya hapa mgao ni sasa

Mamilioni ya kindege yapo tayari kwa ajili yako. Paisha kindege sasa na uvune mamilioni. Kila siku huku ni kicheko.

Aviator banner

Vita ya MVP yashika kasi

Aziz tuzo
Aziz ambaye yupo Wydad kwa sasa na tuzo ya MVP 2023/24.

Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC asilimia ndogo kubaki

MVP, (Most Valuable Player) msimu wa 2023/24 alikuwa ni Aziz Ki wa Yanga SC. Aziz Ki alifunga mabao 21 na pasi 8 za mabao. Yanga SC ilitwaa ubingwa wa ligi.

Msimu wa 2024/25 Pacome amefunga mabao 12 na pasi 10 za mabao. Kahusika kwenye mabao 22 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga. Yanga SC ni mabingwa wa ligi wakiwa na pointi 82 huku nafasi ya pili ni Simba SC yenye pointi 78. Ahoua kafunga mabao 16 na pasi 9 za mabao kahusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC.

Sakata la MVP limemalizwa namna hii Yanga SC

Ahoua J C
Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25

“Tuliona maneno mengi mtandaoni kuhusu tuzo ya MVP. Tuliwaambia suala la MVP litamalizika uwanjani. Kila mtu ameona, sitaki kuwaingilia kamati ya tuzo lakini nafikiri wanapaswa kutoa tuzo ya MPG (Most Penalties goals). Kila mtu apewe tuzo ambayo anastahili ili tutende haki.

“Nilimwambia Pacome, ana kazi zaidi ya moja kwenye Kariakoo Dabi. Kwanza kumpa tabu yule mchezji wao ambaye walikuwa wanamuimba sana na wanamuamini. Halafu kazi nyingine ilikuwa ni kufunga na kutoa pasi hilo najua alikuwa analimudu.

“Kufanya hivyo kulikuwa kunakwenda kuamua nani anakuwa MVP kwa vitendo. Unapozungumzia kuhusu MVP unazungumzia mchezaji ambaye anatoa picha kuhusu ligi yetu. Yaani dunia nzima ikimtafuta mchezaji inaona uwezo wake na kasi yake.

Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB

“Sio unatafuta MVP wa ligi yetu unakutana na mabao yakutengwa sijui penati hapana. Tunataka ukiingia kumtafuta mchezaji bora unakutana na mwendo wa mpira watu wanadondoka chini. Mabao makali yanafungwa na watu wanafurahi.

Pacome vs Simba SC
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Source Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mchongo huu wa ubingwa Yanga – SportPesa Tanzania

“Hakuna namna kazi kaifanya na kila mtu ameona. Sasa nilimwambia kwamba akifunga nitampa milioni moja na akitoa pasi ya bao nitampa milioni moja. Kafanya yote kafunga na kutoa pasi ya bao, nimempa milioni mbili Pacome sio ubabaishaji kwa kuwa pesa ninayo.

Kususu fainali ya CRDB Federation Cup 

“Klabu ya Yanga SC inajiandaa kwenda Zanzibar kwenye fainali ya CRDB federation Cup kucheza dhidi ya Singida black Stars. Taarifa kuhusu safari hiyo, kwamba timu inaondokaje, inaondoka saa ngapi, mimi mwenyewe sijui. Huo ndio utaratibu wetu kwa sasa kwa mechi kubwa.

“Unajua hizi mechi kubwa zina mengi ambayo yanatokea. Kuna watu hapa utashangaa wanauliza timu inaondoka saa ngapi, inapita wapi wanaanza kutoa taarifa huko. Hilo tunalijua na kwa sasa sijui chochote kuhusu timu ila ninachojua itaondoka na itakuwa Zanzibar kwa fainali.

Sherehe za ubingwa zinaanza

“Kwenye sherehe za ubingwa tutaanza na dua ya kumshukuru Mungu. Asiyeshukuru kwa kidogo basi hata kwa kikubwa hawezi kushukuru. Hapo Juni 27, makao makuu ya klabu tutaanza dua ya shukrani na kuomba kheri kwa ajili ya mchezo ujao.

Simba Supu
Shabiki wa Simba SC kwenye sherehe za ubingwa wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi

 “Na baada ya hapo tutaweka historia kwa kunywa supu ya Ngamia. Tumekunywa sana supu hizi za kawaida ila sasa hii ni nyingine. Ni Ngamia mwenyewe na unajua namna alivyo hii kubwa sana.

Kuhusu suala la Parade, nataka niwape siri. Baada ya mechi kuisha, uongozi wa Yanga ulifanya mawasiliano kuulizia upatikanaji wa lile la Bus la Parade. Wenye Bus wakatuuliza kwanini sisi ni mabingwa? Wakasema kuna watu walipiga simu siku kadhaa kuweka oda ya Bus. Kumbe ukimya wa Aviola muda wote walikuwa busy kutafuta Bus la Parade.”

Hili neno la shukrani kutoka Yanga SC

“Shukrani za kipekee ni kwa wachezaji wetu ambao walimwaga jasho na damu, benchi la ufundi wamejitoa kwa namna ya kipekee. Tunawapongeza pia wapinzani wetu wote 14 kwa kutupa ushindani wa kutosha. Lakini kwa kipekee tusiache kumshukuru Aviola kwa ubabaishaji, ubabaifu na propaganda. Yote hayo yamepelekea kutufanya sisi kuongeza umakini.

“Tuna furaha kubwa sana msimu huu. Mtakumbuka pale uwanja wa KMC, Msemaji wa Aviola alitangaza kuwa wao wanacheza mechi za Yanga SC. Ile kauli ilituamsha sana, wananchi Niwaambie ukweli, kauli ile ndiyo iliyokuwa kifo chao. Kubeba ubingwa ni jambo zuri, lakini aviola kutoka kapa ni furaha kubwa zaidi.

“Msimu huu tumepitia mengi sana kama Klabu. Lakini siri yetu ya mafanikio. Licha ya mawimbi makubwa ni umoja na mshikamano umetusaidia. Viongozi ambao tuliwaamini watusaidie kwenye nyakati ngumu wamefanikisha hilo na tumevuka salama. Bila kusahau mchango wa Viongozi wote wa Matawi, Mashabiki na Wanachama tunasema Asante sana.”.

Hitimisho

Yanga SC msimu wa 2023/24 ilitoa mchezaji bora ambaye ni Aziz Ki. Kiungo huyo kwenye idara yakufunga mabao alikuwa namba moja alipofunga mabao 21. Ilitwaa ubingwa wa ligi wa 30 kibindoni ikiwa ni timu iliyotwaa taji hilo mara nyingi zaidi.

Share this: