Diatus Ishengoma ni mmoja wa watanzania wenye bahati, ambae amefanikiwa kujishindia shilingi 15,000,000 katika Kampeni ya Maokoto Deilee ya SportPesa na Tigo pesa, Kampeni hii ilizinduliwa mnamo tarehe 21mwezi wa nane mapema mwaka huu., ambapo washindi 571 wameweza kuzawadiwa zawadi tofauti tofauti zikiwemo simu janja na fedha taslimu.
Akizungumza kutoka kempu ya yanga Avic Town, Diatus alisema yeye alianza kucheza na SportPesa kuanzia mwaka 2017 wakati yuko chuo

Kipindi hicho Rafiki yangu alikuwa akijua kuwa Kampuni ya SportPesa imetokea kenya.” Anasema Diatus.
Anaendelea kwa kusema tangu ameanza kucheza na SportPesa amewahi kushinda kuanzia hela ndogo ndogo100,000, 30,000, 50,000 na viwango vingine vya kawaida ambavyo alikuwa anashinda kupitia mechi za multibet.
’Najiona ni mtu mwenye bahati kidogo, naweza kusema Mungu ni mwema kwa kuwa tangu nimeanza kucheza au kujua kubashiri nimekuwa napata japo kidogo.
Diatus anasema yeye anapenda sana kubet na huwa anabeti anafurahia jinsi anaweka mikeka, kusubiria kuangalia kama amepata au amekosa, kwa sababu huwa inampa hamasa kubwa hasa kwa sababu yeye mshabiki mkubwa wa mpira.
“Mimi napendelea sana kuweka over and under inanipa mimi nafasi ya kuwa na uhakika wa kuongeza ushindi zaidi, kwasababu matokeo makubwa zaidi.”
Anaelezea kuwa kampuni ziko nyingi za kubeti , lakini yeye anaangalia urahisi katika kufanya miamala, kama kutoa pesa kutoka Tigo pesa kwenda kwenye akaunti yake ya SportPesa, na pia hata ukishinda kutoa miamala kutoka kwenye akaunti ya SportPesa ni rahisi sana.
Aliongeza kuwa Jackpot za SportPesa ni kubwa sana na zinavutia na zinashawishi mtu kuweka hela na kubeti, pia application ya SportPesa inakupa machaguo mengi kuweka bashiri zako.
Anaelezea kwa kusema siku ambayo alipigiwa simu kwamba yeye ndio mshindi wa shilingi 15,000,000 wa promosheni ya Maokoto Deilee alikuwa kwenye shughuli zake. Hakuamini kwa sababu alikuwa anahisi ni utapeli.
“Niliwasiliana nao wakaniambia kweli nimeshinda na wakaniomba nitume vitambulisho vyangu, hapo ndipo niliamini kweli nimeshinda”
Anasema kiasi alichokipata ni kikubwa na bado hajapanga bado anapanga kufanya kwa sasa,hivyo anahitaji muda aweze kufikiria ni kitu gani atafanya, kama ni biashara au kumpa mke wake mtaji wa kufanya biashara.
Ningependa kuwashukuru sana SpotPesa kwa mapokezi yao mazuri sana, na pia nimefurahi sana kupata nafasi ya kutembelea ofisi za SportPesa, bila kusahau nimepata nafasi ya kutembelea Avic Town ambapo timu yangu ya The Young African SC wanafanya mazoezi na kupata nafasi ya kuwaona wachezaji.
Anamalizia kwa kuwaasa watanzania kuiamini na kucheza na SportPesa kwani hata yeye mwenyewe hakuwa anaamini mara ya kwanza alipoanza kucheza.
‘’Sina maneno mengi ya kusema zaidi ya kuwaomba watanzania kucheza na SportPesa hasa hasa Jackpot ya kati kati ya wiki na ile ya mwisho wa wiki, kwani bonus zao ni za viwango vya juu sana.

