Fei utambulishoFei utambulisho
  • Simba SC wamefungukia kuiwinda saini ya Feisal Salum kiungo wa Azam FC mwenye uwezo wa kufunga na kutoa pasi za mabao.
  • Yanga SC waajiri wake wa zamani wanatajwa kuwa vitani kuwania pia saini ya kiungo huyo anayevaa jezi namba sita.
  • Feisal Salum rekodi zake hazikamatiki ndani ya uwanja, msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Azam FC alifunga mabao 19.

Simba SC wamefungukia ishu ya kuiwinda saini ya Feisal Salum kiungo wa Azam FC ambaye tetesi zinaeleza kuwa timu zenye maskani yao Kariakoo ambazo ni Simba SC mtaa wa Msimbazi na Yanga SC mtaa wa Jangwani. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wanatambua namna utaratibu ulivyo ikiwa watahitaji kupata saini ya mchezaji.

Fei Toto
Fei Toto kiungo wa Azam FC. Source: Azam FC.

Soma hii: Fei Toto kusaini Simba au Yanga? Tetesi usajili Bongo, Ulaya

Feisal alisajiliwa na matajiri wa Dar, Azam FC Juni 8 2023 kwa kandarasi ya miaka mitatu akitokea katika kikosi cha Yanga SC bado ni mali ya matajiri hao mkataba wake ukiwa umesalia mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo. Jina lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kuwa katika rada za Simba SC na Yanga SC.

Ahmed amebainisha kuwa hakuna timu ambayo haitahitaji kuwa na mchezaji kama Feisal lakini kwa sasa ipo wazi ana mkataba na timu ya Azam FC hivyo hawataweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa kanuni za mpira wa miguu haziwapi ruhusa kuzungumza kuhusu mchezaji ambaye ana mkataba na wao wanazitambua kanuni.

Rekodi za Fei Toto msimu wake wa kwanza Azam FC

 Fei Toto msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Azam FC 2023/24 alikuwa kwenye ubora wake akifanya kazi kubwa katika kutimiza majukumu yake ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani. Zama hizo Kocha Mkuu wa Azam FC alikuwa Yusuph Dabo, Azam FC iligotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na Feisal alikuwa ni chaguo la kwanza.

Ikumbukwe kwamba timu hiyo ilimaliza msimu ikiwa na pointi 69 baada ya kucheza mechi 30 ambapo ilikuwa inapambania nafasi ya pili na Simba SC iliyokuwa inanolewa na Juma Mgunda kwa zama hizo. Ni tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa yaliwatenganisha wababe hao wawili.

Toto Fei
Msimu wa 2024/25 Fei Toto ametoa jumla ya pasi 13 za mabao. Source: Azam FC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC majina yao yametawala ufungaji bora 2024/25

Kwenye kasi ya ufungaji ni mabao 63 Azam FC ilifunga huku ile ya Simba SC ikifunga mabao 59 na katika ulinzi ni mabao 25 Simba SC iliruhusu kufungwa na Azam FC ni mabao 21 ilifungwa msimu wa 2023/24 ndani ya ligi na wakapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Makali ya Fei Toto yalikuwa hivi

Kiungo Fei aliwaka kwa kuwa namna alivyoanza msimu ndivyo alivyomaliza. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza akiwa na uzi wa Azam FC ilikuwa dhidi ya Tabora United, Uwanja wa Azam Complex kwenye mchezo huo alifungua akaunti ya mabao na alifunga hat trick akiwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.

image

 Mchezo wa mwisho kwa msimu ilikuwa dhidi ya Geita Gold alifunga bao moja na kufikisha jumla ya mabao 19 kwenye ligi akiwa mzawa mwenye mabao mengi kwa viungo washambuliaji Bongo. Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Aziz Ki alikuwa mfungaji bora alipofunga mabao 21.

Alifunga mabao 17 akiwa ndani ya 18 hivyo alikuwa na hatari kubwa akiwa kwenye eneo hilo na alifunga mabao mawili akiwa nje ya 18 kiungo huyo ambaye aliibuka Azam FC akitokea Yanga SC. Msimu wa kwanza alifunga akiwa miongoni mwa nyota waliokuwa kwenye kikosi bora cha msimu.

Huyu hapa msimu wa 2024/24 ndani ya Azam FC

Feisal msimu wa 2024/25 amekuwa imara kwenye eneo la pasi za mwisho akiwa ni namba moja kwa wachezaji katika ligi namba nne kwa ubora Afrika. Ni pasi 13 za mabao ametoa ndani ya ligi. Mbali na kutoa pasi 13 za mabao amefunga mabao manne na yote alitumia mguu wa kulia. Katika mabao 48 ambayo timu ya Azam FC imefunga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 57 kahusika kwenye mabao 17.

Simba SC tamko lao kuhusu Fei Toto

Kutokana na tetesi kueleza kuwa Simba SC inahitaji saini ya kiungo huyo, uongozi wa Simba SC kupitia kwa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ahmed Ally umeweka wazi kuwa unatambua kwamba mchezaji huyo ana mkataba na Azam FC hivyo hawawezi kumzungumzia kwa kuwa kanuni haziwaruhusu.

ahmedally------------------------------------------
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Dickson Job beki wa Yanga SC anatajwa Simba SC

“Hatuwezi kuzungumzia kuhusu mchezaji ambaye ana mkataba na timu nyingine, Feisal Salum tunajua kwamba ana mkataba na timu yake ya Azam FC na sisi kama watu ambao tunafahamu kanuni na sheria za mpira wa miguu hatuwezi kuzungumzia mchezaji mwenye mkataba. Tunafahamu namna gani tufanye tukishafanikiwa hapo tunaweza kumzungumzia.

 “Ambacho tunajua kwa sasa ni kwamba bado ana mkataba na sisi hatuwezi kuzungumzia mchezaji ambaye ana mkataba. Kama tutakuwa tunahitaji saini yake hilo linajulikana kuwa kuna namna ambayo ipo na utaratibu unapaswa kufuata kwa kuwa kwa sasa bado ana mkataba na Azam FC kuna utaratibu ambao unapaswa kufuatwa.

“Tukishafanikiwa kumpata kama tukifuata utaratibu hapo tutaruhusiwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari na sheria haziruhusu kumzungumzia mchezaji ambaye bado ana mkataba na timu yake. Hayo yote yanayosemwa yabaki kuwa matamanio tu bado ni mchezaji wa watu ana mkataba na timu nyingine kwa sasa. Ninachoweza kusema ni kuwa kila timu inapenda kuwa na mchezaji kama Feisal Salum.” Alisema Ahmed kupitia Azam TV.

Share this: