Sopu AzamSopu --
  • LIGI Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili ni kivumbi kwa timu kusaka pointi tatu uwanjani
  • Yanga, Simba, Azam FC kwenye shughuli nzito kwelikweli kwa wapinzani wao
  • Homa ya Mzizima Dabi yaanza mapema kabla ya kazi yenyewe

RATIBA ya Ligi Kuu Bara Machi ni ngumu kwa kila timu kutokana na kila mpinzani kutazama kwa umakini mchezo unaomuhusu mpango mkubwa ikiwa ni kupata ushindi kwenye mechi husika ambazo zina ushindani mwanzo mwisho ndani ya dakika 90.

Ipo wazi kwamba mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya SportPesa inaongoza ligi chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye ameweka wazi kuwa anapenda kushuhudia burudani uwanjani kwenye kutafuta pointi tatu muhimu.

Kwenye mchezo wao uliopita mzunguko wa pili Yanga ilikuwa Uwanja wa Azam Complex na iliambulia pointi tatu kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ihefu walipolipa kisasi kwa kuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Machi inaendelea kwa timu kushuka uwanjani kusaka ushindi ambapo wachezaji wanapambania kombe kwenye majukumu yao jambo ambalo linaongeza ushindani katika mechi za ligi.

Gamond mpya
KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi 18 kikipata ushindi mechi 16, sare ni sawa na kupoteza mechi mojamoja. Source: Yanga

RATIBA INAWAPA KAZI HAWA

Machi 14 kuna mechi za ligi ambazo zinatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kuwa katika kazi ya kusaka pointi tatu ndani ya uwanja ili kufikia malengo yao  huku ratiba ikiwa kazi ya kufanya.

Vinara wa ligi Yanga wakiwa na pointi 49 watakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi itakuwa dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Azam Complex, saa 2:15 usiku.

Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Denis Kitambi imekusanya pointi 21 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 20 ikiwa imebakiwa na mechi 10 kukamilisha mzunguko wa pili.

Kitambi amebainisha kwamba wanatambua uimara wa Yanga ulipo wanahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo kutokana na kutokuwa na mwendo mzuri kwenye mechi ambazo wamecheza.

Aidha kocha huyo amesema wanatambua namna uimara wa Yanga ulipo kutokana na kuwa na matokeo mazuri kwenye mechi zao ambazo wanacheza uwanjani jambo linalowafanya wawe tayari.

“Yanga ni timu imara inawachezaji wazuri na kazi kubwa ni kuona namna gani tutapata pointi kwenye mchezo wetu, kikubwa ni kuona kwamba baada ya dakika 90 tunapata pointi tatu muhimu.

“Wachezaji wapo tayari kutokana na maandalizi ambayo tumefanya tunaamini kwamba tunakwenda kucheza na timu nzuri tunawaheshimu wapinzani wetu hivyo tutaingia kwa tahahadhari kupata pointi tatu,”.

MKWAKWANI KUNA KAZI

Tanga pale Uwanja wa Mkwakwani kutakuwa na kazi pia ambapo kuna mchezo wa ligi kwa dakika 90 za wachezaji kuvuja jasho kutafuta ushindi.

Ni Coastal Union iliyotoka kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Simba kwa kuruhusu mabao 2-1 wao watakuwa wanasaka pointi tatu dhidi ya  Ihefu ambao nao wanazihitaji pia pointi hizo tatu.

Ihefu mchezo wake uliopita ilikuwa Uwanja wa Azam Complex na ilishuhudia ubao ukisoma Yanga 5-0 Ihefu waliacha pointi tatu Dar na Machi 14 watakuwa Tanga, Uwanja wa Mkwakwani kusaka ushindi.

SIMBA KWENYE KAZI NYINGINE

Baada ya kumalizana na Singida Fountain Gate kwenye mchezo wao uliopita na sasa watakuwa na kazi nyingine Simba kusaka pointi tatu wakiwa nyumbani huku wapinzani wao nao pia hesabu zao ni kuzipata pointi hizo tatu.

Machi 15 itakuwa ni Simba SC dhidi ya Mashujaa mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex kwa wababe hao kuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

 

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa 0-1 Simba ikiwa pointi tatu mali ya Simba na sasa itakuwa ni kisasi kwa Mashujaa huku Simba wakihitaji kulinda ushindi wao.

WAKULIMA WA ALIZETI KAZINI

Wakulima wa alizeti, Singida Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Simba kwa kufungwa mabao 3-1 sasa watakuwa nyumbani Mwanza kwenye msako wa pointi.

Mchezo wao itakuwa ni Machi 16 ni dhidi ya Namungo Uwanja wa CCM Kirumba ambapo yapo maskani ya Singida Fountain Gate inayofundishwa na Jamhuri Kiwelu (Julio) ambaye amepewa agenda 10.

MZIZIMA DABI HII HAPA

Mzizima Dabi ipo njiani ndani ya Machi ikiwa ni mzunguko wa pili kwa wababe hawa wawili kukutana Uwanja wa Mkapa ndani ya dakika 90.

Kazi ni ngumu kwa kila mm

HABIB Kyombo na Kazad wachezaji wa Singida Fountain Gate wakiwa uwanja wa mazoezi kwa maandalizi ya mechi za ushindani. Source: Singida Fountain Gate
Habib Singida

oja kupiga hesabu za kukomba pointi tatu ambapo kwenye mzunguko wa kwanza Azam FC ilipoteza pointi tatu mazima.

Machi 17 Jumapili inatarajiwa kuwa ni Azam FC dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa saa 2:15 usiku.

Kubet mechi hii bofya hapa:

 

Share this: