https://sportpesa.co.tz/YANGA
Kariakoo Dabi

MOTO utawaka kwa dakika 90 leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambapo Yanga wanaobebwa na udhamini mnono wa Kampuni ya michezo ya SportPesa wanatarajia kushuka Uwanjani kuikaribisha Simba katika mchezo mkubwa wa Dabi ya Kariakoo.

KUMBUKUMBU YA SIMBA 1-5

https://blog.sportpesa.co.tz/https://sportpesa.co.tz/YANGA
Matokeo ya mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 5, 2023

Mchezo huu ni wa Mzunguko wa pili kwa timu hizo mbili ambapo kila timu itaingia na kumbukumbu ya tofauti kutokana na mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulipigwa Novemba 5, mwaka jana na kuishuhudia Simba ikikubali kipigo cha aibu cha mabao 5-1.

Kipigo hicho kilipelekea mpasuko mkubwa kwa Simba ambao ndio walikuwa wenyeji wa mchezo kiasi cha kuigharimu ajira ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mbrazili, Robert Olivieira ambaye alifutwa kazi kufuatia matokeo hayo.

WABABE WA KUCHANA NYAVU NOVEMBA 5, 2023

Kweye mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao ulipigwa Novemba 5, mwaka jana ni Wanaume watano ambao walitupia kambani kwenye mchezo huo ambao ni;

Maxi Nzengeli

Alienda kambani mabao mawili na kuwa nyota pekee ambaye alifunga mabao mengi zaidi katika mchezo huo, huku mpaka sasa akiwa tayari amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 9 kwenye ligi.

 

Kennedy Musonda

Straika wa kimataifa wa Zambia ambaye alifunga bao la kwanza tena katika dakika ya tatu tu ya mchezo akiunganisha kwa kichwa krosi ya, Yao Kouassi Attohoula.

Aziz KI

Ndiye kinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa akiwa amefunga mabao 14, ambapo katika mchezo huo alifanikiwa kufunga bao moja.

Zouzoua Pacome

Akicheza mchezo huo kwa mara ya kwanza, Pacome alipachika bao moja kwa mkwaju wa penalty akihitimisha  karamu hiyo ya mabao matano.

Kibu Dennis

Nyota pekee wa Simba ambaye alifunga bao na kuonyesha mchezo bora kabla ya kuumia na kutolewa.

MAKOCHA YANGA, SIMBA WANASEMAJE KUELEKEA MCHEZO WA LEO?

https://sportpesa.co.tz
Kocha Seleman Matola

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola akizungumzia mchezo wa leo amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani zao wa Jadi utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Matola amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali zipo juu na wataingia kwenye mchezo huo kwa lengo la kupambana na kupata pointi tatu.

Matola ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao kwa sasa, lakini wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanawakabili.

Matola ameongeza kuwa kuhusu ubingwa bado wapo kwenye mbio za kupigania na hawawezi kukata tamaa mpaka mwisho.

“Kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo, hii ni Dabi na mara zote haijawahi kuwa rahisi. Yanga ni timu bora na kila mtu anajua lakini tupo tayari kuwakabili.

“Tunafahamu mara ya mwisho tulipokutana hatukuwa bora lakini mechi ya leo ni mpya, na kuna dakika 90 nyingine kabisa na hatutafanya makosa ambayo yataweza kutugharimu,” amesema Matola.

KAPOMBE AAHIDI FURAHA SIMBA

Kwa upande wake mlinzi wa kulia wa timu hiyo, Shomari Kapombe amesema wao kama wachezaji wapo tayari kupambana ili kuwapa furaha mashabiki.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tutahakikisha tupambana kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Kapombe.

YANGA WANASEMAJE?

YANGA
Kocha Mkuu Yanga, Miguel Gamondi

Kwa upande wa kocha wa Yanga Muargentina, Miguel Gamondi amesema: “Mchezo wa leo ni mchezo mgumu na tunajua wanataka kuja kucheza ili washinde mechi na kulipa kisasi, lakini tumejiandaa kwa hilo sisi tuna timu imara ambayo inaweza kucheza kwenye presha ya aina yoyote.

“Kama wanadhani wakija na presha ya kulipa kisasi inaweza kuwasaidia, basi linaweza pia kuwa kosa. Mashabiki wetu wamekuwa nyuma yetu wakati wote, hata dakika ambazo hatuchezi vizuri Uwanjani wamekuwa wakiendelea kushangilia kwa nguvu na kutupa nguvu.

“Nina amini leo kutakuwa na namba kubwa ya mashabiki wetu Uwanjani na tumejiandaa kwa mchezo mzuri.”

JOB ATANGAZA WANAZITAKA POINTI 3

Kwa niaba ya wachezaji wa Yanga nahodha wao, Dickson Job amesema: “Simba SC ni timu nzuri, nasi tuna timu nzuri, bila shaka utakuwa mchezo mzuri wenye ushindani hivyo tumejiandaa vyema sana kuhakikisha tunaondoka na alama tatu muhimu.

“Mchezo wa leo utakuwa mgumu, haijalishi watu wanatupa nafasi kubwa ya kushinda. Sisi hatusikilizi maneno ya watu bali tunazingatia maelekezo ya mwalimu. Hatuendi kutafuta idadi fulani ya magoli tunakwenda kutafuta alama tatu.”

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.