InongaInonga

 

JOHN Bocco
NAHODHA wa Simba 2023/24 John Bocco ambaye amekutana na Thank You. Source: Simba.

SIMBA mpya inasukwa ikiwa ni mwanzo wa maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 baada ya kuanza kuwaaga rasmi wachezaji ambao hawatakuwa kwenye kikosi hicho msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ipo wazi kwamba ndani ya 2023/24 mwendo wa Simba haukuwa kwenye kiwango bora. Hiyo ilipelekea kuporomoka kutoka nafasi ya pili ilipokuwa kwa msimu wa 2022/23 na kugota mpaka nafasi ya pili msimu wa 2023/24.

HAWA WALIANZA KUPEWA ASANTE

Jean Baleke
Jean Baleke mshambuliaji aliyekutana na Thank You ndani ya Simba akiwa na mabao 8 msimu wa 2023/24. Source: Simba.

Kwenye dirisha dogo ni mastaa wawili walishtua kutokana na kupewa mkono wa asante ndani ya Simba licha ya kuwa kwenye ubora wao ikiwa ni pamoja na Jean Baleke. Ikumbukwe kwamba Baleke alifunga jumla ya mabao 8 msimu wa 2023/24 kwenye ligi alisepa akiwa anaongoza kwa mastaa waliokuwa na mabao mengi.

Mrithi wa mikoba ya Beleke ambaye msimu wa 2022/23 alifunga mabao 8 kwenye ligi hivyo kusepa akiwa kafunga jumla ya mabao 16 alikuwa anatajwa kuwa ni Michael Fred ambaye kamaliza msimu akiwa katupia mabao 6.

Hajafanikiwa kuvunja rekodi ya Baleke kwa kuwa kwenye mechi za mwisho hakupata nafasi kutokana na kupata maumivu kwenye moja ya mchezo wa ligi. Nyota huyo anatajwa kuwa kwenye orodha ya nyota wanaofanyiwa tathimini kama waondoke ama wakabiki ndani ya Simba.

MOSES PHIRI

Nyota Phiri yeye ni winga mshambuliaji maumivu ya mguu aliyopata msimu wa 2022/23 kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba yalimfanya azidi kurejea kwenye ubora taratibu na hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2023/24.

Alikutana na Thank You kwenye dirisha dogo mbadala wake alikuwa anatajwa kuwa Pa Omary Jobe ambaye alishindwa kuonyesha ubora wake kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi.

Pa Jobe anatajwa kuwa atakuwa miongoni mwa nyota ambao hawatakuwa ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu mpya wa 2024/25. Ikumbukwe kwamba kwa sasa Mohamed Dewji, Mo amerejea kwenye nafasi yake na amebainisha kwamba mpango mkubwa ni kuirejesha Simba kwenye ubora.

BOCCO IMEISHA SIMBA

John Bocco mshambuliaji bora wa muda wote amekuwa nyota wa kwanza kupewa mkono wa asante ndani ya Simba kuelekea msimu mpya baada ya dirisha la usajili kufunguliwa kuelekea msimu wa 2024/25.

Ikumbukwe kwamba Mei 28 2024 kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Bocco alitupia video akiwa na uzi wa Simba kisha akaachia ujumbe uliosomeka, First & Last, Thank You Lion. Bocco rasmi ameagwa ndani ya Simba Juni 17 2024.

Anashikilia rekodi ya kuwa nyota ambaye kafunga zaidi ya mabao 100 ndani ya Simba. Aliibuka Simba akitokea kikosi cha Azam FC ambapo nyota wengine aliotambulishwa nao akitokea Azam FC ni Aishi Manula, Shomari Kapombe ambao bado wapo Simba huku Erasto Nyoni yeye kwa sasa yupo ndani ya Namungo.

NTIBANZOKIZA NA SIMBA

Saido
Saido Ntibanzokiza kinara wa utupiaji ndani ya Simba 2023/24 mabao 11. Source: simba.

Mwingine ambaye anatajwa kuwa hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba ni Saido Ntibanzokiza ambaye ni mkali wa mapigo huru ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24. Huyu inatajwa kuwa ameomba kusepa ndani ya kikosi hicho akapate changamoto mpya kwenye timu nyingine.

Yeye ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu kwenye ligi ndani ya Simba. Ni mabao 11 kafunga akiwa ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu Simba iliyofunga mabao 59 baada ya kucheza mechi 30. Nyota huyo kafunga mabao 7 kwa penalti akiwa ni mchezaji namba moja kufunga mabao mengi kwa penalti ndani ya ligi.

Ikumbukwe kwamba Simba imegota nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 69. Msimu wa 2024/25 itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika itaungana na Coastal Union ya Tanga iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya nne.

Kwa msimu wa 2022/23 Simba iligotea nafasi ya pili na ilishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. Imekuwa tofauti kwa msimu wa 2023/24 ikigotea nafasi ya tatu na ile ya pili kuwa mikononi mwa Azam FC itakayopeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

HENOCK INONGA

Henock Inonga beki wa kazi ngumu ndani ya Simba naye anatajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao watasepa ndani ya kikosi cha Simba. Ni mechi 10 alicheza ndani ya kikosi hicho kwenye mechi za ligi kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Taarifa zinaeleza kuwa amepata ofa kutoka timu moja ya Morocco hivyo atauzwa kwa kuwa mkataba wake na Simba unatarajiwa kugota mwisho 2025.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally hivi karibuni alibainisha kwamba watafanya kazi kubwa kuboresha kikosi cha Simba kurejea kwenye ubora wake.

“Kuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya maboresho ya kikosi. Wapo wachezaji ambao wataondoka kutokana na mikataba yao kuisha na wapo ambao wapo kwenye mazungumzo na uongozi ili kuongeza mikataba yao hivyo mashabiki wasiwe na hofu ni muda wa kuwa pamoja zaidi.”

 

Share this: