Sopu na SillahSopu na Sillah
  • Azam FC 5-0 Tabora United Ligi Kuu Bara 2024/25 balaa zito, wafunga biashara Uwanja wa Azam Complex.
  • Vita ya Yanga SC vs Simba SC inaendelea kufukuta kabla ya Kariakoo Dabi inayotarajiwa kuchezwa Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.
  • Gibrill Sillah kiungo mshambuliaji wa Azam FC hakamatiki kutokana na kasi yake kwenye kucheka na nyavu.

Azam FC 5-0 Tabora United Ligi Kuu Bara 2024/25 balaa zito kwa wababe waliopo ndani ya tatu bora kutokana na matokeo yao kuwa na mfanano mzunguko wa 29. Ni mchezo mmoja umebaki kwa Azam FC kukamilisha mzunguko wa pili kwenye msako wa pointi tatu muhimu ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 60.

Yahya
Yahya Zayd nyota wa Azam FC akipambana dhidi ya Tabora United, Juni 18 2025. Source: Azam FC.

Soma hii: Wakali wa pasi za mwisho Bongo 2024/25 – SportPesa Tanzania

Mchezo wa mwisho kwa Azam FC itakuwa dhidi ya Fountain Gate iliyo nafasi ya 14 na pointi 29 baada ya kucheza mechi 29 unatarajiwa kuchezwa Juni 22 2025. Ikumbukwe kuwa Fountain Gate imetoka kupoteza mchezo wake uliopita Juni 18 2025 kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ukisoma Coastal Union 1-0 Fountain Gate.

Mchezaji bora wa mchezo atoa ya moyoni

Azam FC kwenye ubora wao walianza kwa kasi ndani ya dakika 20 walikuwa wamepachika mabao mawili jambo ambalo liliwapa tabu wapinzani wao Tabora United. Kipa ambaye alianza Seleman Fikiri alikuwa anafikiria namna ya kuokoa jahazi na mwisho wakapishana na pointi tatu mazima.

Nyota wa Azam FC, Gibrill Sillah ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo wa ligi Juni 18 2025 dhidi ya Tabora United amebainisha kuwa haikuwa kazi rahisi kupata ushindi katika mchezo huo kutokana na kila timu kupambania pointi tatu.

“Kila timu ilikuwa inahitaji kupata pointi tatu unajua hivyo tulifanya kazi kutimiza majukumu yetu na tunamshukuru Mungu imekuwa hivyo. Ushindi ambao tumepata ni muhimu kwetu na mashabiki na tuzo hii ninashukuru kwa kupata.”

Balaa lilikuwa kwenye mwendo huu Azam FC 5-0 Tabora United

Ni Sopu alifungua ukurasa kwa kupachika bao moja dakika ya 11 akitumia pasi ya Pascal Msindo likiwa ni bao lake la pili ndani ya ligi msimu wa 2024/25. Ikumbukwe kwamba Mei 13 2025, baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 5-0 Dodoma Jiji, Sopu alifungua ukurasa wa mabao kwa kufunga bao moja na alitoa pasi moja alimpa Lusajo Mwaikenda ilikuwa dakika ya 5

G- Sillah
Sillah kiungo mshambuliaji wa Azam FC. Source: Azam FC.

Soma hii: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya

Ukiweka kando Sopu ambaye alifunga bao moja kwenye mchezo huo huku Sillah akifunga mabao mawili dakika ya 16 na dakika ya 26 yote akitumia mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18, Idd Nado alipachika bao moja dakika ya 45 na Nassoro Saadun alipachika bao moja dakika ya 89.

Mabao mengine ya Azam FC kwenye mchezo dhidi ya Tabora United yalifungwa na Gibril Sillah ambaye alifunga mabao mawili dakika ya 16 na dakika ya 29 akifikisha mabao 11 na pasi zake ni mbili. Idd Nado alipachika bao moja dakika ya 45 na alitoa pasi moja kwa Sillah dakika ya 29 naye alihusika katika mabao mawili mfungaji wa kwanza ndani ya Azam FC kwenye mechi za ligi alipofungua ukurasa huo mbele ya KMC Complex,

Nassoro Saadun alipachika bao moja dakika ya 89 akitumia pasi ya Sopu, Saadun ndani ya ligi anafikisha mabao 8 na pasi nne za mabao ndani ya Azam FC, msimu wa 2024/25. Amehusika kwenye mabao 12 kati ya 53 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo ndani ya tatu bora.

Mabao yaliyofungwa ni 22 mzunguko wa 29

KenGold FC vs Simba SC 'live'

Baada ya dakika 90 kukamilika mzunguko wa 29 jumla yamefungwa mabao 22 kutoka katika viwanja 8 tofautitofauti msimu wa 2024/25. Mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa dakika 90 ziligota mwisho bila kupatikana kwa bao kwa timu zote mbili na ubao ulisoma Namungo FC 0-0 Kagera Sugar.

Timu mbili zilikomba pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0, ilikuwa Pamba Jiji 1-0 JKT Tanzania bao la ushindi likifungwa na Zabona Mayombya ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
 Coastal Union 1-0 Fountain Gate kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga pointi tatu zikiwa ni mali ya Coastal Union.

Yanga SC vs Simba SC vita yao inaendelea

Ateba v Aucho
Mudathir Yahya wa Yanga SC na Aucho wakipambana na Ateba wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: KenGold FC 0-5 Simba SC: magoli yote, uchambuzi, mnara umesoma 5G Tabora

Vita ya watani wa jadi, Yanga SC vs Simba SC ambao wanatarajia kukutana kwenye mchezo wa ligi Juni 25 inaendelea kutokana na kasi yao kuwa kubwa kwenye eneo la kufunga na kusepa na pointi tatu muhimu. Juni 18 2025, wababe hawa wawili wote walikomba pointi tatu kwenye mechi zao kwa ushindi wa mabao 5-0, ilikuwa Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC na KenGold 0-5 Simba SC.

Pointi ambazo wanazo wababe hawa tofauti yao ni moja, Yanga SC ni pointi 76 imekusanya na Simba SC ina pointi 75 zote zikiwa zimecheza mechi 28 msimu wa 2024/25. Dakika 75 iliandika rekodi ya watani haw awa jadi kukamilisha ushindi wao wa mabao 5-0 dhidi ya wapinzani wao.

Kwa Simba SC bao la ufunguzi lilifungwa na kiungo Kibu Dennis dakika ya 20 huku kwa Yanga SC bao la ufunguzi likifungwa na kiungo Mudathir Yahya. Bao la funga kazi kwa Simba SC lilifungwa na kiungo Jean Ahoua dakika ya 75 na bao la funga kazi kwa Yanga SC lilifungwa na Pacome dakika ya 75.

Share this: