Aucho v FeiAucho v Fei

KUMECHANGAMKA balaa ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na ushindani ambao umeanza msimu wa 2024/25 huku vinara wakiwa ni Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 huku wakimataifa wakirejea kazini kwenye mechi za ligi.

Ipo wazi kuwa mabingwa watetezi Yanga inayodhaminiwa na SportPesa chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi hawajacheza kwa kuwa walikuwa na mechi za kimataifa kama ilivyokuwa kwa Azam FC iliyogotea nafasi ya pili msimu wa 2023/24.

Wakati wakiwa uwanjani kusaka ushindi wachezaji nawe unaweza kuweka mkeka wako na SportPesa ukavuna mkwanja.

AZAM FC KAZINI

 

Blanco
KUMECHANGAMKA kwa mashabiki wa Azam FC kushuhudia burudani zikirejea ndani ya ligi kutoka kwa wachezaji wao. Source: Azam FC.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwendo wameumaliza Azam FC baada ya kufungashiwa virago na APR ya Rwanda, Jumatano watakuwa uwanjani kusaka pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania ambapo matajiri hao wa Dar watakuwa ugenini.

MABINGWA WATETEZI ALHAMISI

 

Aziz na Mzize
WACHEZAJI wa Yanga wakiwa wamechangamka baada ya kufunga moja ya bao kwenye mchezo wa ushindani. Source: Yanga.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa wakiwa ni mabingwa watetezi kibarua chao kazini itakuwa ni Alhamisi ya Septemba 29 watakuwa ugenini kukabiliana na Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi. Ikumbukwe kwa Kagera Sugar mchezo wa ufunguzi walicheza dhidi ya Singida Black Stars wakapoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba.

REKODI MAPEMA

 

Ahoa
Kiungo mshambuliaji wa Simba Ahoua kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Fountain Gate. Source: Simba.

Jean Ahoua kwa wakali wa kutengeneza pasi za mwisho ni namba moja akiwa ametoa jumla ya pasi tatu ndani ya ligi msimu wa 2024/25. Mchezo aliohusika kwenye mabao mengi ilikuwa dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ambapo alitoa pasi mbili na kufunga bao moja ilikuwa Agosti 25 2024.

Pasi yake ya kwanza kwenye mchezo huo alimpa Edwin Balua ambaye alifunga bao lake la kwanza kwa pigo la kichwa na pasi ya pili alimpa Valentino Mashaka ambaye kwenye mchezo huo alianzia benchi alipoingia akafunga bao lake kwenye mchezo huo.

Ni msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Simba ameanza kwa mwendo mzuri katika kutengeneza nafasi za kufunga na amefunga pia bao moja akiweka wazi kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ndani ya uwanja.

“Kazi kubwa ipo na furaha ni kuona tunapata matokeo mazuri imani yetu ni kuendelea kuwa vizuri zaidi katika mechi zetu zote ambazo tunacheza hilo linawezekana.”

ZIMBWE

 

Zimbwe Jr
Zimbwe Jr nahodha wa Simba kwenye majukumu yake: Source: Simba.

Mohamed Hussein Zimbwe Jr nahodha wa Simba kazi yake inaendelea ndani ya uwanja akiwa ni namba moja kwa mabeki wenye rekodi ya kuwa na pasi nyingi akiwa namba mbili kiujumla.
Zimbwe katoa pasi mbili za mabao na timu ya Simba katika mechi mbili haijaruhusu mabao ya kufungwa ndani ya dakika 180.

MAKAMBO
Nyota wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi cha Tabora United, Heritier Makambo naye ni miongoni mwa nyota waliotoa pasi iliyoleta bao ilikuwa kwenye mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Namungo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.

KAPOMBE/ CAMARA
Nyota wa Simba, Shomari Kapombe ambaye ni beki yeye anaingia kwenye orodha ya nyota waliotoa pasi moja ya bao ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate, Uwanja wa KMC, Mwenge.
Kapombe pasi yake ya kwanza alimpa mwamba Steven Mukwala ambaye alifunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Simba ndani ya ligi. Ukiweka kando Kapombe, Mohamed Camara nyota wa Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani naye ana pasi moja ya bao.

WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU
Mshambuliaji Valentino Mashaka ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba anaingia kwenye orodha ya vinara wa kucheka na nyavu mwanzo kabisa wa msimu wa 2024/25 kwa sasa akiwa katupia mabao mawili.

Mashaka mabao yake yote mawili amefunga akitokea benchi anaingia kwenye rekodi ya super sub ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tabora United na mchezo wa pili kufunga ilikuwa dhidi ya Fountain Gate na mechi zote Simba ilicheza Uwanja wa KMC, Mwenge.

MWENDO WA MOJAMOJA
Mastaa wengi ndani ya ligi kwa sasa wameanza na mwendo wa mojamoja kwenye mechi ambazo walipata kucheza hivyo ni mwanzo mzuri kwao kwa kuwa hatua moja huongeza hatua nyingine mbele.

Miongoni mwa wakali waliotupia bao mojamoja ni Heritier Makambo wa Tabora United, Ahoa wa Simba, Salum Chuku wa Tabora United, Djuma Shaban wa Namungo, Awesu Awesu wa Simba.

Share this: