WAKATI joto la mashindano ya SportPesa Shabiki Cup likizidi kuichangamsha mitaa ambapo leo Alhamisi moto unatarajiwa kuwaka kwenye Wilaya ya Babati mkoani Manyara, IMETHIBITISHWA kuwa Mkuu wa Wilaya Babati Mhe. Emmanuela Kaganda Mtatifikolo atakuwepo kuongoza shangwe hilo.

Uwepo na ushiriki wa DC, Emmanuela unadhihirisha mashirikiano chanya ya Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa na Serikali na mchango wa kampuni hii katika ustawi wa Uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kipute cha leo kinatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Majengo CCM – Wazazi, ambapo wadau wa soka na michezo kwa ujumla watapata burudani kali kutoka kwa SportPesa hivyo wakazi wa Wilaya ya Babati na mkoa wa Manyara usipange kukosa.

SPORTPESA SHABIKI CUP NI NINI? NA LENGO KUU NI LIPI?
Ikumbukwe mara baada ya kuwepo matamanio ya muda mrefu ya mashabiki mbalimbali na wadau wengine wa michezo hatimaye Kampuni bora ya ubashiri wa michezo ya SportPesa ilizindua mashindano maalum yaliyopewa jina la ‘SportPesa Shabiki Cup’.
SportPesa Shabiki Cup ni mashindano ya soka yanayoendeshwa na jamii ambayo yameandaliwa na SportPesa, yakiwa na lengo la kuwakutanisha wapenda soka kutoka mikoa mbalimbali kushirikiana na vilabu vinavyodhaminiwa na SportPesa.
Mashindano haya yanalenga kuimarisha uhusiano kati ya jamii na mashabiki wa soka wa maeneo ya karibu kwa kutoa fursa ya kushiriki, kushindana, na kushirikiana.
MUUNDO WA MASHINDANO UTAKUWAJE?
Mashindano hufanyika katika mikoa mbalimbali nchini. ambapo kila eneo, timu mbili zitashindana ambapo:
Timu 1: Timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vilabu vinavyodhaminiwa na SportPesa.
Timu 2: Timu iliyochaguliwa kutoka kwa jamii ya eneo husika.
Washindi wa kila eneo watapokea tuzo zao kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya zawadi.
MBEYA YABEBA HISTORIA YA UZINDUZI

Mashindano haya yalianza kutimua vumbi rasmi jijini Mbeya ambapo yalipata baraka ya kuhudhuriwa na mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Beno Malisa na kushuhudia timu za Yanga Comnbine na Vijana Combine zikivaana kwenye mchezo wa ufunguzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Mwenge, Mbeya na kuishuhudia Yanga Combine ikichomoza na ushindi wa bao 1-0.

VIGEZO VYA USHIRIKI NI VIPI?
Wachezaji lazima wawe na umri wa miaka 18 na kuendelea.
Washiriki lazima wawe raia, au wakazi wa kudumu wa Tanzania.
Kwa Timu 1, wachezaji wote lazima wawe wanachama hai wa tawi linalotambulika.
Kwa Timu 2 (Timu ya Jamii ya Wenyeji), wachezaji wote lazima watoke katika jamii ya eneo linaloandaa tukio.
Usajili
Fomu za usajili zitapatikana kwenye vibanda maalum vya SportPesa katika kila eneo pamoja na ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa. Wachezaji lazima wajisajili mmoja mmoja, wakitoa uthibitisho wa makazi katika jamii husika.
Mchakato wa Uteuzi
Kamati ya uteuzi, ikijumuisha makocha wa soka wa eneo, wawakilishi wa matawi, na maafisa wa SportPesa, watapitia wachezaji wote waliosajiliwa.
Maonyesho ya vipaji yatafanyika kwa siku mbili katika kila eneo, ambapo wachezaji waliosajiliwa wataonyesha ujuzi wao mbele ya kamati ya uteuzi. Kamati ya uteuzi itawapima wachezaji kwa kuzingatia ujuzi wa soka, ushirikiano wa timu, na nidhamu ya michezo.
Kamati itachagua wachezaji 14 (11 wa kuanza na 3 wa akiba) kuunda Timu ya Jamii ya Wenyeji. Uteuzi utatangazwa mwishoni mwa majaribio.
Sheria za mashindano;
Muda wa Mchezo: Kila mchezo utakuwa na vipindi viwili vya dakika 30, na mapumziko ya dakika 10 katikati.
Kuamua Mshindi: Iwapo mchezo utamalizika kwa sare ya 0-0 katika dakika ya 70, mshindi ataamuliwa kwa kupiga mikwaju ya penalti.
Badiliko la Wachezaji: Kila timu itaruhusiwa kufanya mabadiliko matatu kwa kila mechi.
Madhibiti: Mechi zote zitaendeshwa na waamuzi waliothibitishwa na shirika husika.
Hatua za Nidhamu: Sheria za kadi ya njano na nyekundu zitatumika kulingana na kanuni za kawaida za soka. Wachezaji watakaopokea kadi nyekundu watafungiwa kushiriki.
Zawadi

Timu Inayoshinda: Timu itakayoshinda mechi ya mwisho ya mashindano itazawadiwa Kikombe cha SportPesa Shabiki Cup na zawadi ya Fedha kiasi cha TZS 500,000.
Jezi za Timu: Seti kamili ya jezi za mpira kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
Medali: Medali kwa kila mshiriki wa timu.
Timu ya Pili
Zawadi ya Fedha: TZS 250,000, Medali: Medali kwa kila mshiriki wa timu.
Zawadi za Wachezaji Binafsi
Mfungaji Bora: TZS 100,000.
Kipa Bora: TZS 100,000.
Mchezaji Bora (MVP): TZS 100,000.
Sheria za Jumla
Uamuzi wa waamuzi na kamati ya waandaaji ni wa mwisho na lazima uheshimiwe.
Timu lazima zifuate ratiba ya mashindano. Kushindwa kufika kwa wakati wa mchezo kutasababisha kupoteza.
SportPesa inahaki ya kuwaondoa timu au mchezaji yeyote atakayekiuka sheria za mashindano au kuonyesha tabia isiyo ya kimichezo.
Udhamini na Uwekaji Nembo
SportPesa inahifadhi haki zote za kipekee kwa matangazo na shughuli za utangazaji zinazohusiana na mashindano.
Timu zote zinahitajika kuvaa jezi zenye nembo za SportPesa wakati wa mechi.
Vyombo vya Habari na Matangazo
Kwa kushiriki kwenye mashindano, wachezaji na timu wanakubali kuruhusu SportPesa kutumia picha zao, majina, na sura kwa ajili ya matangazo na uendelezaji kwenye majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari.
Mabadiliko
SportPesa inahifadhi haki ya kubadili Masharti na Vigezo hivi wakati wowote washiriki watajulishwa mapema kuhusu mabadiliko yoyote.
Dhima
SportPesa haitahusika kwa majeraha, ajali, au uharibifu wowote utakaotokea wakati wa mashindano na washiriki wanahimizwa kuchukua tahadhari zinazofaa.

