Fadlu SimbaFadlu Simba
  • Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC kuna asilimia ndogo kubaki ndani ya kikosi hicho kukinoa kwa msimu wa 2025/26 kutokana na timu kubwa Afrika kuhitaji huduma yake.
  • Simba SC imegotea nafasi ya pili kwenye ligi na katika Kombe la Shirikisho Afrika ni washindi wa pili na mabingwa ni RS Berkane.
  • Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika imempa jina kocha huyo ambaye anawafundisha Jean Ahoua, Ellie Mpanzu miongoni mwa wachezaji wa Simba SC.

Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC asilimia ndogo kubaki katika kikosi hicho kwa msimu wa 2025/26. Kocha huyo amekiongoza kikosi cha Simba SC kwenye mechi 30 za ligi wakigotea nafasi ya pili. Simba SC ina pointi 78 itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Paisha kindege uvune mamilioni sasa hivi

Aviator banner

Paisha kindege uvune mamilioni sasa hivi. Rahisi sana hii na inakupa mamilioni bila chenga. Cheza sasa zamu yako kupaa na kuvuna mamilioni.

Fadlu Davis C
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mchongo huu wa ubingwa Yanga – SportPesa Tanzania

Kocha huyo amekuwa akitajwa kuwa kwenye hesabu za timu mbalimbali Afrika. Alipoulizwa kuhusu kuwepo ndani ya timu hiyo jibu lake liliongeza utata kama atabaki ama hatabaki ndani ya Simba SC. Ikumbukwe kwamba mchezo wa Juni 25 2025, Kariakoo Dabi baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC, wakipishana na ubingwa wa ligi.

Huyu hapa Fadlu Davids anafunguka

“Pongezi kwa Yanga SC nadhani wamekuwa na wachezaji wa mechi kubwa na hilo limekuwa tofauti kwenye siku ya leo. Namna ambavyo Yanga SC wamekuwa, kile ambacho wanakifikiria na kukifanya kwenye mechi kubwa.

Ahoua vs Aucho
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC dhidi ya Khalid Aucho wa Yanga SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25

“Nje na ndani kumekuwa na tofauti kubwa. Ambacho tumeona ni kwamba tumefikia malengo ambayo tulikuwa nayo lakini kuna mambo hayajaenda. Unajua kuna mengi hayajaenda vizuri kwetu hatujafurahia. Ila tuna muda wa kukaa na uongozi kuzungumzia hili kwani unaona aina ya kikosi ambacho tupo nacho.

“Akili katika kutawala mechi kubwa. Kwa msimu huu hatujafurahia na tutakaa na uongozi kuona namna gani tutakwenda mbele. Kikosi ambacho tupo nacho tunahitaji kupata wachezaji wengine bora ambao watakuwa na nguvu na ushindani.

Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB


“Ni mwendelezo wa kutengeneza timu kwa kuwa tumekuwa na vijana ambao wanafanya kazi kubwa. Kuna maono ambayo yapo kwa ajili ya wakati ujao. Tunapaswa kufanya maboresho.

“Labda tumefanikiwa kufikia malengo kulingana na aina ya kikosi ambacho tupo nacho. Tunapaswa kuangalia mbele zaidi katika kutengeneza timu. Tunahitaji nguvu zaidi, uwezo mkubwa na kuwa bora zaidi. Kwa uaminifu zaidi ninaweza kusema kwamba tumefanikiwa.

“Kuwa mshindani mbele ya Yanga SC na kikosi ambacho tupo nacho imekuwa ni jambo kubwa. Ila utaona kwamba kuna wachezaji ambao nilikuja niliwakuta wakiwa katika kikosi. Kuna baadhi ya wachezaji ambao nilikuwepo wakati wanasaini inaweza kuwa watatu hivi kama Mpanzu, Camara, Ateba.

“Tunahitaji muda zaidi, mechi zaidi kuwa imara. Timu mpya na muundo mpya ndani ya Simba SC. Ni muda wa kukaa na kuona kwamba kipi ambacho tutafanya kwa ajili ya wakati ujao. Shukrani kwa mashabiki, uongozi wa Simba SC, Rais Mo amekuwa na maono makubwa.

Fadlu Davids kuhusu kubaki Simba SC msimu ujao


Alipoulizwa na mwandishi wa Azam TV kuhusu uwepo wake msimu ujao wa 2025/26 kifupi alijibu kuwa: “Tutaona”. Jibu hilo limeacha maswali kama kocha huyo atabaki ndani ya Simba SC ama ataondoka.

Timu ambazo zinatajwa kuiwinda saini ya Fadlu

Davids Fadlu
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids. Source: Simba SC.

Inahusiana na hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC anatajwa Raja Casablanca

Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuiwinda saini ya Fadlu ni Raja Casablanca. Ipo wazi kuwa timu hiyo imekwama kufika fainali ya mashindano makubwa Afrika 2024/25. Wanahitaji saini ya kocha huyo ili kuongeza ushindani kitaifa na kimataifa.

Rekodi nzuri alizonazo Fadlu Davids, Raja Casablanca ya Morocco imevutiwa naye. Wanamfuatilia kwa ukaribu kocha huyo ili kufanya naye kazi kwenye msimu ujao wa 2025/26. Kwa kuwa msimu umeisha kuna uwezekano wakaanza mazungumzo.

Mbali na Raja Casablanca kutajwa kuweka ofa mezani kupata huduma ya Fadlu inaelezwa kuwa Esperance De Tunis ya Tunisia. Timu kubwa mbili ambazo zinahitaji saini yake zinaongeza ugumu kubaki. Ni suala la kusubiri namna gani Simba SC wataongeza dau.

Jina la Fadlu limekuwa gumzo ghafla

Kutinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika ni miongoni mwa sababu za jina la Fadlu kukukua. Simba SC ilikuwa haipewi nafasi kutinga fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Mipango na mbinu za Fadlu kwa wachezaji zilijibu ikatinga hatua ya fainali.

Licha yakupoteza mbele ya RS Berkane, bado kulikuwa na ushindani mkubwa. Katika mchezo wa fainali ya kwanza ugenini ilikuwa RS Berkane 2-0 Simba SC na mchezo wa pili ilikuwa Simba SC 1-1 RS Berkane. Simba SC ikagotea nafasi ya pili na RS Berkane mabingwa wa Kombe la Shirikisho.

Fadlu aliweka wazi kuwa walikutana na ugumu mkubwa fainali. Wachezaji walijituma kutafuta matokeo licha ya kukwama. Anaamini wakifanya maboresho makubwa watakuwa bora zaidi wakati ujao.

Share this: