- Usajili wa Fei Toto unafuatiliwa na mamilioni ya watu kutoka ndani na nje ya Tanzania, mpaka sasa Simba, Yanga na Azam zote zimetajwa kumgombania.
- Yanga wameweka mezani ofa ya Milioni 750 ya usajili na mshahara wa Milioni 40.
- Simba walianzia Milioni 600, wanataka kuongeza.
Fei Toto kusaini Simba au Yanga? Ndio habari inayofuatiliwa na mamilioni ya wapenda soka Afrika wakati huu kukiwa na vita kali ya timu zinazosaka saini yake.
Simba, Yanga na Azam zote katika nyakati tofauti zimefanya mazungumzo na Fei Toto ili kuona uwezekano wa kumsaini kiungo mshambukliaji huyo wa Tanzania huku Simba na Yanga zikiongoza mbio, sasa je, Fei Toto Kusaini Simba au Yanga?
NINI KINAENDELEA KWENYE DILI LA FEI TOTO KUSAINI SIMBA AU YANGA?

Kwa mujibu ya mwandishi na mchambuzi, Hans Raphael kuhusu Fei Toto kusaini Simba au Yanga? muda wowote kuanzia sasa tajiri wa Simba, Mo Dewji atatua nchini ili kufanya mazungumzo na kambi ya Fei Toto.
Tayari Mo ameomba kikao na kambi ya Feisal na ikumbukwe awali Simba walimpa Fei Toto ofa ya mkataba wa miaka mitatu, wenye thamani ya Tsh 600m kama (sign on fee).
Simba waliahidi kutoa tsh 400m mwanzo na tsh 200m kwenye msimu wake wa pili ofa ambayo ilikataliwa. Ikumbukwe mezani Fei ana ofa ya Tsh 750m na mshahara wa tsh 40 kutoka Yanga.

MAKUBALIANO YA YANGA NA AZAM
Mchambuzi, Hans anaendelea kusema kuwa makubaliano yaliyowekwa kati ya Yanga na Azam ni endapo Fei atajiunga na timu yeyote tofauti na Simba basi Yanga watapata 25% ya mauzo.
Kama Fei atajiunga na Simba basi Azam watatakiwa kuilipa Yanga Tsh 1B. Hiki ni kizungumkuti kwa Fei, ni vita ya Yanga na Simba lakini pia Azam wanataka kumbakisha na wamefanya mazungumzo naye.
CHIKOLA AZIINGIZA VITANI YANGA, AZAM

Kutoka kwa mchambuzi, Hans amegusia pia kuwa Yanga wanapambana kusaka saini ya staa wa Tabora United Effen Chikola ambapo ameeleza nyota huyo ana makubaliano binafsi na Yanga, licha ya Azam kumtaka na tayari wametuma ofa chafu ya pesa ili kuwapiku Yanga.
TETESI ZA USAJILI HUKO ULAYA
Kutoka barani Ulaya tetesi za usajili kuelekea majira ya kiangazi nazo zinapamba moto ambapo makala haya yanaungana na mwandishi mashuhuri, Fabrizio Romano.
Fabrizio, ambaye anajulikana sana kwa taarifa zake sahihi na za haraka kuhusu usajili wa wachezaji, ameendelea kutoa taarifa moto moto kuhusu uhamisho wa wachezaji barani Ulaya.
Hapa kuna muhtasari wa taarifa mpya kabisa kuhusu usajili ambazo ameripoti hivi karibuni:
Usajili wa Victor Osimhen

Klabu ya Napoli inataka kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wao, Victor Osimhen, mapema kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa. Kifungu chake cha kuachiliwa ni €75 milioni, lakini Napoli wako tayari kujadiliana.
Manchester United na baadhi ya vilabu vya Saudi Arabia vinaonesha nia, ingawa mshahara wake mkubwa unaweza kuwa kikwazo.
Ian Maatsen kuelekea Aston Villa
Ian Maatsen wa Chelsea yuko karibu kujiunga na Aston Villa kwa ada ya £37.5 milioni. Makubaliano ya binafsi karibu yamekamilika, na mkataba unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni. Borussia Dortmund walikuwa na nia, lakini sasa wamejiondoa katika mazungumzo.
Geovany Quenda kuelekea Chelsea
Chelsea wamekamilisha makubaliano na Sporting CP kwa ajili ya kumsajili winga chipukizi Geovany Quenda, atakayejiunga mwaka 2026. Ada ya uhamisho inakadiriwa kuwa kati ya €45 hadi €50 milioni. Quenda, mwenye umri wa miaka 18, amevutia wengi msimu huu na mechi 40, mabao 2 na pasi za mwisho 7.
Xabi Alonso kuelekea Real Madrid?

Kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso, anatajwa kuwa chaguo la kwanza la Real Madrid kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti. Mazungumzo yanaendelea, huku Leverkusen wakifahamu hali hiyo. Alonso alikataa ofa kutoka Ligi Kuu England na Bayern Munich, huenda akawa alikuwa akisubiri nafasi hii ya Real Madrid.
Robbie Ure kujiunga na IK Sirius
Aliyekuwa mshambuliaji wa Rangers, Robbie Ure, anatarajiwa kujiunga na klabu ya IK Sirius ya Sweden kwa ada ya €750,000, baada ya kushindwa kupata nafasi Anderlecht. Anatazamiwa kuanza upya maisha ya soka katika ligi ya Allsvenskan.
Liverpool kwenye Soko la Usajili

Liverpool wanatafuta mchezaji mpya wa beki wa pembeni kwa dau la €33 milioni na pia wanafikiria kumsajili Carney Chukwuemeka kwa mkopo. Pia kuna uvumi kuhusu ofa ya £70 milioni kwa Darwin Núñez kutoka vilabu vya Saudi Arabia.

