-----------------------------------------------n-----------------------------------------------n

BAADA ya michezo 50 kupigwa katika mashindano ya EURO 2024 mpaka sasa, hatimaye leo Jumapili mchezo mkubwa wa Fainali unatarajiwa kupigwa kwenye dimba la Olympiastadion.

Kuelekea katika fainali hiyo ambayo inatarajiwa kuikutanisha timu ya Taifa ya England dhidi ya Uhispania, mashabiki 75,000 wanatarajiwa kuushuhudia mubashara ‘live’ mchezo huo.

Nawe unaweza kuwa mshindi wa mamilioni kwa kuweka ubashiri wako wa mchezo huu kupitia Kampuni ya michezo ya Kubashiri ya SportPesa sasa, tembelea tovuti yao ya www.sportpesa.co.tz

EURO
Lamine Yamal

Timu ya Taifa ya Uhispania imefanikiwa kutinga hatua hiyo mara baada ya kuwaondosha Ufaransa katika mchezo wa Nusu Fainali ambao ulishuhudiwa ukimalizika kwa Uhispania kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Ni kinda wa timu ya Taifa ya Uhispania na klabu ya Barcelona, Lamine Yamal mwenye asili ya Afrika ambaye amekuwa gumzo kubwa duniani kufuatia kuonyesha kiwango cha juu katika mashindano hayo ikiwemo kufunga bao kali kutokea nje ya 18 dhidi ya Ufaransa kwenye mchezo huo wa Nusu Fainali na kuisaidia timu ya Taifa ya Uhispania kutinga fainali ya Euro 2024.

Kiwango bora ambacho kimeonyeshwa na Lamine katika michuano kimewafanya, Barcelona kuingia hofu ya kumpoteza staa huyo kiasi cha kuweka kifungu cha kuhitaji  kiasi cha Euro 868 milion kwa timu yoyote itakayomtaka staa huyo, wakati huu akitazamiwa kurithi mikoba ya Lionel Messi.

Yamal ambaye alizaliwa nchini Uhispania mwaka 2007 kwa wazazi wenye asili ya Afrika, ambapo baba yake ana asili ya Morocco huku mama yake akiwa na asili ya Equatorial Guinea.

Staa huyo pamoja na kinda mwenzake, Nico William ambaye pia ana asili ya Afrika kutokea Ghana kwa sasa wanatajwa kuwa ‘Combination’ bora zaidi na wanatabiriwa kuwapa wakati mgumu England leo.

ALICHOSEMA KOCHA WA UHISPANIA

Kuelekea mchezo huo wa fainali kocha mkuu wa Uhispania, Luis de la Fuente Castillo amenukuliwa akisema: “Tunao miongoni mwa wachezaji bora zaidi kwenye kikosi chetu ambao sote tunapaswa kufurahia uwepo wao na kuwalinda kwa ajili ya manufaa ya baadae.

“Tunatarajia mchezo mgumu kutoka miongoni mwa timu bora kwa sasa, lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda ubingwa huu.

“Kuhusu Yamal na Nico tuna bahati kuwa nao, ni vijana wadogo lakini wanacheza kama wazoefu na wana vipaji vikubwa, lakini suala la fainali ni la timu na tumejiandaa kama timu.”

 

EURO KWA ENGLAND NI ‘IT’S COMING HOME’

EURO
Bellingham na Kane

England ambao ni wanafainali wenza wa Uhispania leo, wamefanikiwa kuandika rekodi ya kufika fainali kwa mara ya 2 mfululizo tena katika mashindano makubwa.

Timu hiyo ilifanikiwa kutinga fainali usiku wa kuamkia Alhamisi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uholanzi katika mchezo wa Nusu Fainali ya pili ya mashindano ya Euro 2024.

England ya kocha, Gareth Southgate ililazimika kufanya kazi ya ziada katika mchezo huo kusawazisha bao la kuongozwa ambalo lilifungwa na staa wa Uholanzi, Xavi Simons dakika za awali za mchezo huo.

Straika na nahodha wa England, Harry Kane aliisawazishia timu hiyo kwa mkwaju wa penalti, kabla ya straika, Ollie Watkins kuipatia England bao la ushindi dakika ya mwisho ya mchezo zikiwa ni dakika 9 tu, tangu alipotokea benchi.

 

FAINALI EURO 2024 BERLIN

Fainali ya leo inatarajiwa kupigwa jijini Berlin ambapo inaelezwa viwanja vya ndege vimeripoti ingizo kubwa la wageni waliojipanga kushuhudia tukio hilo.

England wataingia katika fainali hiyo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza fainali ya kampeni iliyopita ya Euro mbele ya timu ya Taifa ya Italy katika mchezo wa fainali uliopigwa katika ardhi yao ya nyumbani kwenye Uwanja wa Wembley.

KANE, BELLINGHAM KUIBEBA ENGLAND

Nahodha wa England, Kane na kiungo wa Real Madrid, Jude ndio wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa ya kui8beba England leo kutokana na kiwango bora walichoonyesha katika mashindano hayo.

 

ALICHOSEMA KOCHA WA ENGLAND

EURO
Southgate

Licha ya kukosolewa sana kufuatia mwanzo wa kusuasua wa England katika michuano ya Euro 2024, Southgate ana nafasi nyingine ya kuandika historian a England ambapo amesema: “Sababu pekee nilikubali nafasi ya kuongoza timu hii ni kwa sababu nimetamani kuhakikisha naleta mafanikio ya soka kwenye nchi hii. Najivunia kuongoza timu hii kufika fainali ya mashindano haya ya EURO 2024 tena mbali na ardhi ya nyumbani.

“Tunajua haitakuwa kazi rahisi lakini tupo tayari kupambana kwenye fainali na kushinda ubingwa.”

 

VIKOSI TARAJIWA VITAKAVYOANZA LEO

England

Pickford; Walker, Stones, Guéhi; Saka, Mainoo, Rice, Trippier; Foden, Bellingham na Kane.

Spain

Unai Simon; Carvajal, Le Normand, Laporte, Cucurella; Rodri, Fabian, Dani Olmo; Lamine Yamal, Morata na Nico Williams.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.