Jean Ahoua --Jean Ahoua --
  • Tuzo ya ufungaji bora vita yake inazidi kuchangamka ndani ya uwanja msimu wa 2024/25 kwa wachezaji kufanya kweli dakika 90.
  • Kariakoo Dabi inayotarajiwa kucheza Juni 25 2025, Yanga SC vs Simba SC kumaliza utata wa nani atakuwa shujaa.
  • Jean Ahoua ujanja wake ni kwenye mguu wa kulia na akiwa ndani ya 18 kuwaliza makipa ndani ya ligi.

Tuzo ya ufungaji bora vita yake inazidi kuchangamka kutokana na ushindani uliopo 2024/25. Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC ameshikilia chati huku nyota wa Yanga SC Clement Mzize akiwa ni mzawa aliyefanya kazi kubwa kwenye eneo la ushambuliaji kwa kufunga mabao zaidi ya 10 ndani ya uwanja. Aziz Ki alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2023/24.

Aziz Stephan
Aziz Stephan

Soma hii: Ufungaji bora 2024/25 orodha ya waliopo kwenye vita

Bado haijafahamika nani atatwaa tuzo hiyo kwa kuwa kuna mechi ambazo zinatarajiwa kuchezwa Juni 22 2025 hizi zitatoa picha ya mshindi wa tuzo ya ufungaji bora. Kariakoo Dabi mchezo unaotarajiwa kuchezwa Juni 25 Uwanja wa Mkapa huu utaamua nani atakuwa nani kwenye kila idara. Hapa tunakuletea orodha ya wafungaji vinara katika kucheka na nyavu namna hii:- 

Jean Ahoua wa Simba SC mabao 16

Jean C- Ahoua
Jean Ahoua kinara wa utupiaji akiwa na mabao 16. Source: Simba SC.

Soma hii: KenGold FC 0-5 Simba SC: magoli yote, uchambuzi, mnara umesoma 5G Tabora

Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC, raia wa Ivory Coast anaongoza kwenye orodha akiwa na mabao 16. Ingizo hili jipya ndani ya kikosi cha Simba SC limekuwa kwenye mwendelezo mzuri katika kufunga. Kwenye mabao 16 ambayo kafunga, katumia mguu wa kulia kufunga mabao 15 na pigo la kichwa ni bao moja alifunga dhidi ya Pamba Jiji, Uwanja wa KMC Complex.

Clement Mzize wa Yanga SC, mabao 13

Clement Mzize wa Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ni namba mbili kwenye orodha ya vinara katika ufungaji. Mzize kafunga mabao 13. Yanga SC baada ya mechi 28 imetupia mabao 76. Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Juni 18 2025 alimpa pasi ya bao Clatous Chama dakika ya 35.

Prince Dube wa Yanga mabao 13

Clement Mzize na Dube
Clement Mzize na Dube washambuliaji wa Yanga SC wenye mabao 13 msimu wa 2024/25. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB sasa kupigwa Juni 29, Zanzibar 28/06/2025 – SportPesa Tanzania

Prince Dube mshambuliaji wa Yanga kafunga mabao 13 yeye ni raia wa Zimbabwe. Ukurasa wa mabao wa Dube ulifunguliwa kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa FC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Ni mabao matatu alifunga akiwa nyota wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi.

Leonel Ateba wa Simba SC mabao 13

Ateba raia wa Cameroon amefunga jumla ya mabao 13. Kwenye mabao hayo Ateba alipachika mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Mei 8 2025. Bao lake la 13 alifunga kwenye mchezo dhidi ya KenGold, Juni 18 2025, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Steven Mukwala wa Simba SC mabao 12

Mshambuliaji wa Simba SC, Steven Mukwala yeye amefunga jumla ya mabao 12 ni raia wa Uganda. Simba SC baada ya kucheza mechi 28 imefunga jumla ya mabao 68 ikiwa ni timu namba mbili kufunga mabao mengi ndani ya ligi.

Jonathan Sowah wa Singida Black Stars mabao 12

Screenshot----------------sportpesa-co-tz

Raia huyu wa Ghana yupo ndani ya Singida Black Stars akiwa katupia jumla ya mabao 12. Ni miongoni mwa washambuliaji wenye nguvu kubwa kwenye kutumia nafasi ambazo anazipata ndani ya uwanja na mguu wake wenye hatari zaidi ni ule wa kulia.

Elvis Rupia wa Singida Black Stars mabao 10

Mshambuliaji wa Singida Black Stars Elvis Rupia kwenye chati ya ufungaji ni mabao 10 kafunga ndani ya ligi. Huyu ni raia wa Kenya ambaye ana zali la kucheka na nyavu. Singida Black Stars imefunga mabao 42 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi 56.

Pacome Zouzoua wa Yanga SC-11

Kiungo mshambuliaji wa Pacome Zouzoua kafunga jumla ya mabao 11. Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alifunga mabao mawili na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo Juni 18 2025 kwenye mzunguko wa pili.

Yanga SC ikiwa imefunga mabao 76 yeye kahusika kwenye mabao 20 akifunga mabao 11 na kutoa pasi za mabao 9 ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika. Yanga SC nit imu namba moja kwenye kufunga mabao mengi.

Tuzo mikononi mwa Aziz Ki

Msimu wa 2023/24 tuzo ya ufungaji bora ilichukuliwa na Aziz Ki wa Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa lig. Aziz Ki atapishana na tuzo hiyo kwa kuwa amesajiliwa na Wydad Casabalanca alihusika kwenye mabao 29 kati ya 71. Alifunga mabao 21 na kutoa pasi 8 za mabao.

Nyota ambaye alikuwa akimpa ushindani wa karibu alikuwa Feisal ambaye alihusika kwenye mabao 26 kati ya 63. Kwa msimu wa 2024/25 kiungo Feisal ni namba moja kwenye eneo la kutengeneza pasi za mwisho akiwa nazo 13 huku eneo la utupiaji akiwa hajaonyesha ubora wake kwa ukubwa katika kuifikia rekodi yake mwenyewe akiwa kafunga mabao manne.

Share this: