barcelona Vs Inter Milan 30/4/2025barcelona

  • Hili ni taji la 32 la Copa Del Rey kwa Barcelona katika historia ya timu hiyo tangu kuanzishwa kwake.
  • Barcelona imeicharaza Real Madrid katika michezo yote 3 waliyokutana msimu huu.
  • Goli la dakika ya 116 la Mfaransa Kounde laamua matokeo

Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025, hii ni baada ya usiku wa kuamkia leo Jumapili kuicharaza Real Madrid mabao 3-2 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.

Goli la Jules Koundé katika dakika za mwisho za muda wa nyongeza liliipa Barcelona ushindi wa kusisimua wa 3-2, dhidi ya mahasimu wao wakubwa Real Madrid katika fainali ya kuvutia ya Copa del Rey.

Kounde alifunga bao hilo dakika ya 116 ya mchezo katika fainali ya kuvutia ambayo iliyochezwa katika uwanja wa La Cartuja mjini Seville, jana Jumamosi.

BARCELONA MABINGWA COPA DEL REY 2025, UBINGWA WA 32

Barcelona Mabingwa Copa Del Rey
Barcelona Mabingwa Copa Del Rey

Ushindi huo unaifanya Barça kunyakua taji lao la 32 la Kombe la Mfalme, rekodi ya kihistoria, kupitia shuti kali kutoka kwa beki wa Kifaransa Koundé, ambaye alitumia pasi ya Brahim Díaz na kufunga kwa mguu wa kulia katika kona ya chini ya goli la Thibaut Courtois kutoka yadi 25.

KADI NYEKUNDU ZATAWALA WACHEZAJI WA REAL MADRID

Thank you- #Madridistas!
Jude Bellingham

Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025 ni mchezo ambao ulikamilika kwa huzuni kwa Real Madrid baada ya Antonio Rüdiger na Lucas Vázquez, ambao walikuwa benchi baada ya kutolewa, kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kuonyesha utovu wa nidhamu wakiwa pembeni.

Jude Bellingham naye alionywa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho kwa tabia isiyo ya kiungwana.

MCHEZO ULIKUWAJE?

Matokeo
Matokeo ya mchezo

Mchezo ulianza vyema kwa Barcelona mara baada ya, Pedri kuwapa Barca uongozi katika dakika ya 28 kwa shuti la kuvutia kutoka nje ya eneo la hatari, huku Barcelona wakitawala kipindi cha kwanza.

Hata hivyo, Madrid walitawala kipindi cha pili wakati Kylian Mbappé, ambaye hakuanza kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu, aliingia uwanjani na kusawazisha kwa mkwaju wa faulo dakika ya 70.

Aurélien Tchouaméni aliwapa Real Madrid uongozi dakika saba baadaye kwa kichwa safi kutoka kona kabla ya Ferran Torres kusawazisha tena kwa shambulizi la kushtukiza dakika ya 84, na kupeleka mchezo hadi muda wa nyongeza.

Wakati ilionekana kama mshindi angepatikana kupitia mikwaju ya penalti, Koundé alifunga bao la ushindi lililoipa Barcelona taji na hatua ya kwanza kuelekea uwezekano wa kutwaa mataji matatu msimu huu.

Barcelona walitawala kipindi cha kwanza, Torres naye alikaribia kufunga kwa kichwa kilichogonga mwamba kabla ya mapumziko, katika kipindi kilichotawaliwa na Barca huku Real Madrid wakionekana kuwa na bahati ya kufungwa bao moja pekee.

Ancelloti abadili gia kipindi cha pili

Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025
Kylian Mbappe

Katika juhudi za kubadili hali, Ancelotti alimtoa Rodrygo na kumuingiza Mbappé, ambaye alibadilisha kabisa mchezo kwa ushirikiano wake wa kasi na Vinicius Junior.

Licha ya nafasi mbili za wazi za Vinicius Junior kuokolewa na kipa Wojciech Szczesny, Mbappé alifunga bao dakika ya 69 kwa mkwaju wa chini wa faulo hivyo mchezo kuwa Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025.

BARCELONA KUWAVAA INTER NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA JUMATANO

Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025 na baada ya sasa, Barcelona wanachukua ushindi huo kama motisha kuelekea mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan siku ya Jumatano. Pia wanaongoza LaLiga kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Madrid.

MASTAA WAZUNGUMZA BAADA YA MECHI

“Ilikuwa wakati mzuri kuwapa mashabiki kitu cha kushangilia. Tufurahi, lakini tusizidishe maana tuna nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya siku chache.

“Nimefurahi na nimechoka. Bila shaka, huu ndio mchezo mgumu zaidi kimwili niliowahi kucheza. Lakini sisi ni timu kubwa isiyokata tamaa. Inakuwa na ladha tamu zaidi, hasa ukiwaumiza Real Madrid kweli Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025,” alisema Ferran Torres, aliyechaguliwa mchezaji bora wa mechi.

KUHUSU ISHU YA MADRID KUGOMEA MAREFA

Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025, ilikuwa mechi ya kuvutia na yenye mvutano, ikichochewa na mvurugano wa Ijumaa baada ya Real Madrid kugoma kushiriki shughuli za kabla ya mechi wakipinga marefa wa FA ya Uhispania.

BARCELONA WAENDELEZA UBABE DHIDI YA MADRID

Barcelona mabingwa Copa Del Rey 2025 ukiachana na ubingwa huo, Barcelona wameifunga Madrid katika mechi zote tatu za El Clásico msimu huu. Waliwazidi nguvu Madrid 5-2 katika fainali ya Super Cup mwezi Januari baada ya kuifunga 4-0 katika LaLiga mwezi Oktoba.

Kipigo hiki kwa mahasimu wao ni pigo jingine kwa Real Madrid baada ya kutolewa katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Arsenal. Hii inaweza kuwa fainali ya mwisho kwa Carlo Ancelotti akiwa kocha wa Madrid.

Kocha huyo Muitaliano amesema atatoa uamuzi kuhusu mustakabali wake majira ya joto huku kukiwa na tetesi kuwa anatarajiwa kuinoa Brazil.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.