Inter Milan Vs FC BarcelonaInter Milan Vs FC Barcelona

  • Inter Milan Vs FC Barcelona ‘live’ ni mchezo mkali wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao unatarajiwa kupigwa leo saa 4:00 usiku.
  •  Mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Hispania wiki iliyopita uliisha kwa sare ya mabao 3-3.
  • Inter wanatarajia kuwa na straika wao, Lautaro Martinez aliyerejea kutoka majeruhi na ndiye mfungaji bora wa kihistoria wa Inter katika mashindano ya vilabu ya Ulaya, akiwa na magoli 20, ikiwemo manane msimu huu.

Inter Milan Vs FC Barcelona ni mchezo mkali wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao unatarajiwa kupigwa usiku wa leo na kufuatiliwa na mamilioni ya wapenda soka duniani.

Mchezo huu wa kukata na shoka unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa San Siro jijini Milan.

Timu zote zinaingia katika mchezo huu huku mzani ukiwa umebalansi mara baada ya sare ya mabao katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulipigwa nchini Uhispania wiki iliyopita.

INAHUSIANA: Barcelona Vs Real Madrid 26/4/2025, Uso Kwa Uso Fainali Copa Del Rey

Hali ya kikosi cha Inter Milan

Told through images #ForzaInter #UCL #BarcellonaInter
Lautaro Martinez

Hamasa ndani ya kikosi cha Inter Milan imezidi kupamba moto baada ya nahodha wao, Lautaro Martinez kufanya mazoezi na kikosi.

Nahodha wa Inter Milan, Lautaro Martínez, anatarajia kuanza pacha na mshambuliaji mwenzake, Marcus Thuram kuelekea mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa leo dhidi ya Barcelona.

Ikumbukwe Katika maandalizi ya mchezo wa mkondo wa kwanza wiki iliyopita, mashaka yalikuwepo kama, Thuram angepona kwa muda kuweza hata kukaa benchi baada ya kukosa mechi tatu kwa jeraha la paja.

Lakini, Thuram alishangaza kwa kuanza mechi na kufunga bao la kwanza sekunde chache baada ya mchezo kuanza katika sare ya kusisimua ya 3-3.

Licha ya kufanya mazoezi, Lautaro bado huko kwenye mashaka ikiwa atakuwa sehemu ya kikosi baada ya kuondolewa kipindi cha kwanza, dhidi ya Barcelona Jumatano iliyopita kutokana na jeraha la misuli ya paja.

INAHUSIANA: FC Barcelona vs. Sevilla: Clash of Titans at Estadi Olímpic

Alichosema kocha wa Inter, Inzaghi

Kocha wa Inter, Simone Inzaghi, alikiri wiki iliyopita kuwa itakuwa “vigumu sana” kumpata Lautaro kwa wakati kwani aina hiyo ya jeraha kwa kawaida huchukua siku 10 hadi wiki mbili kupona.

Lakini matumaini yameongezeka kambini mwa Inter baada ya Lautaro kufanya mazoezi na kikosi Jumatatu alasiri.

Lautaro ndiye mfungaji bora wa kihistoria wa Inter katika mashindano ya vilabu ya Ulaya, akiwa na magoli 20, ikiwemo manane msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amefunga magoli 21 na kutoa pasi za mabao sita kwa Inter katika mashindano yote msimu huu.

Inter kuweka Yamal ‘chini ya uangalizi maalum’

Inter Milan Vs FC Barcelona 'live'
Lamine Yamal na Raphinha

Kuhusu nyota hatari na kinda wa Barcelona, Lamine Yamal kocha wa Inter, Inzaghi ameendelea kusema: “Kwa hakika, atawekewa ulinzi wa karibu. Tutajaribu kumdhibiti, lakini kama nilivyosema kwenye mkondo wa kwanza baada ya kumuona moja kwa moja, ni kipaji cha ajabu.

