Aziz KiAziz Ki
  • Stephane Aziz Ki huyoo Marekani kuwavaa Manchester City kwenye mashindano ya klabu bingwa ya dunia ya Guardiola.
  • Leo Jumanne msafara wa wachezaji 55 na maofisa mbalimbali wa timu ya Wydad Casablanca wamesafiri kwenda nchini Marekani.
  • Mashindano ya Kombe la Dunia la klabu yanatarajia kuanza kutimua vumbi rasmi Juni 15, mwaka huu.
  • Katika mashindano hayo Wydad AC wamepangwa katika Kundi G pamoja na; Manchester City, Juventus, na Al Ain.

Kiungo wa kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki huyoo Marekani kuwavaa Manchester City kuanza ukurasa mpya wa maisha ya soka ndani ya Wydad AC ya Morocco, ambapo leo Jumanne amekuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichosafiri kwenda nchini Marekani.

Aziz Ki, Mwalimu kupeperusha bendera ya Tanzania Marekani

Msafara wa Wydad AC
Msafara wa Wydad AC

Leo Jumanne msafara wa wachezaji 55 na maofisa mbalimbali wa timu ya Wydad Casablanca wamesafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya ushiriki wao katika mashindano ya Kombe la Dunia la klabu ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi rasmi Juni 15, mwaka huu.

Katika msafara, Aziz Ki pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Selemani Mwalimu ni wanatarajia kuibeba taswira ya Tanzania, hii ni kutokana na mafanikio makubwa ambayo nyota hao wawili wamekuwa nayo kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.

Ikumbukwe Mwalimu alijiunga na Wydad AC mara baada ya kuuwasha moto akiwa na kikosi cha Fountain Gate FC, huku Aziz Ki akijiunga na Wydad akitokea ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga ambayo amedumu kwa misimu mitatu.

SOMA HII PIA: Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo

Safari ya Aziz Ki ndani ya Wydad AC

Kama sehemu ya pendekezo la aliyekuwa kocha wa Wydad AC, Rhulani Mokwena mnamo Mei 2025, Wydad AC walithibitisha rasmi kumsajili Aziz Ki kwa mkataba wa miaka miwili. Kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Klabu la Dunia.

Wydad AC ni miongoni mwa timu nne kutoka Afrika ambazo zimepata nafasi ya kushiriki Kombe la Klabu la Dunia la 2025 litakalofanyika nchini Marekani kutoka Juni 15 hadi Julai 13. Mashindano haya yamepanuliwa na sasa yanashirikisha timu 32 kutoka mabara yote.

Wydad yapangwa na Manchester City, Juventus kundi G

Man City
Man City

Katika mashindano hayo Wydad AC wamepangwa katika Kundi G pamoja na; Manchester City, Juventus, na Al Ain. Hivyo ikiwa atapata nafasi ya kucheza Aziz Ki anatarajiwa kuvaana na timu mbili zenye heshima kubwa kwenye soka duniani.

SOMA HII PIA: Clement Mzize anafuata kuondoka Yanga SC baada ya Aziz Ki, sababu zatajwa

Changamoto na Fursa kwa Aziz Kin a Mwalimu

Kushiriki katika Kombe la Klabu la Dunia ni fursa kubwa kwa Aziz Ki na Mwalimu ili kuonyesha uwezo wao katika jukwaa la kimataifa. Hata hivyo, watakutana na changamoto kubwa kutokana na upinzani kutoka kwa timu kubwa za Ulaya na Asia.

Ratiba ya kundi G, Wydad AC kufungua dimba na Manchester City

Katika mshikemshike wa kundi G, Wydad AC itaanza kuchanga karata zake kwa kuvaana na Manchester City ambapo ratiba nzima ni kama ifuatavyo;

Juni 18, 2025: Wydad AC vs Manchester City – Lincoln Financial Field, Philadelphia.

Juni 22, 2025: Wydad AC vs Juventus – Lincoln Financial Field, Philadelphia.

Juni 26, 2025: Wydad AC vs Al Ain – Audi Field, Washington, D.C.

Ikiwa watafanikiwa kumaliza katika nafasi mbili za juu za kundi lao, Wydad AC itakata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano, ambapo mechi za robo fainali zitachezwa kati ya Juni 30 na Julai 1, 2025. Fainali ya mashindano hayo imepangwa kufanyika Julai 13, 2025, kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey.

Wachezaji muhimu wa Wydad AC

Stephane Aziz Ki huyoo Marekani kuwavaa Manchester City
Wydad

Ukiachana na Aziz Ki na Mwalimu, Wydad AC ina wachezaji kadhaa wenye uwezo mkubwa, wakiwemo Amrabat, Nassim Chadli, Hamza Sakhi, Walid Nassi, na Mohamed Rayhi. Chadli, ambaye ni mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji.

Nyota hawa wameonyesha kiwango bora katika michuano ya ndani na kimataifa katika misimu ya hivi karibuni. Wachezaji hawa wanatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika michuano ya Kombe la Klabu la Dunia.

SOMA HII PIA: Aziz Ki anaondoka Yanga SC kusaini Wydad AC, Simba SC yatajwa

Hitimisho

Safari ya Wydad AC kwenda Marekani kwa ajili ya Kombe la Klabu la Dunia la 2025 ni ishara ya mafanikio ya soka ya Morocco na Afrika kwa ujumla. Kwa kuzingatia uwezo wa wachezaji wao na mabadiliko ya kiufundi yaliyofanywa kupitia usajili mkubwa waliofanya.

Wydad AC inatarajiwa kuwa na michuano ya kuvutia na yenye ushindani mkubwa. Mashabiki wa soka duniani kote watafuatilia kwa karibu michuano hii, wakitarajia kuona ubora na nguvu ya ushindani kutoka kila bara.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.