tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26Yanga vs Prisons
  • Mchezo wa Tanzania Prisons vs Yanga SC utawaka Juni 18 2025 na ni zaidi ya mchezo wa ligi, hivi ni vita ya ubingwa na kuepuka kushuka daraja.
  • Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana, Prisons walikubali kipigo cha Mbwa koko cha mabao 4-0, ilikuwa Desemba 22, 2024.
  • Mpaka sasa Yanga imefunga mabao 71 na kuruhusu mabao 10 tu, huku Tanzania Prisons wao wakifunga mabao 23 na kuruhusu mabao 38.

Huku kukiwa na sintofahamu juu ya uwepo wa mchezo wa dabi ya Kariakoo uliopangwa kupigwa Juni 15, mwaka huu, uongozi wa Yanga umetamba kuwa maandalizi yao ya sasa ni kwa ajili ya mchezo wa Tanzania Prisons vs Yanga SC utawaka Juni 18 2025. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa ugenini jijini Mbeya. Soma zaidi kuhusu mchezo huo and uelewe utaenda vipi.

image
image

Kuhusu Tanzania Prisons vs Yanga SC kutawaka Juni 18 2025

Ratiba ya mechi za Yanga
Ratiba ya mechi za Yanga

Huu ni mchezo wa mkondo wa pili wa ligi kuu Bara (NBC Premier League), ambao umepangwa kupigwa tarehe 18 Juni 2025, kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo mchezo huu ni kati ya michezo miwili tu, ambayo uongozi wa Yanga umetamba kusaliwa nayo.

Mchezo huu unatarajiwa kuendelea kutoa taswira ya ubingwa wa ligi kwa msimu huu, kwani mpaka sasa Yanga wanaongoza msimamo wa kofauti ya pointi moja wakikusanya pointi 73, dhidi ya mshindani wao wa karibu na watani zao Simba  ambao mpaka sasa wamekusanya pointi 72.

Ikiwa Yanga atapoteza pointi kwenye mchezo huu basi Simba watakuwa kwenye nafasi ya kuwapiku Yanga na kuongoza msimamo, lakini hii ni iwapo tu, watashinda michezo yao, wakati huu Simba wakitamba kuwa maandalizi wanayoyafanya ni kwa ajili ya kuwavaa Yanga.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB, H2H Ngoma kupigwa Zanzibar 28/06/2025

Mara ya mwisho timu hizo kukutana H2H

Tanzania Prisons vs Yanga SC kinawaka Juni 18 2025
Yanga vs Prisons matokeo ya mwisho

Historia yamchezo baina ya timu hizi inaibeba Yanga zaidi ambapo mara ya mwisho walipokutana Prisons walikubakli kipigo cha Mbwa koko cha mabao 4-0, ambapo hii ilikuwa Desema 22, mwaka jana 2024 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo wa Desemba 22, mwaka 2024 magoli ya Yanga yalifungwa na Clement Mzize, Prince Dube huku Mlinzi wa kimataiwa wa Tanzania, Ibrahim Bacca akifanikiwa kufunga mabao mawili ambayo ni bao la tatu na la nne.

Ikumbukwe ushindi huo ulifanya Yanga ambao walikuwa nafasi za chini kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, nyuma ya Simba SC kwa tofauti ya pointi moja.

SOMA HII PIA: KVZ FC vs Yanga patachimbika Muungano Cup 2025

Aucho ashtua! Semaji Ali Kamwe athibitisha amebaki moja tu

Aucho (-)
Aucho

Licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa huenda Yanga wataachana na kiungo wao wa ulinzi raia wa Uganda, Khalid Aucho staa huyo ameshtua na kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo baada ya kurejea uwanjani mapema akitokea majeruhi ambayo yalimfanya akose sehemu kubwa ya michezo ya ligi.

Utofauti wa mizania ya Yanga na Tanzania Prisons

Young Africans SC (Yanga)

Yanga ni moja ya timu kongwe na zenye mafanikio makubwa nchini Tanzania. Ikiwa na wachezaji wenye uzoefu na vipaji vikubwa, timu hii inajivunia safu imara ya ulinzi na ile ya ushambuliaji, wachezaji kama Prince Dube, Clement Mzize, na Ibrahim Bacca ikiwa sehemu ya mifano ya ubora na uzoefu.

Mpaka sasa safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao 71 na kuruhusu kufungwa mabao 10 tu, huku Tanzania Prisons wao wakifunga mabao 23 na kuruhusu nyavu zao zitikiswe mara 38.

Uwepo wa kocha mwenye wasifu mkubwa, Miloud Hamdi ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaiongezea sifa ya ushindi kwa Yanga kuulekea mchezo huu, kwani kocha huyo amewahi kufundisha klabu kadhaa kubwa.

Tanzania Prisons SC

Timu hii kutoka Mbeya inatarajiwa kukutana na changamoto kubwa dhidi ya Yanga, lakini ina wachezaji wenye uwezo wa kupambana na wameahidi kuimarisha ulinzi na kuongeza kasi ya mashambulizi ili kupata matokeo chanya ili kujinusuru na janga la kusuka daraja

Hitimisho utabiri wa mchezo

------------------------------------------------n
Rais wa Yanga Hersi

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku kila timu ikitafuta pointi tatu muhimu. Yanga inahitaji ushindi ili kuendelea kuongoza vita ya ubingwa kwa msimu wanne mfululizo, huku Tanzania Prisons inahitaji pointi ili kuboresha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi.

Mashabiki wa soka kutoka viunga mbalimbali vya Mbeya watakuwa na hamu kubwa ya mchezo huu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.