DubeDube

PRINCE Dube mshambuliaji wa Yanga ameandika rekodi ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 kwa kufungua akaunti ya mabao akiwa na uzi wa Yanga na kusepa na tuzo ya mchezaji bora baada ya kucheza mechi 9 bila kufunga.

Dube ambaye ni mali ya Yanga inayodhaminiwa na SportPesa aliandika rekodi hiyo mbele ya Mashujaa, waliposepa na pointi tatu mazima baada ya dakika 90 kugota mwisho.

Dubee
Dube Prince nyota wa kwanza kufunga hat trick 2024/25. Source: Yanga.

Mabao hayo alifunga dakika ya 7 na dakika ya 21 kipindi cha kwanza Uwanja wa KMC, Complex na bao la tatu alifunga dakika ya 52 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-2 Mashujaa na mabao ya Mashujaa yalifungwa na David Uromi dakika ya 45 na Idrisa Mohamed dakika ya 62.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa ni furaha kwake kufunga ndani ya ligi kwa kuwa alikuwa anapitia kipindi kigumu jambo ambalo lilikuwa linampa presha kubwa.

“Nimefurahi kufunga na ninamshukuru Mungu, ilikuwa ni kipindi kigumu napitia lakini kwa sasa nimefunga nafurahi, nawashukuru mashabiki na wachezaji.Kuhusu kiatu cha ufungaji mimi sifikirii kwa kuwa kuna washambuliaji wengi wazuri na wanafunga.

“Ambacho ninafikiria kwa sasa ni timu kupata ushindi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza nina amini itakuwa hivyo. Ninamshukuru Ally Kamwe yeye alikuwa akinitumia meseji mara kwa mara kunipa moyo kwamba kipindi kigumu kitapita.”

 

REKODI MASTAA WA YANGA DHIDI YA MASHUJAA

Khomeiny alianza langoni ni mabao mawili aliokota akiwa langoni kwenye mchezo huo wa ligi, Yao, Kibwana Shomari ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kwenye ligi msimu wa 2024/25 akitoa pasi yake ya kwanza alimpa Prince Dube dakika ya 52.

Dickson Job beki wa kazi alivaa kitambaa cha unahodha, Bacca alirejea kwenye kikosi baada ya adhabu aliyopata kadi nyekundu ya moja kwa moja mchezo dhidi ya Azam FC.

Khalid Aucho alikuwa na kazi ya kupiga pasi ndefu na kutibua mipango ya Mashujaa, Clemet Mzize alitoa pasi yake ya bao kwa Dube dakika ya 21 akiwa ndani ya 18.

Duke Abuya, Prince Dube alifunga mabao yote matatu kwenye mchezo huo akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo, Aziz Ki, Pacome alitoa pasi moja ya bao.

Wachezaji wa akiba ilikuwa ni Mshery, Kibabage, Nondo, Boka, Sure Boy, Sheikhan, Farid Mussa, Moses, Mudathir Yahya.

NAFASI YA YANGA KWENYE LIGI

Dickson Job
Dickson Job beki wa Yanga kwenye kazi dhidi ya nyota wa Mashujaa 2024/25. Source: Yanga.

Yanga ni mabingwa watetezi wa ligi kwenye msimamo ni nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 12 kibindoni wana pointi 30 namba mbili ni Simba wenye pointi 31 nao wamecheza mechi 12 pia huku vinara wakiwa ni Azam FC, wenye pointi 33.

Ushindi kwenye mechi 10, imepoteza mechi mbili na haijaambulia sare ndani ya ligi. Kwenye kupoteza mchezo wa kwanza ilikuwa dhidi ya Azam FC na mchezo wa pili ilikuwa dhidi ya Tabora United zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.

Katika eneo la utupiaji ni mabao 19 safu ya Yanga imefunga ambapo Prince Dube kiongozi kwenye safu ya ushambuliaji mabao matatu, Clement Mzize na Kennedy Musonda wametupia mabao mawilimawili.

USAJILI KAZI IPO

Wakati huu wa dirisha dogo, Yanga wameweka wazi kuwa watafanya usajili makini kulingana na ripoti ya benchi la ufundi na tayari wameanza kutambulisha wachezaji waliomalizana nao wakianza na Israel Mwenda.

Mwenda alikuwa ndani ya Singida Black Stars ametua Yanga kwa mkopo wenye kipengele cha kuuzwa moja kwa moja ikiwa atafanya kazi kubwa katika kutimiza majukumu yake.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa sio Mwenda peke yake bali kuna wachezaji wengine ambao watatambulishwa ndani ya kikosi hicho kwenye dirisha dogo la usajili hivyo mashabiki wasiwe na mashaka.

Israel P Mwenda
Israel P Mwenda mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga dirisha dogo 2024. Source: Yanga.

“Tunajua kwamba mashabiki wanahitaji kuona kwamba tunawaambia ni mchezaji gani ambaye yupo nan ani ameshasajiliwa hilo lisiwape mashaka kila kitu kipo kwenye mpangilio na taarifa zitawafikia.

“Usajili kwenye dirisha dogo unahitaji umakini mkubwa na ukizingatia kwamba kila mchezaji yupo kwenye timu yake ambacho kinafanyika ni mpango kazi mzuri, wachezaji wapo.”

Share this: