Taifa StarsTaifa Stars

BAADA ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kete yake ya kwanza kutoshana nguvu dhidi ya Ethiopia Uwanja wa Mkapa, Septemba 4 2024 leo tena Septemba 10 2024 itakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu uwanjani kuwania tiketi ya kufuzu AFCON 2025.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo huo Stars ilikuwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Hemed Morocco ambaye aliweka wazi kuwa walikutana na timu bora uwanjani jambo lililowapa ugumu kwenye kupata matokeo ndani ya uwanja.

Bechi la Stars
HEMED Morocco, Juma Mgunda, Kiemba benchi la ufundi la Taifa Stars inayosaka tiketi kufuzu AFCON 2025. Source: Taifa Stars.

“Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa na kila timu ilikuwa inahitaji kupata ushindi na mwisho tukapata pointi moja. Makosa ambayo yamepita tunayafanyia kazi ili kuwa bora kwenye mechi zinazofuata.

“Wapinzani walikuwa bora hivyo kushindwa kutumia nafasi kumetufanya tukose ushindi. Kwa mechi zinazofuata tunaamini tutakuwa bora hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi na kutuombea dua tupate matokeo mazuri.

Kuhusu mchezo wa leo Morocco ameweka wazi kuwa matokeo yaliyopita hayawezi kubadilika hivyo kikubwa ni kuwa tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Guinea wakiwa ugenini.

“Wachezaji wana morali nzuri na kila mchezaji yupo tayari, tulirudi kwenye uwanja wa mazoezi kufanyia kazi makosa yaliyopita hivyo tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Guinea.”

LEO KAZINI DHIDI YA GUINEA

Wachezaji Stars
Wachezaji Stars wakiwa Ivory Coast tayari kuwakabili Guinea mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2025. Source: Taifa Stars.

Septemba 10 timu ya taifa ya Tanzania inatarajiwa kuwa na kibarua kusaka ushindi dhidi ya Guinea ambapo utachezwa Uwanja wa Charles Konani Benny, Ivory Coast kwa wababe hawa wawili kukutana uwanjani kusaka ushindi.

Huu ni mchezo muhimu wa kundi H ambapo utakuwa ni wa pili baada ya ule wa kwanza kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 4 2024 ubao uliposoma Tanzania 0-0 Ethiopia.

Ethiopia kwenye mchezo waliocheza Uwanja wa Mkapa Septemba 9 2024 walishuhudia ubao ukisoma Ethiopia 0-2 Dr Congo ambapo mabao yalifungwa na Bongonda dakika ya 62 na Fiston Mayele dakika ya 76 kwenye mchezo huo ambapo mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga aliweka wazi kuwa ni furaha kwa timu kupata ushindi.

“Tumefurahi kuona timu imepata ushindi na hili lilikuwa jambo kubwa na lenye umuhimu. Wapinzani wetu walikuwa imara lakini tumepata nafasi kwenye mchezo wetu na kuzitumia hivyo ni jambo la furaha kwa taifa kushinda.”

ORODHA YA WACHEZAJI WA STARS

Balua
Balua Edwin yupo kwenye orodha ya wachezaji wa Taifa Stars inayowania AFCON 2025. Source: Taifa Stars.

Bakaari Nondo kutoka Yanga, Nickson Kibabage wa Yanga, Abdulmalick Zakaria wa Mashujaa Adolf Mtasingwa wa Azam FC, Himid Mao wa Talaal El Geish ya Misri, Novatus Dismas wa Goztepe ya Uturuki, Mudathir Yahya wa Yanga, Hussein Semfuko wa Coastal Union Edwin Balua wa Simba, Feisal Salum wa Azam FC, Wazir Junior wa Dodoma Jiji, Cyprian Kachwele wa Vancouver Whitecaps ya Canada, Clement Mzize wa Yanga, Abel Josiah wa TDS TFF Academy.

Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ethiopia kikosi cha kwanza kilikuwa namna hii:-Ally Salim, Lusajo Mwaikenda, Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Himid Mao, Edwin Balua,Novatus Dismas, Feisal Salum, Clement Mzize, Nickson Kibabage.

NAHODHA HUYU HAPA

Himid Mao ameweka wazi kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Guinea ambao ni kuwania AFCON kutokana na kushindwa kupata matokeo kwenye mchezo uliopita jambo ambalo linawapa nguvu ya kupambana ndani ya uwanja kusaka matokeo mazuri.

“Kwenye mchezo uliopita yale yameshapita ambacho tunaangalia kwa sasa kwenye mchezo wetu dhidi ya Guinea tunaamini kwamba hautakuwa mchezo rahisi lakini tupo tayari na tutapambana kufanya vizuri.

“Tunajua furaha yakupata ushindi kwenye mchezo wetu hilo lipo wazi na wachezaji wana ari kubwa. Kila kitu tunaamini kwamba kitakwenda vizuri kwani ambacho tunahitaji ni kupata matokeo mazuri uwanjani hivyo ni mchezo ambao tunautaka.”

Wazir Jr
Wazir Jr nyota wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayowania tiketi kufuzu AFCON 2025. Source: Taifa Stars.

HII HAPA RATIBA YA MECHI ZA LEO

16:00 Botswana v Egypt
16:00 Eswatini v Mali
16:00 Mozambique v Guinea Bissau
16:00 Rwanda v Nigeria
16:00 South Sudan v South Africa
19:00 Gabon v Central Africa
19:00 Guinea v Tanzania
19:00 Liberia v Algeria
19:00 Namibia v Kenya
19:00 Zimbabwe v Cameroon
22:00 Benin v Libya
22:00 Burkina Faso v Malawi
22:00 Cape Verde v Mauritania
22:00 Chad v Ivory Coast
22:00 Zambia v Sierra Leone

Share this: