- Sakata la Yanga SC na hela za ubingwa wa CRDB Federation Cup 2023/24 limezua balaa kwa kuibua mapya kuhusu malipo na matumizi.
- CRDB wabainisha namna walivyokamilisha malipo ya zawadi kimkataba kuelekea kwa TFF.
- TFF watoa tamko na kuwaita Yanga SC asubuhi ofisini wakiwa na vielelezo vyote kufanya ukaguzi wa masuala ya fedha.
Sakata la Yanga SC na hela za ubingwa CRDB Federation Cup 2024 lazua balaa. Yanga SC wamebainisha kuwa mpaka watakapopewa hela ya ubingwa ya msimu uliopita watacheza fainali jambo ambalo limewaibua wadhamini na mamlaka ya soka Tanzania, (TFF) kubainisha ukweli wote wa suala hilo.

Soma hii: Yanga SC wametoa matakwa manne yakitimizwa Kariakoo Dabi kuchezwa
Ipo wazi kwamba Yanga SC ina kibarua cha kucheza mchezo wa fainali dhidi ya Singida Black Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Juni 28 2025, Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Yanga SC imetwaa taji hilo mara nne na imetinga fainali yake ya tano kutetea taji lake kwa mara nyingine tena.
Yanga SC walitinga fainali hiyo baada ya kuwafungashia virago JKT Tanzania kwa ushindi wa mabao 2-0 huku Singida Black Stars wao wakitinga fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Simba SC kwenye hatua ya nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.
Hatuchezi ya Yanga SC iliibuka hapa
Ikumbukwe kwamba Juni 9 2025, Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa hawatacheza mchezo wa fainali ya CRDB mpaka watakapolipwa hela ya ubingwa waliotwaa msimu uliopita. Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ilitwaa taji la CRDB Federation Cup mbele ya Azam FC kwenye fainali iliyochezwa Zanzibar kwa ushindi wa penati 6-5. Penati ya Azam FC iliyowapa ubingwa Yanga SC mpigaji alikuwa ni Idd Nado.

Soma hii:Yanga SC vs Simba SC iliyopangwa Juni 15 2025: Ngoma imekuwa ngumu, Yanga yatishia maamuzi magumu
Pigo lake Nado lilipaa mazima kwenye mchezo huo ambapo langoni alianza Djigui Diarra kipa namba moja wa Yanga SC na kwa upande wa Azam FC ni Mustapha alianza langoni aliokoa penati iliyopigwa na Aziz Ki ambaye hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/25.
Aziz Ki ambaye mchezo wake wa mwisho ilikuwa kwenye hatua ya nusu fainali dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani Tanga yeye amepata timu mpya ambayo ni Wydad Casablanca atakuwa huko kwenye changamoto mpya.
Huyu hapa Kamwe Ofisa Habari wa Yanga SC
Kamwe alisema:” Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF na wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB kuwa hatutacheza mchezo wa fainali wa CRDB siku ya tarehe 28 mpaka tutakapolipwa hela yetu ya ubingwa kwa msimu uliopita.
“Tumevumilia dharau hizi kutoka kwa mamlaka za soka kwa muda mrefu sana. Sasa hii imefika mwisho. Hii ya Zanzibar pia hatuchezi. Kamwe aliongeza kuwa hawatakuwa tayari kucheza ligi msimu wa 2025/26 na hawatayumba kwa lolote lile kwa kuwa ni msimamo wao.
“Napenda kuwajuza waandishi wa Habari yasipofanyiwa kazi matakwa yetu matatu kwa uharaka Yanga SC hatutakuwa tayari kucheza mchezo namba 184, mechi zote mbili za ligi zilizobaki na hatutashiriki Ligi Kuu msimu ujao. Huu ndio msimamo wetu na hatutayumba kwa lolote.
CRDB waweka bayana suala la malipo kukamilika
Baada ya taarifa hiyo, CRDB Juni 10 2025 walitoa taarifa kwa uma kuwa benki ilikamilisha wajibu wake kifedha kwa TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano hayo. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanyika kwa TFF kwa mujibu wa mkataba baina ya Benki ya CRDB na TFF.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa benki ya CRDB inatambua kuwa mbali na mchezo wa soka kuunganisha jamii yetu na kutoa burudani lakini pia mchezo huu ni ajira kwa vijana wengi hivyo dhamira ni kuendelea kushirikiana na TFF, vilabu mbalimbali na wadau wengine katika kukuza mchezo kwa maslahi mapana ya taifa letu.
Hawa hapa TFF kuhusu sakala la fedha ya ubingwa wa Yanga SC
TFF kupitia kwa Ofisa Habari, Clifford Ndimbo wametoa taarifa kuwa TFF ndiyo inayoidai Yanga SC na iliomba kwa barua fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zitumike kulipa malipo wanayotakiwa kulipa kwa TFF ikiwemo ada za wachezaji wa kigeni.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa: “Tunapenda kuuthibitishia umma kuwa benki ya CRDB ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la TFF, na inatekeleza ipasavyo majukumu yake. Kwa msimu wa 2023/24 wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB benki hiyo ililipa milioni mia mbili na Hamsini kwa ajili ya uendeshaji wa mashindano hayo.

“Tumemskia Meneja Habari wa Yanga SC, kupitia vyombo vya habari akidai kuwa klabu inaidai TFF milioni mia mbili ambayo ni zawadi ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho la benki ya CRDB. Hivyo ili kutoendelea kusababisha sintofahamu kwa umma tumeiandikia barua Yanga SC kutuma kwetu mtaalamu wao wa fedha kesho saa 4 asubuhi kuhakiki deni la klabu hiyo akiwa na vielelezo vyote ofisi za TFF.”

