KibabageKibabage
  • Simba SC inayonolewa na Fadlu Davids ukuta wake umetunguliwa mabao machache ndani ya ligi 2024/25.
  • Fountain Gate inatia huruma kwenye eneo la ulinzi ikiwa ni timu iliyofungwa mabao mengi ambayo ni 51.
  • Ken Gold yashuka daraja na mengi, uchungu na mateso kwenye kuokota mipira mingi nyavuni.

Kuna timu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika zimefungwa mabao machache kutokana na uimara wa safu ya ulinzi msimu wa 2024/25.

Aziz KI V Chemalone
Aziz Ki kiungo wa Yanga akitafuta njia mbele ya beki wa Simba Che Malone. Source: Yanga.

Ipo wazi kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni mabingwa watetezi wa taji la ligi, kwenye msimamo ni namba moja wanafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili.

Kwa sasa ni mzunguko wa pili ndani ya ligi huku ukuta wat imu ambayo imeruhusu mabao mengi yakufungwa ni ule wa Fountain Gate ambayo imetunguliwa mabao 51 baada ya mechi 27.

Ken Gold ambayo rasmi imeshuka daraja kutoka Mbeya ni namba mbili kwa timu iliyofungwa mabao mengi  ambayo ni 50. Baada ya kucheza mechi 27 ina pointi 16 ni mechi tatu zimebaki ikiwa itashinda itafikisha pointi 25ambazo zimeshapitwa na Tanzania Prisons yenye pointi 27 nafasi ya 14.

HIZI ZIMEFUNGWA KIDUCHU

 SIMBA SC

Wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 57 baada yakucheza mechi 22, ukuta wa Simba SC ni namba moja kwa kufungwa mabao kiduchu ambayo ni 8 na kipa namba moja Moussa Camara alifungwa mabao yote hayo.

Camara kwenye mazoezi ya Simba Misri
Camara Moussa kipa namba moja wa Simba ambaye ana hati safi 15 kwenye ligi 2024/25. Source: Simba.

Licha ya makosa ambayo safu ya ulinzi imekuwa ikifanya yale yanayojirudia bado kazi kubwa ilifanyika kwa mlinda mlango Camara ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Miongoni mwa mechi ambazo alifungwa ilikuwa kweye mchezo dhidi ya Yanga ikiwa ni mchezo ambao Simba ilipoteza katika mzunguko wa kwanza jitihada za beki Shomari Kapombe kuokoa krosi ya Maxi Nzengeli ziligonga mguu wa Kelvin Kijili ambaye alijifunga kwenye mchezo huo.

Kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, mabao yote Camara alitunguliwa nje ya 18 baada ya wachezaji wa Coastal Union kusoma madhaifu yake na namna safu ya ulinzi ilivyokuwa ikifanya makosa kwenye kukaba hasa mpira ukiwa nje ya 18.

Mzizima Dabi, Uwanja wa Mkapa, Camara alitunguliwa mabao mawili ambapo moja alilofungwa na Gibril Sillah linaingia kwenye orodha ya bao la mapema zaidi kufungwa na bao la pili alifungwa na Zidane dakika ya 86.

MABINGWA WATETEZI YANGA

Kwenye msimamo wa ligi Yanga ni namba moja chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ni mabao 10 ukuta wa timu hiyo uliruhusu na mchezo ambao walifungwa mabao mengi ilikuwa Yanga 1-3 Tabora United.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex langoni alianza kipa namba moja Djigui Diarra ambapo Yanga ilipoteza pointi tatu mazima baada ya dakika 90.

Job
Dickson Job beki wa Yanga ambao ni mabingwa watetezi. Source: Yanga.

Mchezo wa pili Yanga kutunguliwa mabao mengi ilikuwa Yanga 3-2 Mashujaa, mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex wakati Yanga ikisepa na pointi tatu mazima huku rekodi ya hat trick ikiandikwa ndani ya msimu wa 2024/25 mtupiaji alikuwa ni Prince Dube, ilikuwa ni Desemba 19 2024

Diarra ana hati safi 14 kwenye ligi akiwa ni chaguo la kwanza na Yanga inaongoza  ligi ikiwa na jumla ya pointi 70 baada ya mechi 26.

MATAJIRI WA DAR AZAM FC

Matajiri wa Dar, Azam FC kwenye msimamo wa ligi wamekusanya pointi 54 nafasi ya tatu na pia kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ndani ya ligi ni namba tatu ikiwa imeruhusu mabao17 pekee kwenye mechi 27.

Matajiri hao wameshajiondoa kwenye mbio za kuwania ubingwa kutokana na pointi walizonazo na mechi zilibaki kuwa ngumu kwao kufikia malengo hayo.

Ikiwa watapata pointi tatu kwenye mechi tatu watavuna alama tisa ambazo zitawafanya wakamilishe mzunguko wa pili wakiwa na pointi 63, pointi hizo Yanga wamevuka hivyo hawatakuwa na kigezo cha kuwa namba moja.

SINGIDA BLACK STARS

Kipa namba moja wa Singida Black Stars ni Metacha Mnata. Uwanja wa Liti unatumiwa na Singida Black Stars kwenye mechi za nyumbani ambapo walikuwa wanashiriki Kombe la Muungano wameshafungashiwa virago huko.

Singida Black Stars ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 53 baada ya kucheza mechi 27 ni mabao 21 safu ya ulinzi imefungwa kwenye mechi za ushindani.

WAJEDA JKT TANZANIA

Fei v JKT Tanzania
Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum akipambana na nyota wa JKT Tanzania, Machezo. Source: Azam FC.

JKT Tanzania ipo ndani ya tano bora kwa timu ambazo zimeruhusu mabao machache yakufungwa kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi.

JKT Tanzania ni mabao 24 imefungwa ikiwa namba tano kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache kwenye msimamo ipo nafasi ya  7 ikiwa na pointi zake 32.

Share this: