Mayele na ubingwa wa CLMayele na ubingwa wa CL
  • Pyramids FC 2-1 Mamelodi Sundowns CAF Mayele atikisa Afrika, Pyramids Mabingwa, ndivyo bango linavyosomeka mara baada ya kumalizika kwa dakika 90, na Pyramids kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
  • Mayele ameendele kuitiksa Afrika, hii ni baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao sita katika mechi 10 za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ikiwemo bao moja la fainali leo.
  • Huu ni mchezo wa 4 kwa timu hizi mbili kukutana katika mashindano ya vilabu barani Afrika, ambapo Mamelodi Sundowns wameshinda mechi moja, michezo 2 imeisha kwa sare, huku Pyramids nao wakilipa kisasi leo kwa 3-1.

Pyramids FC 2-1 Mamelodi Sundowns CAF Mayele atikisa Afrika,Pyramid Mabingwa, ndivyo bango linavyosomeka mara baada ya kumalizika kwa dakika 90, na Pyramids kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Mayele akiendele kuitiksa Afrika.

Pyramids FC 2-1 Mamelodi Sundowns CAF Mayele Mchezo ulikuwaje?

Matokeo ya mwisho
Matokeo ya mwisho

Mara baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza ambao uliopigwa wiki iliyopita nchini Afrika Kusini, kila mmoja alitarajia mchezo mgumu leo na ndicho kilichotokea kwenye Uwanja wa 30 June Air Defence nchini Misri.

Timu zote mbili zilifanya mashambulizi hatari dhidi ya mpinzani huku, Pyramids wakianza kutangulia kwa bao la mapema la straika wao Mkongomani, Fiston Mayele baada ya mlinzi wao Kekana kushindwa kuondoa hatari na Mayele kupiga shuti kali lililomshinda kipa Williams.

Baada ya bao hilo Mamelodi walijaribu kutengeneza mashambulizi ya kusawazisha bao, lakini wakajikuta wakiongezwa bao la pili dakika ya 56 na Ahmed Samy na kufanya mzigo uzidi kuwa mzito kwa Mamelodi Sundowns.

Goli pekee la kufutia machozi la Mamelodi lilifungwa na straika wao, Iqram Rayners dakika ya 76 ya mchezo na kufanya mchezo uzidi kuwa na kasi, lakini mpaka filimbi ya mwamuzi kuashiria kumaliza mchezo inapulizwa Mamelodi walishindwa kuongeza bao.

SOMA HII PIA: Fiston Mayele shujaa wa Pyramids FC 2024/25, aipeleka Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika

Mchezo wa kwanza kati ya timu hizi mbili ulimalizika kwa sare.

Pyramids FC walifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho za mchezo wa kwanza na kupata sare muhimu. Bao hilo liliwapa matumaini na kupunguza presha kuelekea mchezo huu wa nyumbani na kuwapa ari ya kubadili matokeo.

Costa ndiye aliyefunga bao pekee la Sundowns kwenye mchezo wa kwanza. Kiungo huyo kutoka Brazil mwenye umri wa miaka 26 alijaribu kurudia kiwango chake bora leo lakini alishindwa safu ya kiungo na timu yake kuipa ubingwa timu hiyo.

Mambo muhimu kuhusu mchezo wa leo

Mahali: Cairo, Misri

Uwanja: 30 June Air Defence Stadium

Tarehe: Jumapili, Juni 1

VAR: Inatumika

Fiston Mayele aitikisa Afrika

One for the books! Pyramids FC claim a vital --- win over Mamelodi Sundowns in the second leg of the #TotalEnergiesCAFCL final!
Mastaa wa Pyramids wakishangilia ushindi

Mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo, Mayele mwenye umri wa miaka 30 amekuwa na msimu bora sana kulinganisha na msimu wake wa kwanza tangu ajiunge Pyramid FC. Mayele amefunga mabao sita katika mechi 10 za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

SOMA HII PIA: Mamelodi Sundowns vs Yanga: Preview, Betting Tips & Prediction 23/24

Ubingwa wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa katika historia ya timu hiyo

Pyramids mabingwa Afrika
Pyramids mabingwa Afrika

Pyramid wamefanikiwa kutwaa ubingwa huu ukiwa ni wa kwanza katika historia ya timu hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2008, kabla ya kubadilishwa jina baada ya kununuliwa na tajiri.

Kwa upande wa Masandawana, wao waliingia katika mchezo huu wakiwa wanawania taji lao la pili la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Fomu za Hivi Karibuni na Rekodi ya Mikutano:

Pyramids wamemaliza ligi kuu ya Misri wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 56, mbili nyuma ya mabingwa Al Ahly. Hii inaonyesha ni ubora kiasi gani wamekuwa nao msimu huu.

Kwa upande wa kikosi cha Mamelodi Sundowns ya kocha, Miguel Cardoso kilishinda Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa mara ya nane mfululizo, jambo ambali liliwapa kujiamini zaidi kuelekea mchezo wa fainali.

Kwa kuangalia mwenendo wa michezo mitano iliyopita, Pyramids kabla ya mhezo wa leo walifanikiwa kushinda mechi 3, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.

Kwa upande wa Mamelodi Sundowns wao katika michezo mitano iliyopita walifanikiwa kushinda michezo minne na kutoa sare mchezo mmoja pekee.

Mwisho, Pyramids wamelipa kisasi

Pyramids FC 2-1 Mamelodi Sundowns CAF Mayele
Pyramids vs Mamelodi Sundowns

Huu unakuwa mchezo wa nne kwa timu hizi mbili kukutana katika mashindano ya vilabu barani Afrika, ambapo katika mara nne ambazo wamekutana Mamelodi Sundowns ameshinda mechi moja, michezo miwili imeisha kwa matokeo ya sare, huku Pyramids nao wakilipa kisasi leo kwa kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-1.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.