Ahmed ArajigaAhmed Arajiga

AHMED Arajiga ametangazwa kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 8 2025 ambapo wababe wawili wanatarajiwa kukutana Yanga na Simba kwenye Kariakoo Dabi ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Ikumbukwe kwamba Arajiga alikuwa mwamuzi kwenye mchezo wa Mzizima Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Azam FC wababe hao walipogawana pointi mojamoja baada ya mchezo kukamilika. Rekodi nyingine alikuwa ni mwamuzi wa kati mchezo wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa 0-1 Azam FC katika mchezo huu Ibrahim Bacca alionyeshwa kadi nyekundu.

Bacca na Ateba
BACCA na Ateba kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza msako wa pointi tatu Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ni Ramadhan Kayoko alikuwa ni mwamuzi wa kati ila mzunguko wa pili jina lake halipo kwenye orodha ya waamuzi. Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga, bao la Kelvin Kijili aliyejifunga lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Karim Boimanda Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) amesema kuwa kwenye asilimia ya maandalizi wapo juu sana kutokana na kila kitu kuwa kwenye mpangilio mzuri huku akiwataja watakaosimamia mchezo huo.

Salim Singano, Mohamed Mkono, (mwamuzi msaidizi namba moja) hawa kutoka Tanga Kassim Mpanga, (mwamuzi msaidizi namba mbili) kutoka Dar, Amina Kyando,(mwamuzi wa akiba)  kutoka Morogoro, Soud Abdi kutoka Dar ikiwa ni baadhi ya maofisa kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwamuzi wa kati atakuwa Ahmed Arajiga.

Arajiga --
Arajiga mwamuzi ambaye atasimamia sheria 17 Kariakoo Dabi, Machi 8 2025 Uwanja wa Mkapa. Source: Honest

MUKWALA NA ATEBA

Mastaa wawili kwenye eneo la ushambuliaji ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, ngoma ni nzito kutokana na kuliamsha dude kwenye eneo la ufungaji katika mechi ambazo wamechza.

Ni Machi 8 2025 Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa kazini kwa wababe wawili Yanga na Simba kukutana uwanjani kwenye msako wa pointi tatu huku Yanga katika eneo la ushambuliaji wakiwa na rekodi bora Simba wakifuata.

Ni mabao 58 safu ya ushambuliaji ya Yanga imetupia huku ile ya Simba ikiwa na mabao 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 na Yanga ni mechi 22 imecheza msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa mwanzo mwisho.

Ateba ni dakika 1,117 kakomba uwanjani akifunga mabao 8 na pasi tatu za mabao katika mechi 17 ambazo alipata nafasi huku Mukwala akiwa amecheza jumla ya mechi 19 akikomba dakika 666 akifunga mabao 8 na pasi mbili za mabao.

DUBE NA MZIZE WANAPETA

Wakati Mukwala na Ateba ikiwa ni pasua kichwa kwa upande wa Yanga, washambuliaji wawili Prince Dube na Clement Mzize wote wanapeta kutokana na benchi la ufundi la Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kuwa na mfumo wa kutumia washambuliaji wawili.

Clement Mzize na Dube
Clement Mzize na Dube washambuliaji wa Yanga wote wametupia mabao 10 ndani ya ligi. Source: Yanga.

Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba ubao uliposoma Pamba Jiji 0-3 Yanga wakali wote wawili walianza kikosi cha kwanza hivyo wao wanapeta kutokana na benchi la ufundi kutambua namna ya kuwatumia wote ndani ya uwanja.

Kocha Mkuu, Miloud Hamdi aliwatumia wote pia kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa 0-5 Yanga walipokomba pointi tatu ugenini mazima kwenye mchezo wa ligi.

WAKALI KWENYE KUCHEKA NA NYAVU

Katika eneo la kucheka na nyavu kuna wakali kutoka kila kona hivyo eneo hili linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ndani ya dakika 90 zakuvuja jasho uwanjani. Yanga kuna wakali wawili ambao wametupia mabao 10, Clement Mzize ambaye ni mzawa na Prince Dube ambaye huyu ni rai awa Zimbabwe kazi kubwa itakuwa kwa wababe hawa kusaka rekodi ndani ya Uwanja wa Mkapa.

Kuna Pacome, Aziz Ki hawa wakali wametupia mabao 7 kila mmoja hivyo ni miongoni mwa wachezaji wenye njaa yakufunga wakiwa uwanjani kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi. Kwa upande wa Simba kinara ni Jean Ahoua ambaye huyu katupia mabao 10 na kutengeneza pasi sita za mabao akihusika kwenye mabao 16 ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Fadlu.

VIINGILIO HIVI HAPA

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kuelekea kwenye mchezo huo ambapo mzunguko ni 5,000, machungwa 10,000, VIP C 20,000, VIP B 30,000.

Share this: