Maxi tuzoMaxi tuzo
  • Dakika 270 safu ya ushambuliaji Yanga yatupia kambani mabao manne, Muungano Cup 2025.
  • Maxi Nzengeli mfungaji bora, katupia kambani mabao mawili sawa na Fredy Seleman wa JKU SC.
  • JKU SC ina rekodi yake kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara zilikiona cha mtema kuni.

Yanga SC imetwaa Muungano Cup 2025 huku zikiandikwa rekodi zakutosha kwenye mechi za ushindani ndani ya uwanja kwenye ushindani.

Yanga Bingwa Muungano Cup ---- (-)
Yanga bingwa Muungano Cup 2025. Source: Yanga SC.

Chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, Yanga ilikamilisha kete yake ya dakika 270 kwa  kushuhudia ubao wa Uwanja wa Gombani ukisoma JKU 0-1 Yanga, bao la ushindi likipachikwa na kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli.

Kuna rekodi ambazo zimeandikwa Muungano Cup 2025 hapa tunakuletea baadhi namna ilivyokuwa kwenye msako wa ushindi namna hii:-

Zimamoto dakika 180 walikuwa wanazima

 Zimamoto walikuwa moto kweli kwa kuanza hatua yar obo fainali ilikuwa ni Aprili 25 2025 ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

 Kwenye mchezo huo bao pekee la ushindi lilifungwa na Rashid Salum dakika ya 28 na bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na Coastal Union ya Tanga safari ikawa imegota mwisho katika Muungano Cup 2025.

  Rashid Salum wa Zimamoto kwenye mchezo huo wa hatua ya robo fainali alitwaa tuzo ya mchezaji bora kwa kuwa alipachika bao la ushindi lililoipeleka Zimamoto hatua ya nusu fainali.

Yanga SC waizima Zimamoto

Baada ya Zimamoto kuizima Coastal Union kwenye ndoto za safari ya kuelekea kutwaa Muungano Cup walikutana na Yanga SC hatua ya nusu fainali hapo wakatulizwa kwa kufungashiwa virago.

Katika mchezo wa nusu fainali ilikuwa Zimamoto 1-1 Yanga SC Aprili 29 2025. Mshindi alipatikana kwa penati ambapo ni Zimamoto 1-3 Yanga SC, Yanga ikakata tiketi kutinga hatua ya fainali.

Yanga SC mwendo wao dakika 270

Walianza kwenye hatua ya robo fainali dhidi ya KVZ FC baada ya dakika 90 wakawafungashia virago wapinzani wao ilikuwa ni Aprili 26 2025 siku ya Muungano Yanga SC ilipata ushindi wa mabao 2-0.

--’- #MuunganoCup KVZ FC --- Young Africans SC#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko
Kiungo wa Yanga SC Aziz Ki kwenye mchezo wa dhidi ya KVZ. Source: Yanga SC.

Mabao ya Yanga SC kwenye mchezo huo yalifungwa na Aziz Ki alipachika bao la ufunguzi dakika ya 29 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Gombani na bao la pili Dennis Nkane alifunga na kwenye mchezo huo alianzia benchi alipachika bao hilo dakika ya 85.

Kiungo Mudathir Yahya alitwaa tuzo ya mchezaji bora baada ya mchezo kugota mwisho katika hatua ya robo fainali.

Nusu fainali waliipoteza Zimamoto

Zimamoto ambayo iliwafungashia virago Coastal Union hatua ya robo fainali ilimaliza mwendo mbele ya Yanga SC kwenye hatua ya nusu fainali.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa dakika 90 ilikuwa Zimamoto 1-1 Yanga SC Aprili 29 2025. Ushindi wa Yanga SC ulikuwa ni penati 3-1 wakakata tiketi kutinga hatua ya fainali.

Fainali na Muungano Cup mkononi

Kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Gombani, Mei Mosi 2025 baada ya dakika 90 walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Maxi Nzengeli ambaye alisepa na tuzo ya ufungaji bora.

Rekodi za mfungaji bora Maxi

Kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli ni mfungaji bora Muungano Cup 2025 akifunga jumla ya mabao mawili kwenye mechi tatu ambazo Yanga SC imecheza.

Nzengeli alifungua ukurasa wa mabao katika mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Zimamoto ilikuwa Aprili 29 2025 alipopachika bao dakika ya 29. Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Gombani ulisoma Zimamoto 1-1 Yanga SC, bao la Zimamoto lilifungwa na Saidi Mwinyi dakika ya 71.

Yanga SC ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penati ambapo ilikuwa Zimamoto 1-3 Yanga SC, langoni kwa Yanga SC. Bao la pili Nzengeli alipachika kwenye mchezo wa fainali dhidi ya JKU SC ilikuwa ni Mei Mosi 2025.

Baada ya dakika 90 ubao ukasoma JKU SC 0-1 Yanga SC, bao la ushindi lilipachikwa dakika ya 45 na likadumu mpaka mwisho wa mchezo huo. Ikumbukwe kwamba JKU SC waliwafungashia virago Singida Black Stars hatua ya robo fainali na Azam FC kwenye nusu fainali.

Lusajo
Azam FC iliondolewa hatua ya nusu fainali Muungano Cup na JKU SC. Source: Azam FC.

Dakika 29 na maajabu yake

Yanga SC kwenye mechi tatu ambazo wamecheza ni mabao manne safu ya ushambuliaji imetupia huku dakika ya 29 ikiwa na maajabu yake kwa kuwa nyota wawili walifunga bao katika mechi tofautitofauti. Bao la kwanza la Aziz Ki ambalo lilikuwa la ufunguzi lilifungwa dakika ya 29 dhidi ya KVZ FC hatua ya robo fainali na bao la kwanza la Maxi ambalo lilikuwa la ufunguzi lilifungwa dakika ya 29 nusu fainali dhidi ya Zimamoto.


Share this: