Wachezaji wa Iceland U19Iceland-U

Leo Tarehe 4 ya Mwezi Julai 2023, katika dimba la MFA Centenary Stadium Malta, utapigwa mchezo wa kombel la Ulaya kwa vijana, yaani UEFA Euro U19 2023, baina ya timu za vijana ya Iceland U 19 dhidi ya timu ya vijana ya Spain U19.

Timu zote mbili zinakutana katika mechi hii ya kwanza ya kundi B baada ya kufanya vizuri katika hatua ya kufuzu ambapo Iceland U19 pamoja Spain U 19 wapo kundi moja na timu za Greece U19 na Norway U 19.

Takwimu zilizopo zinaonyesha timu hizi mbili hazijawahi kukutana katika mechi ya aina yoyote hivyo mechi hii itakuwa ya kwanza baina yao. Kwa Takwimu zilizopo timu ya U 19 ya Iceland imeshacheza mechi 10, tangu kuundwa kwake.

Timu hii imecheza mechi hizi zaidi katika mashindano au michuano ya aina mbili tu. aina ya kwanza ya michuano ni mashindano ya kufuzu Ulaya (European Championship Qualification) na mechi za kirafiki.

Mechi ambazo tayari Iceland U19 ameshacheza na matokeo yake ni pamoja na Iceland U19 dhidi ya Hungary U19 mchezo uliopigwa Tarehe 28 March 2023, ambapo timu ya Iceland U19 ilishinda magoli mawili kwa bila yakifungwa na Orri Steinn Oskarsson dakika ya 67 na Hilmir Mikaelsson, goli lililofungwa katika dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kuisha.

Mechi nyingine ni mechi dhidi ya England U19. Mechi hii ilipigwa Tarehe 25 na timu ya Iceland U19 ilishinda kwa goli moja kwa nunge. Goli hilo lilifungwa dakika ya 50 na mchezaji yule yule machachari Orri Steinn Oskansson ambaye anakipiga katika timu ya FC Kobenhavn ya Denmark.

Timu hii ya Iceland U19 ilicheza mechi nyingine mnamo Tarehe 22 Mwezi Machi 2023 dhidi ya timu ya vija ya Uturuki na matokeo yalikuwa sare ya magoli mawili mawili. Mchezaji Orri Steinn Oskarsson alifungua pazia la magoli dakika ya 34, akifuatiwa na mchezaji wa Turkey U19 Ilker Akar aliyefunga goli moja kabla ya mchezaji Kristian Hlynsson kufunga goli la kusawazisha katika dakika za nyongeza.

Mechi iliyofuata Iceland U19 walicheza na Kazakhstan U19 na kufanikiwa kushinda kwa jumla ya magoli 4 kwa moja. Alikuwa ni mchezaji Orri stein Oskarsson aliyengára vilivyo katika mchezo huo baada ya kufunga magoli mawili kisha wachezaji wengine wawili wa Iceland U19 Hilmir Mikaelsson na Adolf Daoi Birgisson wakihitimisha msiba kwa Kazakhstan kwa kufunga goli moja moja, huku mchezaji wa Uturuki U19 Saif Popov akifunga goli moja la kufutia machozi.

Mchezo mgumu kuliko yote ambao timu ya Iceland U19 imekutana nao ni dhidi ya timu ya France U19. Huu ndio mchezo pekee waliofungwa magoli mawili bila majibu. Mchezaji Marvin De Lima alifunga goli la mapema katika dakika ya tisa, kabla ya winga wa kulia Yoan Kore ajaongeza goli la pili kwa Ufaransa dakika ya 68.

Mechi ya mwisho katika mechi ambazo Iceland U19 imecheza ni mechi dhidi ya Scotland. Mechi hii Iceland U19 alishinda kwa goli moja lililofungwa na mchezaji Orri Steinn Oskarsson katika dakika ya 70.

 

Wachezaji wa Spain U19Kwa ufupi katika takwimu hizi ambazo nimeziweka hapa za Iceland U19 timu hii, nimeweka matokeo ya mechi sita alizocheza ambapo kati ya hizo timu hii imeshinda mechi nne kutoa sare moja na kufungwa moja.

Kwa upande wa Spain U19 wao takwimu zao katika mechi 6 za karibuni walicheza dhidi ya Ukraine U19, Tarehe 28 Machi 2023 na kufanikiwa kuwashindilia magoli manne yaliyofungwa na Cesar Palacios goli lililofungwa dakika 3, Angel Galiot (3), Dani Rodriguez dakika ya 22 na mchezaji Victor Barbera alifunga goli la mwisho dakika 59.

Mechi iliyofuata kwa Spain U19 ilikuwa dhidi ya Luxembourg ambapo Spain U19 ilishinda kwa magoli manne kwa bila. Baada ya mechi hiyo timu hii ya Spain U19 ilicheza na Denmark U19 na matokeo yalikuwa 0-0.

Mechi ya nne ilikuwa dhidi ya Norway U19, ambapo Spain U19 waliwachapa Norway U19 kwa magoli matatu kwa bila. Mechi ya tano walicheza ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Mauritania na kushinda magoli manne kwa bila.

Baada ya kuangalia takwimu za timu zote mbili utagundua mechi hii itakuwa ya ushindani kutikana na aina ya matokeo ambayo yameonekana kupatikana kwa timu zote mbili na pia aina ya wapinzani, kwa maana ya timu walizocheza nazo.

Wachezaji wa kuchungwa kwa upande wa Iceland U19, mchezaji Orri Stann Oskarsson na mwenzake Hilmir Mikaelsson wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga hivyo itabidi wapewe ulinzi wa kutosha.

Kwa upande wa Spain U19 mchezaji wa kuchungwa zaidi ni kiungo anayecheza katika timu ya Barcelona Aleix Garrido. Huyu ni kiungo mnyumbulifu ambaye anafananishwa na mchezaji mwingine wa Barcelona Pedri, almaarufu kama Pedro Gonzalez.  Mchezaji mwingine wa kuchungwa ni Pedro Gonzalenz Lopez.

Mechi hii tayari ipo katika tovuti ya Sportpesa. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

Share this: