YANGA imefunga jumla ya mabao 42 ikiwa nit imu namba moja kuwa na safu kali ya ushambuliaji kwa msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa huku wakiwa ni vinara wa ligi namba nne kwa ubora Afrika.

Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ilianza kwa mwendo wa kinyonga ndani ya msimu kabla ya kurejea kwenye ubora wake kwa kupata matokeo chanya katika mechi za ushindani ndani ya ligi.
Timu hiyo inashikilia rekodi yakupata ushindi mkubwa kwenye mechi za ligi ambapo rekodi hiyo iliandikwa Uwanja wa Azam Complex, Februari 5 2025 walipokuwa wakisaka pointi tatu mbele ya Ken Gold.
PICHA ILIVYOKUWA KMC COMPLEX

Katika mchezo huo ikiwa ni baada ya Sead Ramovic kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo pointi tatu zote zilibaki Yanga ambayo ilipata ushindi wa mabao 6-1.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Prince Dube aliyefunga mabao mawili dakika ya 2,46 mshambuliaji Clement Mzize alipachika mabao mawili dakika ya 6 na 42 dakika ya 38 Pacome alipachika bao moja na bao la sita lilipachikwa na Duke Abuya dakika ya 85.
Kwenye mchezo huo Duke Abuya alianzia benchi na alipoingia alifunga bao moja kukamilisha kamba ya sit ana Yanga kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa zaidi ndani ya ligi.
Pacome anafikisha mabao 7 kwenye ligi akiwa kiungo mwenye mabao mengi ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinaongoza ligi huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa Simba.
KIKOSI CHA YANGA KILICHOANZA

Djigui Diarra, Israel Mwenda, Boka, Dickson Job ambaye amevaa kitambaa cha unahodha,Khalid Aucho, Clement Mzize.
Mudathir Yahya, Prince Dube, Aziz Ki, Pacome hawa walianza kikosi cha kwanza na wachezaji wa akiba ni Mshery, Kibwana Shomary, Nodo, Sure Boy, Shekhan, Maxi, Abuya, Ally, Chama, Kennedy Musonda ilikuwa ni Februari 5 2025.
MAKOCHA WATOA YAMOYONI
Kocha Msaidizi wa Ken Gold, Omar Kapilima ameweka wazi kuwa makosa ambayo waliyafanya kwenye mchezo huo yaliwagharimu jambo ambalo likawafanya wakose ushindi ndani ya dakika 90.
“Tulifanya makosa kwenye mchezo wetu yakatugharimu tukafungwa hivyo tutakwenda kufanyia kazi makosa ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zijazo.”
KOCHA WA YANGA HUYU HAPA
Kaimu Kocha wa Yanga, Abdihamid Moalin amebainisha kuwa kazi kubwa inafanywa na wachezaji kutafuta ushindi hivyo wanastahili pongezi kutokana na kazi ambayo wanaifanya ndani ya uwanja.
“Wachezaji wanastahili pongezi kwa kutafuta ushindi na inakuwa ni zawadi kwa kocha Sead Ramovic kwa kuwa amekuwa akiwapa mbinu ambazo zinaleta matokeo. Kwa namna ambavyo ipo wachezaji hawa wanafanya kazi kubwa hilo wanastahili pongezi.
“Ukiwa na wachezaji kama hawa, kila kocha anayekuja anakutana na kikosi bora hivyo jukumu linakuwa kwenye kufanikisha malengo ambayo ni kupata ubingwa ndani ya timu.”
YANGA NA REKODI ZAO
Yanga inafikisha jumla ya mabao 42 ndani ya ligi baada ya kucheza mechi 17 inakuwa timu namba moja kufunga mabao mengi huku ikiongoza ligi na pointi zake kibindoni 45 inafuatiwa na Simba nafasi ya pili yenye pointi 44.
Kinara wa utupiaji ni mzawa Clement Mzize mwenye mabao 9 na pasi nne za mabao anafuatiwa na Leonel Ateba wa Simba na Elvis Rupia wa Singida Black Stars hawa wote wametupia mabao 8. Rekodi za Yanga zimeipoteza Simba ndani ya ligi kutokana na balaa ambalo wanaonyesha ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.
Ipo wazi kwamba Yanga inakuwa ni timu ya kwanza kufunga mabao mengi zaidi katika mchezo mmoja, Yanga 6-1 Ken Gold katika mchezo uliopita Yanga ilipata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Mbali na hilo pia Yanga ni timu ya kwanza kufungwa bao kutoka katikati ya Uwanja wa KMC, Complex mtupiaji akiwa ni Suleman Rashid dakika ya 87, pigo la mpira wa Rashid lilimshinda mlinda mlango namba moja wa Yanga Djigui Diarra.
HII HAPA RATIBA YA FEBRUARI 7
Coastal Union nafasi ya 11 na pointi 18 v JKT Tanzania iliyo nafasi ya 8 na pointi 19, saa 10:00 jioni
Singida Black Stars nafasi ya 4 na pointi 33 dhidi ya Kagera Sugar,nafasi ya 15 pointi 11 saa 10:00 jioni.
FEBRUARI 9
Pamba Jiji v Azam FC, saa 10:00 jioni
Namungo v Dodoma Jiji, saa 10:00 jioni
FEBRUARI 10
KenGold v Fountain Gate, saa 8:00 mchana
KMC V Singida Black Stars, saa 10:15 jioni
JKT Tanzania v Yanga, saa 10:15 jioni

