Chama JrChama Jr

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi amesema kuwa hesabu kubwa kwenye mechi ambazo wanacheza kwa sasa sio kufunga mabao mengi ndani ya dakika 90 bali ni kuona kwamba wanapata pointi tatu muhimu baada ya dakika 90 akipotezea idadi ya ushindi wa mabao mengi ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.

Hamdi Yanga
Hamdi Miloud, Kocha Mkuu wa Yanga mchezo wake wa kwanza kukaa benchi ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania. Source: Yanga.

Yanga ni timu namba moja kwa timu ambazo zimefunga mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika wakiwa wamefunga mabao 42 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 ambazo ni dakika 1,620 wakiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 38.

Mchezo uliokusanya mabao mengi kwa timu hiyo ilikuwa Yanga 6-1 Ken Gold uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex na ilishuhudiwa bao la maajabu Djigui Diarra akifungwa na Suleman dakika ya 87 akiwa katikati ya uwanja, sare yao ya kwanza kwa msimu wa 2024/25 waliipata mbele ya JKT Tanzania baada ya ubao kusoma JKT Tanzania 0-0 Yanga.

Hamdi ameweka wazi kuwa malengo makubwa kwenye mech izote zilizopo mbele yao ni kupata pointi tatu muhimu jambo ambalo wanalifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi.

“Kupata ushindi wa mabao mengi hilo sio kipaumbele chetu bali mpango mkubwa ni kuona kwamba kwenye mechi zetu ambazo tunacheza tunapata pointi tatu muhimu kwa kuwa hicho ndicho ambacho tunahitaji.”

Baada ya kucheza mechi 18 Yanga inayodhaminiwa na SportPesa imekusanya jumla ya pointi 46 kibindoni nafasi ya pili mchezo ujao ni dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex, Februari 14 2025. Vinara ni watani zao wa jadi Simba wenye pointi 47 nao wamecheza mechi 18.

MKALI WA MABAO

Mkali wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga ni Clement Mzize ambaye amefunga jumla ya mabao 9 ndani ya msimu wa 2024/25 akiwa katika kikosi cha Yanga ambacho kinapambana kutetea taji la ligi. Mzize sio kufunga tu bali anauwezo wa kupiga pasi za mabao kama afanyavyo Clatous Chama, Aziz Ki na Maxi ambao ni viungo wa Yanga.

Mzize v Prisons
Clement Mzize kiungo wa Yanga akiwa kwenye majukumu yake ndani ya ligi 2024/25. Source: Yanga.

Mzize alifungua akaunti yake ya mabao kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar zama za Miguel Gamondi ambapo kwenye mchezo huo alianzia benchi na alipoingia alipachika bao Uwanja wa Kaitaba uliposoma Kagera Sugar 0-2 Yanga, bao la kwanza kwa Yanga lilifungwa na Maxi Nzengeli.

Maxi Nzengeli
Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga, mfungaji wa bao la kwanza ndani ya kikosi hicho msimu wa 2024/25 kwenye ligi. Source: Yanga.

Mchezo huo ulichezwa Agosti 29 2024 Uwanja wa Kaitaba ambapo Yanga ilisepa na pointi tatu mazima, walipokutana kwa mara nyingine na Kagera Sugar, Uwanja wa KMC, Complex kwenye ushindi wa mabao 4-0 Mzize alifunga bao moja katika mchezo huo akimtungua Ramadhan Chalamanda.

Ilikuwa ni Februari Mosi 2025 dakika ya 31 Mzize akitumia mguu wake wa kulia alipachika bao hilo na kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold alifunga mabao mawili ilikuwa dakika ya 6 na 42 mabao yote mawili alifunga kwa kutumia mguu wa kulia akiwa ndani ya 18.

Mzize mguu wake wenye nguvu akiwa ndani ya uwanja ni wa kulia kwa kuwa amekuwa akiwapa makipa wengi mateso kwa kuwaadhibu akiwa kwenye majukumu yake jambo linalomfanya kuwa mtambo wa mabao katika kikosi cha Yanga.

Kahusika kwenye mabao 13 kati ya 42 yaliyofungwa na timu hiyo ambayo inaongoza kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi.Kafunga mabao 9 na kutoa pasi nne za mabao akitumia dakika 968 kwenye mechi 17 ambazo alipata nafasi ya kucheza.

KITUO KINACHOFUATA

Kituo kinachofuata kwa Yanga ni dhidi ya KMC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex. KMC ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 18 imekusanya pointi 22 haijawa kwenye mwendo mzuri katika mechi zake mbele ya Yanga.

Ushindi kwa KMC kwenye ligi ni mechi 6, ilitoshana nguvu na wapinzani wao katika mechi 4 na ilipoteza kwenye mechi 8. Safu yake ya ushambuliaji haijawa imara ikitupia jumla ya mabao 13 kwenye mechi 18 huku ukuta ukiruhusu jumla ya mabao 23.

Duke Abuya
Duke Abuya nyota wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa 2024/25. Source: Yanga.

KMC inakutana na Yanga ambayo imepata ushindi kwenye mechi 15, ilitoshana nguvu mchezo mmoja na ilipoteza mchezo michezo miwili. Safu ya ushambuliaji ya Yanga imetupia mabao 42 na ukuta ukiruhusu kufungwa mabao 7 pointi za oni 46 wakiwa wanapambana kurejea namba moja kwenye msimamo.

Rekodi zinaonyesha kuwa KMC kwenye ligi walipata ushindi mara moja pekee dhidi ya Yanga. Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 KMC, mwamuzi alikuwa Ahmed Arajiga Septemba 29 2024.

Share this: