Mohamed SalahMohamed Salah
  • Salah rekodi zake ndani ya Premier League 2024/25 ni balaa tupu akihusika kwenye mabao 45.
  • Manchester United inasikitisha haipo ndani ya 10 bora kwenye msimamo.
  • Jumamosi na Jumapili rimoti hazigusiki kabisa gemu zote balaa zito.

MOHAMED Salah nyota wa Liverpool raia wa Misri iliyopo katika bara la Afrika ni namba moja katika wakali na kucheka na nyavu Premier League 2024/25 akiwa ametupia jumla ya mabao 27.

Salah (-)
Salah mshambuliaji wa Liverpool ambaye ni kinara kwenye chati ya utupiaji akiwa na mabao 27 na pasi 18 za mabao 2024/25. Source: Liverpool.

Mohamed Salah amekuwa katika ubora kwenye mechi za Premier League kutokana na kuhusika kwenye mchango mkubwa wa mabao ndani ya timu hiyo ambayo inaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 79 baada yakucheza jumla ya mechi 33.

Liverpool inapewa chapuo kubwa kutwaa ubingwa ambao upo mikononi mwa Man City iliyo nafasi ya tatu kibindoni imekusanya jumla ya pointi 61 baada yakucheza jumla ya mechi 34.

Ukiweka kando suala la kufunga kwa Salah katengeneza pasi 18 za mabao akiwa ni namba moja katika eneo hili pia anafuatiwa na Bukayo Saka wa Arsenal ambaye katoa pasi 10 za mabao sawa na Antonee Robinson wa Fulham na Jacob Murphy wa Newcastle United.

Salah amehusika kwenye mabao 45 kati ya 75 yaliyofungwa na timu hiyo ukiwa ni mchango mkubwa kwa nyota huyo ndani ya uwanja katika mechi za ushindani jambo ambalo linaongeza thamani yake.

ISAK NAYE SIO KITOTO

Alexander Isak wa Newcastle United katupia mabao 21 kati ya 62 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 5 kwenye msimamo. Pointi 59 kibindoni kwa timu hiyo baada ya kucheza mechi 33 uwanjani.

Isak
Isak katupia jumla ya mabao 21 ndani ya Premier League 2024/25. Source: Newcastle United.

Ushindani umekuwa ni mkubwa kwa kila timu inayoshuka uwanjani kwenye msako wa pointi tatu muhimu kutokana na ubora wa wachezaji waliopo ndani ya ligi hiyo ambayo inaongozwa kwa kufuatiliwa na wengi duniani.

HAALAND ANAKUJA
Mkali wa kucheka na nyavu Erling Haaland wa Man City anakuja kwa kasi yake akiwa katupia mabao 21 kati ya 66 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 3 kwenye msimamo.  City ni mabingwa watetezi wapo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 34 kibindoni wana pointi 61.

Haaland
Erling Haaland wa Man City katupia mabao 21 msimu wa 2024/25. Source: Man City.

WOOD

Chris Wood wa Nottingham katupia mabao 19 kati ya 53 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya nne ikiwa na jumla ya pointi 60 baada yakucheza mechi 33. Ilipata ushindi kwenye mechi 18 ikipoteza mechi 9 na kuambulia sare kwenye mechi sita ndani ya uwanja.


BRYAN
Nyota Bryan Mbeumo wa Brentford katupia mabao 18 kati ya 56 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 11 kwenye msimamo ikiwa imecheza jumla ya mechi 33 ilipata ushindi kwenye mechi 13 sawa na idadi iliyopoteza na kuambulia sare 7.

HAWA NA REKODI YA KADI NYEKUNDU

Ipo wazi kwamba kila mchezaji ana rekodi yake ambapo kwa upande wa nyota walioonyeshwa kadi nyekundu zaidi ya moja ndani ya msimu wa 2024/25 wapo wakiongozwa na Jack Stephens wa Southampton, Myles Lewis Skelly wa Arsenal na Bruno Fernandez wa Manchester United hawa wanaingia kwenye orodha ya nyota walioonyeshwa kadi mbili nyekundu.

JUMAMOSI NI MOTO HUKO

Aprili 26 2025, Chelsea iliyo nafasi ya sita na pointi 57 itakuwa kazini kumenyana na Everton iliyo nafasi ya 13 na pointi 38 ikiwa ni wiki ya 34 ambapo kila timu inaingia kusaka pointi tatu muhimu kwa mbinu za uwanjani.

Southampton iliyo nafasi ya 20 na pointi 11 baada ya kucheza mechi 33 itawakaribisha Fulham ilyo nafasi ya 9 na pointi 48 nayo itakuwa ni Jumamosi ya Aprili 26 kwa wababe hawa kuzisaka pointi tatu ndani ya dakika 90.

Brighton yenye pointi 48 nafasi ya 10 itakuwa kazini dhidi ya West Ham yenye pointi 36 nafasi ya 17 kwenye msimamo. Newcastle United iliyo nafasi ya 5 na pointi zake 59 itakuwa kibaruani dhidi ya Ipswich iliyo nafasi ya 18 na pointi 21 kibindoni.

JUMAPILI APRILI 27 HAIPO

Wolves yenye pointi 38 nafasi ya 15 itakuwa kazini  dhidi ya Leicester iliyo nafasi ya 19 na pointi 18 huku Bournemouth iliyo nafasi ya 8 itawakaribisha Manchester United iliyo nafasi ya 14 na pointi 38 hizi zote itakuwa ni Aprili 26 na unaweza kubashiri kupitia SportPesa ukakunja mkwanja wako. Vinara Liverpool watalabiliana na Tottenham.

Source: Premier League.

Share this: