SportPesa
  • KUPITIA  SUPA JACKPOT YA SPORTPESA  WATEJA WA M-PESA KWA SHILINGI ELFU MOJA.

 Kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri Tanzania, SportPesa, imeungana na Vodacom kuleta bidhaa mpya ya Supa Jackpot kwa kutumia M-Pesa USSD. Huduma hii ya SupaJackpot inamuwezesha mteja wa Vodacom kupitia M-Pesa kuweka ubashiri wa mechi za mpira wa miguu na kujishindia hadi zaidi ya Bilioni 1.

Ushirikiano kati ya SportPesa na M-Pesa kupitia Supa Jackpot unalenga kuwapa wateja nafasi ya kujishindia Jackpot na kubadili maisha yao, kuburudika huku wakifatilia mechi za mpira wa miguu na kubashiri michezo waipendayo kila wiki.

Kupitia Supa Jackpot mchezaji anaweza kujishindia bonasi endapo atabashiri kwa usahihi mechi kuanzia 12-16 kwenye Jackpot iliyopo kwenye menyu ya M-Pesa. Endapo mchezaji atabashiri mechi zote 17 kwa usahihi basi ataondoka na Jackpot ya wiki hiyo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.

SportPesa

Sabrina Msuya, Mkuu wa Idara wa Uhusiano na Mawasiliano, SportPesa ameelezea juu ya ushirikiano huo kwa kusema, “Tunayo furaha kuungana na Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa kuleta bidhaa hii ya kipekee kwa wateja wa M-Pesa. Supa Jackpot ni moja kati ya huduma mpya tuliyoiongeza ili kuwa karibu zaidi na watumiaji wa mtandao wa Vodacom.”

“Kila wiki tutakuwa tukitangaza washindi wa bonasi na tunamatumaini makubwa kupata mshindi wa bilioni moja kutoka Vodacom.”

Amina Said, Meneja wa Wateja wakubwa wa M-Pesa, amesisitiza namna ya kuwawezesha wateja wa M-Pesa kupitia teknolojia ya mtandao ya simu namna ya kushiriki kwenye Supa Jackpot kupitia M-Pesa na kuweza kujishindia bonasi mbalimbali na hata kuibuka washindi wa Supa Jackpot. Lengo kuu la ushirikiano wetu na SportPesa kupitia huduma mpya kabisa ya Supa Jackpot kuunda mazingira yenye usawa ili watumiaji wa M-Pesa waweze kunufaika na fursa hii kwa kushindia zawadi kubwa na kujivunia mtandao wa Vodacom.

SportPesa

“Kucheza Supa Jackpot, mteja wa Vodacom kupitia M-Pesa anatakiwa kupiga *150*00#, kisha bonyeza 4 kwa malipo ya M-Pesa, ikifuatiwa na namba 8 : Michezo ya Kubahatisha, kisha bonyeza 7 kuchagua Supa Jackpot,na kuanza kuweka ubashiri wa mechi 17 zilizopangwa.”

*Kwa wateja wapya wanapaswa kuanza kwa kujisajili na kuanza kucheza moja kwa moja kuanzia kiwango cha shilingi 1000.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wateja wetu wote wa M-Pesa wanaoendelea kutumia huduma zetu za M-Pesa na waendelee kufurahia mchezo huu mpya ya Supa Jackpot ambayo ipo wazi kwa yeyote mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea”

Kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom wanaweza kuwasiliana na timu yetu ya huduma kwa wateja kwa kupiga 0764115588 ili kupata msaada na maelekezo zaidi.

 

 

Share this: