Mhe- Tarimba na mshindiMhe- Tarimba na mshindi
  • Kijana wa Miaka 23 ajinyakulia TZS 100,000,000 ya Sportpesa Goal Rush, ushindi huo wa kusisimua ameupata baada ya kubashiri kwa usahihi mechi tatu mfululizo kupitia mchezo wa SportPesa Goal Rush.
  • Hii ni kwa mara ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa mchezo wa Goal Rush mwaka jana 2024, SportPesa Tanzania, imeshuhudia mshindi aliyejinyakulia zawadi kubwa ya TZS 100,000,000.
  • Unawezaje kushinda Milioni 100 ya SportPesa Goal Rush? Utajishindia kwa kuchagua nani atafunga bao la kwanza, bao hilo litafungwa katika kipindi gani na dakika gani ya mechi.

Kijana wa Miaka 23 ajinyakulia TZS 100,000,000 ya Sportpesa Goal Rush, katika ushindi huo wa kusisimua ameupata baada ya kubashiri kwa usahihi mechi tatu mfululizo kupitia mchezo wa SportPesa Goal Rush. Ni kwa mara ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa mchezo wa Goal Rush imeshuhudia mshindi aliyejinyakulia zawadi kubwa ya TZS 100,000,000.

Ushindi wa kihistoria na rekodi

It ends level at Anfield-
Moja ya mechi za ushindi

Ushindi huu unaingia katika vitabu vya historia na kumbukumbu kwani ni kwa mara ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa mchezo wa Goal Rush mwaka 2024, SportPesa Tanzania imeshuhudia mshindi aliyejinyakulia zawadi kubwa ya TZS 100,000,000 (Milioni 100), baada ya kubashiri kwa usahihi mechi tatu mfululizo.

Ibrahimu mkazi wa Kilindi, Tanga alibashiri kwa usahihi mechi tatu mfululizo kwa kuchagua nani atafunga bao la kwanza, bao hilo litafungwa katika kipindi gani na dakika gani ya mechi ambapo alifanya utabiri sahihi kwenye mechi zifuatazo:

  • Liverpool vs Arsenal – Bao la kwanza: Liverpool, dakika ya 20 (kipindi cha kwanza)
  • Napoli vs Genoa – Bao la kwanza: Napoli, dakika ya 15 (kipindi cha kwanza)
  • Boavista vs Porto – Bao la kwanza: Porto, dakika ya 20 (kipindi cha kwanza)

SOMA HII PIA: SportPesa Goal Rush: Washindi 3-9 Mei 2025

Liverpool 2-2 Arsenal yampa Milioni 100 za SportPesa; Ibrahimu afunguka furaha kubwa

Nyumbani kwa mshindi
Nyumbani kwa mshindi

Akielezea furaha yake, Ibrahim alisema: “Ilikuwa asubuhi, nilikuwa nimetoka kulala. Nikachukua simu yangu kuangalia, nikakuta ushindi. Nikatuliza kwanza akili yangu, nikakaa chini. Nilikuwa siamini kuwa mimi ndiye mshindi, nilikuwa siamini kabisa kuwa nimeshinda milioni mia ya Goal Rush.”

Bwana Ibrahimu amebeba heshima kubwa sana kwa kuwa mshindi wa kwanza wa Goal Rush na kujiweka kwenye historia ya Mamilionea wa SportPesa Tanzania.

SOMA HII PIA: Goal Rush: SportPesa’s new free-to-play game offering 10 million grand prize

Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Mhe. Tarimba Abbas apongeza

Liverpool 2-2 Arsenal yampa milioni 100 za SportPesa
Tarimba Abbas

Akizungumza kuhusu ushindi wa Ibrahimu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa, Mhe. Tarimba Abbas, alisema: “Kwetu sisi ni fahari kusema kweli, ni mara ya kwanza kupata mshindi wa Goal Rush kutoka Tanzania. Furaha yetu nyingine ni kwamba mshindi wetu Ibrahimu ametokea mbali – Kilindi, Tanga.

“Hii inaonyesha kuwa washindi wetu wanatoka sehemu mbalimbali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na tunaendelea kufurahia kuwa SportPesa imeweza kutoa zawadi kubwa ya TZS 100,000,000, ambayo itaenda kubadilisha maisha yake na ya familia yake.”

Mhe. Tarimba pia aliongeza: “Kumekuwa na majadiliano mengi kuhusu michezo ya kubashiri. Ukweli ni kwamba, “Betting ni Skill game”, ni mchezo wa watu wanaojua wanachokifanya na wanaopenda burudani ya kutumia akili. Watu wamekuwa wakiichukulia poa kutokana na kutokuelewa. Ila betting siyo pata potea.

“Betting pia ni shughuli ya kiuchumi na ushindi wa Ibrahimu unadhihirisha hilo ataweza kutumia ushindi wake kufanya biashara, kutengeneza kipato, kutoa ajira na atatozwa ushuru kama sehemu ya sheria. Kwa maana hiyo, betting ni shughuli ya kiuchumi, maana kitu chochote kinachoingiza kipato lazima kitaotozwa ushuru.” 

Mchezo wa Goal Rush ni nini? Na ufanye nini ili kuibuka mshindi?

image
Supa Jackpot

Goal Rush ni mchezo wa kipekee kutoka SportPesa unaowapa wachezaji nafasi ya kubashiri kati ya mechi tatu na kuchagua timu ipi itafunga bao la kwanza, katika kipindi gani na dakika ipi. Ni mchezo wa BURE kwa wateja wote wa SportPesa ambao wamesuka mkeka ndani ya siku saba za karibuni.

Mchezo huu unatoa zawadi kubwa ya TZS 100,000,000 pamoja na bonus za TZS 200,000 na TZS 10,000 kila siku. Kwa taarifa zaidi kuhusu Goal Rush na michezo mingine ya SportPesa, tembelea: www.sportpesa.co.tz, piga BURE *150*87#, AU pakua Sportpesa App kwenye Google play na App store.

Promosheni ya Zero data inaendelea kuwawezesha wateja wa Sportpesa wanaotumia mitandao ya Vodacom, Yas na Airtel kucheza bila bando.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.