- RS Berkane vs Simba SC 17/05/2025 live ni zaidi ya mechi ya fainali, hii ni vita ya rekodi mpya inayosubiriwa kwa hamu na maelfu ya Watanzania na Wanasimba kote Duniani.
- Mechi hii ya fainali ya mkondo wa kwanza itapigwa leo Jumamosi saa 4:00 usiku kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane.
- Mpaka sasa hakuna mbabe kati ya timu hizo kwani wamekutana mara mbili mwaka 2022, ambapo Berkane walishinda mchezo mmoja na Simba wakishinda mchezo mmoja.
RS Berkane vs Simba SC 17/05/2025 live ndio habari kubwa ya soka wikiendi hii, ambapo Simba watakuwa mgeni wa Berkane nchini Morocco kwenye mchezo wa Fainali yam kondo wa kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo huo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane unatarajiwa kufuatiliwa na maelfu ya mashabiki kutokana na ukubwa na historia ya timu hizo.
Kocha Simba atoa tamko zito kuelekea RS Berkane vs Simba SC 17/05/2025 live

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa mchezo wa leo dhidi ya RS Berkane utakuwa mgumu, kwani Berkane ni timu ambayo imekuwa na historia ya matokeo bora nyumbani kwao msimu huu jambo ambalo Simba inapaswa kuchukua tahadhari.
Akizungumzia hali ya kikosi chake, Fadlu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wataingia katika mchezo wa leo kwa malengo ya kutafuta bao la ugenini, huku wakiwa makini kuzuia wasiruhusu bao.
“Tumejipanga kikamilifu kwa ajili ya mchezo wa fainali kesho, kikosi chetu ni kichanga kwenye michuano hii ukilinganisha na wapinzani wetu lakini tumejipanga vizuri na malengo yetu ni kushinda taji hili,” amesema Fadlu.
SOMA HII PIA: Zanzibar kumenoga huku Simba SC vs RS Berkane kule Yanga watangaza jambo zito
Kocha Simba awa mkali, awaonya mastaa wake
Kocha Fadlu amendelea kusema: “Utakuwa mchezo mgumu kuliko yote ambayo tumecheza msimu huu n ani wazi makosa tuliyokuwa tunafanya kuanzia hatua ya awali, makundi robo mpaka nusu fainali yamepungua kwa kiasi kikubwa, tupo tayari kutimiza malengo yetu.
“Hatupaswi kufanya makosa ambayo yanaweza kutugharimu, tunahitaji kucheza kwa umakini,” amesema Fadlu.
Che Malone asema wachezaji wapo tayari kwa Fainali

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa Simba, Che Malone Fondoh amesema ubingwa wa michuano hii ni fahari ya kila mchezaji wa Simba na wapo tayari kupambana hadi mwisho, kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kikosi kilichoweka historia kuchukua ubingwa.
“Kila mchezaji ana ndoto ya kucheza fainali ya michuano hii mikubwa Afrika, tunafahamu tunaenda kukutana na mpinzani mkubwa lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho kufanikisha malengo ya timu,” amesema Che Malone.
Kikosi cha Simba kinachotarajiwa kuanza mchezo wa leo RS Berkane vs Simba SC 17/05/2025 live
Kikosi cha Simba

Kuelekea mchezo wa leo, haitarajiwi kuona kocha Simba akifanya mabadiliko makubwa ya kikosi kulinganisha na kile kilichocheza mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ugenini dhidi ya Stellenbosch FC, hivyo kikosi kinachotarajiwa kuanza ni:
Camara, Kapombe Zimbwe Jr, Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu Ngoma, Mukwala, Ahoua, Mpanzu.
SOMA HII PIA: Simba SC vs RS Berkane Uwanja wa Mkapa waleta sekeseke CAF, tamko latolewa
Mambo muhimu kuyajua kuhusu RS Berkane vs Simba SC 17/05/2025 live

- Timu hizo mbili zinakutana kwa mara ya kwanza katika historia yao kwenye hatua ya fainali, huku wakiwa wamewahi kukutana kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kila timu ilishinda nyumbani kwao.
- Mara baada ya kufika Morocco, kikosi cha Simba kiliendelea na mazoezi katika Uwanja wa Magazan, kujiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane
- Simba imesafiri na kikosi cha mastaa 24 ambao wameshiriki mazoezi hayo na morali zao zipo juu kuelekea mchezo huo, ambao wamejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.
- Baada ya kufika Oujda kikosi jana ilifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane, ambao unatarajiwa kutumika kwa mchezo.
- Bado kuna sintofahamu juu ya wapi mchezo wa marudiano ambao unatarajiwa kupigwa, hii ni baada ya Caf kutangaza kuuhamishia mchezo huo utakaopigwa Mei 25, Uwanja wa Amaani Zanzibar, huku viongozi mbalimbali wa Simba wakionekana kugomea uamuzi huo.
SOMA HII PIA: Simba SC ratiba yake Bongo ni bandika bandua, mechi nne siku 10

