Ahoua Jean- AwesuAhoua Jean- Awesu

SIMBA, Yanga, Singida Black Stars zinapambana kufanya kweli kwenye eneo la ushambuliaji huku Azam FC kwa 2024/25 wakiwa na staa namba moja kwenye kutengeneza pasi za mwisho ambaye ni Feisal Salum mwenye pasi 9 za mabao.

Ramovic Sead
Ramovic Sead Kocha Mkuu wa Yanga mwenye tuzo ya kocha bora Desemba 2024. Source: Yanga.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa imekuwa kwenye ubora wake kwenye mechi za hivi karibuni na mchezaji wao Clement Mzize ametwaa tuzo ya mchezaji bora na kocha Sead Ramovic ametwaa tuzo ya kocha bora ilikuwa ni kwa Desemba 2024.

Hapa tunakuletea wakali wa kucheka na nyavu ndani ya 2024/25 namna walivyofunga 2024 kwa ajili ya ukurasa mpya 2025 namna hii:-

WAKALI KWENYE KUCHEKA NA NYAVU

ELVIS RUPIA

Rupia
Rupia mshambuliaji namba moja kwa utupiaji yupo Singida Black Stars. Source: Singida Black Stars.

Nyota huyu wa Singida Black Stars ni namba moja kwenye kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa katupia mabao 8 na katoa pasi moja.

Singida Black Stars kwenye msimamo wa ligi ni namba nne ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 16 safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 22.

JEAN AHOUA

Kiungo mshambuliaji wa Simba ni namna moja kwenye kucheka na nyavu ndani ya kikosi cha Simba na namba mbili kwenye ligi kiujumla. Katupia mabao 7 na pasi tano za mabao chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Nyota huyu nim kali kwenye mapigo huru ikiwa ni penalti na faulo. Miongoni mwa timu ambazo alifunga kwa pigo la faulo ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba ambao ulikamilika kwa ubao kusoma Kagera Sugar 2-5 Simba.

Simba kwenye msimamo ni namba moja ikiwa imetupia mabao 31 na kukusanya pointi 40 kibindoni baada ya kucheza mechi 15 za ligi. Ushindi ni kwenye mechi 13 sare moja na ilipoteza mchezo mmoja ilikuwa dhidi ya Yanga mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Simba 0-1 Yanga bao la kujifunga la Kelvin Kijili.

SELEMAN MWALIMU

Gomez
Seleman Mwalimu, mshambuliaji wa Fountain Gate 2024/25. Source: Fountain Gate.

Mshambuliaji huyu wa Fountain Gate amegotea kwenye mabao sita akifunga 2024 akiwa hapo na kazi mpya inatarajiwa kuwa ndani ya 2025 kusaka ushindi kwenye mechi za ushindani.

Fountain Gate ni nafasi ya sita ipo kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 16 imekusanya jumla ya pointi 20. Safu ya ushambuliaji ya Fountain Gate imefunga jumla ya mabao 24.

MZIZE

Mzize
Mzize Clement mshambuliaji wa Yanga mwenye mabao sita ndani ya ligi 2024/25. Source: Yanga.

Clement Mzize ni namba moja kwa watupiaji ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kufikisha mabao sit ana bao lake la sita alifunga kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate ulichezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Mzize ametupia mabao sita na katoa pasi nne za mabao baada ya kucheza mechi 14 kati ya 15 ambazo zimechezwa na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Mabingwa hawa watetezi wamekusanya pointi 39 na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 32 ikiwa inaongoza kwa timu zenye mabao mengi ndani ya ligi kwa wakati huu.

 

LEONEL ATEBA

Leonel Ateba
Mshambuliaji wa Simba, Leonel Ateba mwenye mabao matano ndani ya ligi 2024/25. Source: Simba.

Mshambuliaji wa Simba, Ateba ni mabao matano amefunga kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Fadlu Davids hajawa na uhakika wan amba kikosi cha kwanza.

Katika mabao hayo alifungua akaunti yake ya mabao kwa kufunga dhidi ya Azam FC mchezo wa ligi uliokamilika kwa ubao kusoma Azam FC 0-2 Simba wakisepa na pointi tatu wakiwa ugenini.

EDGER WILLIAM

Nyota wa Fountain Gate, Edger William ni mabao matano amefunga ndani ya kikosi cha Fountain Gate ambacho kwenye upande wa kufunga ni mabao 24 wamefunga na ukuta umeruhusu mabao 32 ikiwa nit imu namba moja kuruhusu mabao mengi ndani ya ligi.

 

PACOME

Pacome Zouzoua kiungo mshambuliaji wa Yanga yupo kwenye chati za wakali wa kucheka na nyavu ambapo ni mabao matano kafunga akiwa na uzi wa njano na kijani kwa msimu wa 2024/25.

Nyota huyo kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate alifunga mabao mawili na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Pacome amesema kuwa kikubwa ambacho wanahitaji katika mechi za oni kupata matokeo mazuri.

PRINCE DUBE

PRINCE Dube
Prince Dube, Clement Mzize, Khalid Aucho mastaa wa Yanga kwenye moja ya mchezo wa ushindani 2024/25. Source: Yanga.

Prince Dube ingizo jipya ndani ya Yanga, ameanza kuchangamka akiwa anaingia kwenye rekodi ya nyota wa kwanza kufunga hat trick msimu wa 2024/25.

Dube alifunga kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-2 Mashujaa ilikuwa Uwanja wa KMC  Complex.Dube aliandika rekodi hiyo ambayo ilikuwa bado haijandikwa na mastaa wote ndani ya Bongo.

Yanga kwenye mechi tano chini ya Sead safu ya ushambuliaji imeonekana kuwa imara ikitupia mabao 18 na kuruhusu mabao mawili pekee ndani ya ligi.

 

 

Share this: