M- CamaraM- Camara

MLINDA mlango namba moja wa Simba, Moussa Camara ameandika rekodi yake ya kuwa namba moja kwa makipa wenye hati safi ndani ya uwanja akiwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids akiwa kwenye vita kubwa na kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra katika kuwania tuzo ya kipa bora.

Camara Air
Camara kipa namba moja wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids 2024/25.

Camara ndani ya ligi ni mechi 18 kacheza akikomba dakika 1,620 akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliokomba dakika nyingi ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani. Simba imecheza mechi 18 za ligi na zote alianza langoni.

Camara kafungwa mabao sita ndani ya ligi namba nne kwa ubora kafungwa ilikuwa mabao mawili dhidi ya Coastal Union, mawili dhidi ya Kagera Sugar, bao moja dhidi ya Yanga na bao moja dhidi ya Fountain Gate. Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni mabingwa watetezi wa ligi na mchezo wao uliopita walishinda mabao 6-1 dhidi ya KMC.

Kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ambapo Camara alionekana kufanya makosa katika kuokoa mpira wa faulo iliyopigwa na kiungo Clatous Chama uliporudi ndani ya uwanja ukakutana na Maxi Nzengeli ambaye alipiga krosi kuelekea langoni ikakutana na Kapombe Shomari ambaye aliokoa hatari hiyo.

Wakati Kapombe akimalizia kuokoa hatari beki wa Simba, Kelvin Kijili aliyekuwa karibu na lango la Simba mpira ule ukamgonga na kuzama mazima nyavuni, Simba ikayeyusha pointi tatu mazima. Kipa wa Yanga, Djigui Diarra amekaa langoni kwenye mechi 12 akikomba dakika 1,080 ni mabao matano kafungwa kipa huyo ndani ya msimu wa 2024/25 akiwa na hati safi 9.

Maandalizi ya mchezo wetu wa Ijumaa dhidi ya KMC FC #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
Kiungo wa Yanga, Clatous Chama akiwa kwenye maandalizi ya mechi za ligi. Source: Yanga.

Ni Machi 8 2025 inatarajiwa kuchezwa Kariakoo Dabi kwa wababe hao kukutana ndani ya uwanja katika msako wa pointi tatu muhimu. Vita yao inatarajiwa kuendelea kwa wababe hao wawili kwenye msako wa hati safi na pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

MASHINE YA KAZI YARUDI

Mashine ya kazi ndani ya kikosi cha Simba, Kibu Dennis imerejea baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti kwa kuwa alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United ambao baada ya dakika 90 ilikuwa Tabora United 0-3 Simba.

Kibu alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate walipotoshana kwa kufungana bao 1-1 na mchezo wa Tanzania Prisons wakati Simba ikishinda mabao 3-0 Uwanja wa KMC, huku mtoto wa maajabu Ladack Chasambi akiwa ni mgeni rasmi na alianza kikosi cha kwanza ikumbukwe kwamba ni Chasambi alijifunga kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate.

Zimbwe v Fountain Gate
Nahodha Zimbwe wa Simba akiwa kwenye majukumu mchezo dhidi ya Fountain Gate ambao Kibu alikosekana. Source: Simba.

Msimu wa 2024/25 Kibu hajafunga bao ndani ya ligi ila ni chaguo la kwanza la kocha Fadlu kutokana na uwezo alionao kwenye matumizi ya nguvu kupambana na mabeki wa kazi ndani ya ligi namba nne kwa ubora. Ikumbukwe kwamba wakati Simba ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars Kibu alikuwa miongoni mwa nyota walioanza kikosi cha kwanza na alikuwa akipambana na mabeki zaidi ya wawili wakiongozwa na Kenedy Juma ambaye ni nahodha wa Singida Black Stars.

Katika mchezo huo bao la Simba lilifungwa na Fabrince Ngoma ambaye alitumia pasi ya Jean Ahoua aliyepiga kona akiwa nje ya 18 na mwisho Simba wakasepa na pointi tatu mazima.

Mchezo ujao kwa Simba dhidi ya Namungo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Februari 19 2025 kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu kwa timu zote kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

NAMUNGO MWENDO WAKE

Namungo kwenye msimamo wa ligi ni namba 9 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 21 baada ya kucheza mechi 19. Ni ushindi kwenye mechi 6, sare katika mechi tatu na ilipoteza pointi tatu mazima kwenye mechi 10 ambazo ni dakika 900 ikiwa haijawa kwenye mwendo bora ndani ya uwanja kwenye rekodi za ushindi.

Inakutana na Simba ambayo baada ya kucheza mechi 18 ni ushindi kwenye mechi 15 ikiambulia sare kwenye mechi mbili na ilipoteza mchezo mmoja ilikuwa ni Kariakoo Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga kwa bao la kujifunga la Kelvin Kijili.

Ikumbukwe kwamba Simba ni namba moja kwa timu ambazo zimeruhusu mabao machache ya kufungwa ambayo ni sita huku Namungo ikiwa imeruhusu jumla ya mabao 23 hivyo kwenye safu ya ulinzi ya Namungo watakuwa na kazi kupambana kufuta makosa yao. Kwa upande wa ushambuliaji Namungo ni mabao 15 safu ya ushambuliaji imetupia na inakutana na Simba ambayo imetupia jumla ya mabao 38 kibindoni.

HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA

Yanga v Singida, Black Stars, KMC Complex

Fountain Gate v Tabora United, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara hizi mbili zitapigwa Februari 17 2025.

FEBRUARI 18 2025

Ken Gold v Kagera Sugar, Uwanja wa Sokoine, Mbeya

KMC v JKT Tanzania, Uwanja wa KMC, Complex, Dar

Dodoma Jiji v Tanzania Prisons, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma

FEBRUARI 19 2025

Mashujaa v Pamba, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma

Namungo v Simba, Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Share this: