- Simba SC kwenye mtihani mzito kuwakabili KenGold, matatizo ya wapinzani hao yapo kwenye eneo la ushambuliaji.
- KenGold haitashiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2025/26 baada yakushuka daraja mazima kabla msimu kugota mwisho.
- Kibu Dennis, Jean Ahoua kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji walikosa nafasi za wazi kufunga mabao.
Simba SC kwenye mtihani mzito kuwakabili KenGold Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni mzunguko wa pili kukamilisha dakika 180. Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba SC ilivuna pointi tatu baada ya dakika 90 mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Soma hii: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya
Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema licha ya KenGold kushuka daraja wataingia kwa tahadhari kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja kwa kuwa wapinzani wao wapo imara katika kutafuta matokeo chanya.
“Tunawaheshimu wapinzani wetu licha yakushuka daraja tunaamini ni timu imara hivyo tutaingia uwanjani kwa ajili yakusaka pointi tatu muhimu. Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu muhimu. Tunapambana kwa ajili yakuona tunavuna pointi tatu muhimu dhidi ya wapinzani wetu”
Msimamo wa KenGold vs Simba SC
KenGold kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 28 msimu wa 2024/25. Tayari KenGold imeshuka daraja hivyo msimu wa 2025/26 itashiriki Championship. Ushindi ni kwenye mechi tatu ndani ya msimu wa 2024/25 ilipata KenGold ambayo ilipanda daraja msimu wa 2023/24 huku ikiambulia sare kwenye jumla ya mechi 7 ndani ya ligi.
Safu ya ushambuliaji ya KenGold haijawa imara kwenye eneo la kutupia ambapo ni mabao 22 pekee imefunga kwenye mechi 28 ambazo imecheza kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika ambayo ushindani wake umekuwa ni mkubwa.
Simba SC ipo nafasi ya pili pointi 72 baada ya mechi 27 ikiwa inapambania kutwaa ubingwa mbele ya Yanga SC ambao ni vinara wenye pointi 73. Tofauti ya wababe hawa wawili ni pointi moja pekee wakiwa wamecheza mechi ambazo ni sawa kwa kila mmoja.
Kwa upande wa mabao Simba SC imefunga mabao 63 inakutana na KenGold ambayo imefunga jumla ya mabao 22. KenGold reodi zinaonyesha kuwa safu yake ya ushambuliaji haijawa imara kwenye mechi za ushindani.

Mbali na kufunga mabao machache KenGold imeruhusu mabao 52 yakufungwa ikiwa ni timu namba mbili kuruhusu mabao mengi yakufungwa ndani ya ligi vinara wakiwa ni Fountain Gate ambao wameruhusu jumla ya mabao 54 baada ya mechi 28.
Mzunguko wa kwanza walipokutana
Wababe hawa wawili mzunguko wa kwanza walipokutana Desemba 18 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba SC 2-0 KenGold pointi zilibaki kwa Simba SC. KenGold kwenye mechi 28 ambazo walishuka uwanjani wakiwa na ushindi wa mechi 7, walipoteza mechi 18 ambapo katika hizo mechi hizo moja walipoteza dhidi ya Simba SC kwenye mzunguko wa kwanza.
Uimara wa Simba SC ndani ya uwanja
Simba SC kwenye mechi za ugenini imekuwa imara ambapo haijapoteza mchezo hata mmoja hivyo KenGold wanakazi kubwa kutibua rekodi hiyo ndani ya dakika 90 kwenye msako wa pointi tatu muhimu. Katika eneo la ushambuliaji Simba SC imefunga mabao 63 na kinara wa utupiaji ndani ya kikosi cha Simba SC ni Jean Ahoua mwenye mabao 15 ndani ya ligi namba nne kwa ubora akiwa ametoa pasi nane za mabao.
Eneo la ulinzi Simba SC wamekuwa imara ambapo ni namba mbili kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ambayo ni 11 baada ya mechi 27 msimu wa 2024/25. Mabao yote hayo alifungwa kipa namba moja Moussa Camara.
Timu namba moja kwenye eneo la ufungaji ni Yanga SC ambayo imetupia mabao 71 baada yakucheza mechi 27. Hii inaongoza pia kwa timu ambazo hazijafungwa mabao mengi ikiwa imefungwa mabao 10 pekee kwenye mechi za ushindani.
Kwa upande wa KenGold eneo ambalo imekuwa imara ni kwenye mashambulizi ya kushtukiza ambapo iliwahi kuwafunga Yanga SC kwa bao la haraka kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, licha yakupishana na pointi tatu muhimu walifanikiwa kufunga bao moja.
Matatizo ya KenGold na Simba SC

Soma hii: KenGold FC vs Simba SC ‘live’: H2H, vikosi, moto utawaka, Simba watoa tamko zito leo
Kwenye eneo ambalo KenGold wamekuwa na tatizo ndani ya ligi ni eneo la ulinzi ambapo safu yao inaingia kwenye orodha ya timu zilizofungwa mabao mengi ndani ya ligi. Mabao 52 kwa mechi 28 yanatoa picha kuwa kumekuwa na tatizo kwenye umakini katika eneo la ulinzi.
Mbali na eneo la ulinzi kwenye kupata ushindi, KenGold wanapambana hali iliyopelekea kuvuna pointi tatu mazima kwenye mechi tatu pekee ikiwa ni timu namba moja kuvuna pointi tatu kwenye timu chache ndani ya ligi.
Mbali na kuongoza kwenye timu iliyopata ushindi kwenye mechi chache ambazo ni tatu, inaongoza kupoteza kwenye mechi nyingi ambazo ni 18 ndani ya msimu wake wa kwanza kwenye ligi. Simba SC ni kwenye eneo la ufungaji, washambuliaji wa timu hiyo wamekuwa wakikosa nafasi nyingi za wazi ndani ya uwanja, rejea mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Kibu Dennis na Jean Ahoua walikosa nafasi zaidi ya mbili kufunga kwenye mchezo huo.

Soma hii:Yanga SC vs Simba SC kwenye msako wa pointi tatu ndani ya ligi Juni 18/ Mechi namba 184 kimbembe
Kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate wakiwa ugenini,mawasiliano kati ya Leonel Ateba na Steven Mukwala yalikosekana jambo lililopelekea wakagongana wakiwa ndani ya 18 nakukwama kufanya jaribio kuelekea langoni.