“Ana umri wa miaka 17 tu, lakini ni hatari sana akiwa na mpira. Katika nyakati ngumu, wachezaji wenzake humkabidhi mpira. Kilichonishangaza zaidi kuhusu yeye ni jinsi alivyo na akili ya haraka  akipokea mpira, tayari anajua hatua inayofuata. Kwa hiyo, atakuwa chini ya uangalizi maalum.”

Kocha wa Barcelona apewa jeuri na Yamal

Barça - Inter- face to face (-)
Hans Flick na Simone Inzaghi

Kocha wa Barcelona, Hans Flick amepongeza kipaji cha Yamal kabla ya mkondo wa pili huko Inter ambapo amemuelezea mshambuliaji huyo kuwa ni jeuri ya Barcelona.

Yamal alifunga bao la kwanza la Barca walipotoka nyuma kwa 2-0 dhidi ya Inter kabla ya kupata sare ya 3-3 katika Uwanja wa Olimpiki.

Kijana huyo wa miaka 17 amekuwa muhimu katika mafanikio ya Barcelona msimu huu, tayari wakiwa wameshinda Supercopa ya Uhispania na Copa del Rey, na wanaongoza LaLiga kwa pointi nne mbele ya Real Madrid wakiwa na mechi nne zilizobaki.

Barcelona na Inter tayari wameshinda mataji manane ya Ulaya kati yao, Barcelona wakisaka taji lao la sita la Ligi ya Mabingwa la kwanza tangu 2015.

Akimzungumzia staa huyo, Flick alisema: “Lamine ni kipaji. Kile anachofanya na mpira ni cha kushangaza. Kila pasi ni sahihi, kwa nguvu inayofaa na urefu sahihi. Ni ajabu kwa mtoto wa miaka 17.

“Na kwa mimi, ilikuwa mechi ya Jumatano iliyopita, alipotuleta nyuma kwenye mchezo kupitia matendo yake na bao lake. Ilikuwa nzuri sana kuona. Lakini lazima aendelee kuonyesha uwezo huo.

“Sasa ni mkondo wa pili na ni muhimu sana, kwa sababu tunataka kufika fainali. Hilo ndilo lengo letu, na tunahitaji kila mmoja kuwa kwenye kiwango cha juu dhidi ya timu bora ya Inter.”

Olmo: Mafanikio ya Barca msimu huu hayanishangazi

Kiungo wa Barcelona, Dani Olmo, amesema hashangazwi kupita kiasi na mafanikio ya Barca msimu huu, kwani alitarajia hali hiyo alipohamia klabuni majira ya joto yaliyopita.

Akizungumza Jumatatu kabla ya mkondo wa pili dhidi ya Inter Milan, alisema: “Nilitarajia kuwa katika nafasi ya kushindania kila kitu kufikia wakati huu.”

Mbali na kuwa mechi moja tu kutoka fainali ya Ligi ya Mabingwa, Barcelona tayari wameshinda Supercopa ya Uhispania, Copa del Rey na wanaongoza LaLiga kwa pointi nne.

Barcelona 3-3 Inter Milan yaandika rekodi

------------------------------------------------n
Mastaa wa Barcelona wakishangilia

Sare ya wiki iliyopita ya 3-3 ilikuwa moja ya mechi za nusu fainali zilizozaa mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa tangu Bayern Munich na Dynamo Kiev walipotoka sare ya aina hiyo mnamo Aprili 1999.

Flick: Ulinzi wetu lazima uwe makini

Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, kuhusu Inter Milan: “Ni timu yenye nguvu, na uzoefu mkubwa. Lakini pia wanapenda kucheza soka na wanajua kucheza pamoja, hivyo ni vigumu kuwadhibiti.”

“Kwa hiyo, kesho kila mmoja lazima ashiriki katika ulinzi hiyo ndiyo jambo la muhimu zaidi tunalopaswa kufanya.”

Lewandowski huenda akarudi benchi

Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, kuhusu Robert Lewandowski: “Tulizungumza jana, kila kitu kinaenda vizuri na yuko tayari, yuko fiti vya kutosha kuwa benchi. Kwa hiyo kama tutamhitaji, huenda akaingia. Ni hivyo.”

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.