Job DJob D

Yanga SC vs Simba SC mbali na mchezo wa Kariakoo Dabi Juni 25 2025 wana vita nyingine. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kuna vita nyingine kwenye eneo la ulinzi. Hizi zinaingia kwenye orodha ya timu ambazo zimefungwa mabao machache ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa. Ukiweka kando kuruhusu mabao machahe zimefunga mabao mengi pia. Katika raundi ya 29 timu zilizo tatu bora zilikusanya mabao 5-0 dhidi ya wapinzani wao.

Diara
Diara kipa namba moja wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC kwenye msako wa pointi tatu ndani ya ligi Juni 18/ Mechi namba 184 kimbembe

Hapa tunakuletea timu tano ambazo zimeruhusu mabao machache kwenye ligi. Wapinzani wao ni muhimu kujipanga kuvunja ngome za ulinzi za timu hizo kutokana na uimara walionao kwenye kutimiza majukumu. Hizi hapa timu tano namna hii:-

Yanga SC – 10

Job
Job beki wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Ligi Kuu Bara Juni 22 mzunguko wa 30

Kwenye msimamo wa ligi Yanga SC ni namba moja chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, chini ya nahodha msaidizi Dickson Job timu hiyo imeruhusu jumla ya mabao 10 kufungwa msimu wa 2024/25 ikiwa ni timu namba moja kufungwa mabao machache kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika.

Safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Clement Mzize na Prince Dube ambao ni washambuliaji hawa wote wawili wametupia mabao 13 kila mmoja. Ipo wazi kwamba Yanga SC inaongoza ligi na timu yenye mabao mengi. Mchezo wa mzunguko wa 29 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ulisoma Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC.

Kipa namba moja wa Yanga SC ni Djigui Diarra. Kipa huyo kwa msimu wa 2024/25 amekusanya hati safi 16 ndani ya ligi kuu bara ambayo ni namba nne kwa ubora. Amekaa langoni kwenye jumla ya mechi 22 akikomba dakika 1,980. Mabao ambayo kafungwa ni 8 na mabao mawili ni Khomeiny alifungwa dhidi ya Mashujaa FC mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Simba SC-11

Camara Moussa
Camara Moussa, kipa namba moja wa Simba SC. Source: Simba SC.

Licha ya makosa ambayo safu ya ulinzi imekuwa ikifanya yale yanayojirudia bado kazi kubwa ilifanyika kwa mlinda mlango Moussa Camara ambaye alikaa langoni kwenye mechi 26 akikusanya hati safi 18 alifungwa kwenye mechi tatu.

Baada ya kucheza mechi 28 ambazo ni dakika 2,520 ilipoteza mchezo dhidi ya Yanga SC mzunguko wa kwanza. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga SC. Pointi tatu zilikuwa za Yanga SC mzunguko wa pili Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa Juni 25 2025. Ilishinda mabao 5-0 dhidi ya KenGold raundi ya 29.

Azam FC-17

Matajiri wa Dar, Azam FC kwenye msimamo wa ligi wamekusanya pointi zao 60 nafasi ya tatu na pia kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ndani ya ligi ni namba tatu ikiwa imeruhusu mabao 17 pekee kwenye mechi 29 ambazo ni dakika 2,610.

Msindo P
Msindo Pascal, beki wa Azam FC. Source: Azam FC.

Soma hii: Azam FC 5-0 Tabora United Ligi Kuu Bara 2024/25 balaa zito

Vita yao kugotea nafasi ya tatu dhidi ya Singida Black Stars wameimaliza kwa kuwa hapo ndipo watagotea. Ushindi waliopata wa mabao 5-0 dhidi ya Tabora United umewahakishia kuwa ndani ya tatu bora na itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa.

Tabora United ipo ndani ya tano bora ikiwa nit imu namba moja kufungwa mabao mengi. Kwenye timu ambazo zipo katika tano bora, Tabora United baada ya mechi 29 ni mabao 44 imefungwa ikiwa na pointi 37. Inavutwa shati na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 6 na pointi zake ni 35.

Singida Black Stars-23

Screenshot----------------sportpesa-co-tz

Ina uhakika wa kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika. Ni Singida Black Stars ambayo inatumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani. Jumla imefungwa mabao 23 ikiwa ni miongoni mwa timu ambazo zimefungwa mabao machache.

Singida Black Stars mchezo wake uliopita ilivuna pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji. Mchezo huo ulichezwa Juni 18 2025 na ubao ulisoma Dodoma Jiji 1-2 Singida Black Stars. Kete ya kufunga mzunguko wa 30 kwa Singida Black Stars itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons. Ikumbukwe kwamba Tanzania Prisons mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu kwa kufungwa mabao 5-0 na kuacha pointi tatu mazima zikienda Jwangwani kwa vinara wa ligi msimu wa 2024/25.

JKT Tanzania-27

Wajeda hawa ndani ya ligi wameonyesha ushindani mkubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja. Itakumbukwa mechi yao ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba SC, Uwanja wa KMC Complex walikaza na dakika za jioni Simba ikapata penalty na mtupiaji alikuwa Jean Ahoua dakika ya 90. JKT Tanzania ni mabao 27 imefungwa ikiwa namba tano kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache kwenye msimamo ipo nafasi ya  6 ikiwa na pointi zake 35 ndani ya msimu wa 2024/25.

Mchezo wa funga kazi kwa msimu wa 2024/25 JKT Tanzania itakuwa Uwanja wa Lake Tanganyika. JKT Tanzania itakuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu dhidi ya Mashujaa mwisho wa reli Kigoma. Mashujaa FC kwenye msimamo ni nafasi ya 7 ikiwa na pointi 34 baada ya mechi 29.

Share this: