Gabon-UGabon-U

Leo Jumamosi ya Tarehe 1- Julai 2023, pale katika Uwanja wa Grand Stade De Tanger utapigwa mchezo wa pili wa kundi B, wa kombe la Africa Nations Cup U-23 , baina ya timu ya taifa ya Vijana ya Gabon U23 dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Egypt U23, ikiwa ni mchezo wa pili wa kundi hilo.

Vijana hawa wa Gabon U 23 ambao wanajulikana zaidi kama the Young Lion walianza michezo hii kampeni hii ya mashindano ya Africa U-23 Cup Nations kwa vijana chini ya miaka 23, kwa kucheza dhidi ya Mali U23 na kuchapwa jumla ya magoli 3-1.

Timu ya Gabon ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia mchezaji wake Emmanuel Ovono, ambaye alifunga goli kwa mkwaju wa penati, baada ya mchezaji kufanyiwa madhambi mwishoni mwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Magoli ya Mali yalifungwa na mshambuliaji Mamadou Sangare (20), kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Mali Ibrahim kuchezewa madhambi, huku mchezaji Cheikhna Doumbia akifunga goli dakika ya 41, kabla ya Alhassane Tamboura kumalizia kazi katika dakika za lala salama.

Egypt kwa upande wao, nao wanacheza mechi ya pili ya keundi, baada ya kutoka sare ya goli 0-0 dhidi ya Niger katika mechi yao ya kwanza ya kundi B katika mashindano haya ya Africa U-23 Cup Nations.

Timu zote mbili zinaingia uwanjani zikiwa zinahitaji ushindi kwa kila timu kwani matokeo yoyote ya sare yataziweka timu hizi yaani Egypt U23 na Gabon U23 katika wakati mgumu wa kusonga mbele katika hatua hii ya makundi.

Hadi wakati huu ambapo tunaandika makala hii kuhusiana na mechi hii ya leo, msimamo wa kundi B unaonyesha Mali anaongoza kwa pointi tatu, baada ya kushinda mechi dhidi ya Gabon lakini ana tofauti ya magoli mawili ya kufungwa.

Egypt U23 na Niger U23 wanafuatia wote wakiwa na pointi moja na kulingana kila kitu kwa kuwa hawakufanikiwa kufungana katika mechi waliyocheza baina yao wenyewe. Hii inatoa tafsiri ya umuhimu wa mechi ya leo kati ya timu ya taifa ya vijana ya Egypt U23 na timu ya vijana ya Gabon U23.

 

Wachezaji wa Egypt U23Kwa upande mwingine Egypt akifanikiwa kutoa sare atakuwa na ahueni kidogo ikiwa timu ya Mali U23 ikifanikiwa kuifunga timu ya Niger U23. Hali itakuwa tofauti kama Niger U23 naye atajikaza na kutoa suluhu au kushinda kwani atapanda mpaka nafasi ya pili, hivyo kulazimisha kuanza kuangalia idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Takwimu za timu hizi zinaonyesha timu ya Egypt U23 katika mechi yao ya kwanza walifanikiwa kupiga mashuti 17, huku mashuti matatu yakifanikiwa kwenda on taget. Wachezaji wa timu ya Egypt U23 walifanikiwa kumiliki mpira kwa asilimia 62.

Umiliki wa mpira kwa Egypt U23 ulienda sambamba na asilimia 65 ya pasi sahihi zilizopigwa na kufikwa kwa walengwa, huku wakifanikiwa kupata kona 6.

Kwa upande wa timu ya vijana ya Gabona U23 wao katika mechi yao dhidi ya Mali U23 walifanikiwa kupiga mashuti 8, lakini ni shuti moja tu lililofanikiwa kwenda on target au kulenga lango la mpinzani, ambaye ni Mali U23.

Kwa upande wa umiliki wa mpira timu ya Gabon U23 walifanikiwa kumiliki kwa asilimia 37 na kufanikiwa kupiga pasi 270 katika mechi yao dhidi ya Mali U23. Umiliki huo ulienda sambamba na upigaji au utawanyaji wa pasi zilizokamilika kwa asilimia 67, huku timu hii ya Gabon U23 ikikosa kupata hata kona moja.

Timu ya Egypt U23 watakuwa wanawategemea wachezaji wao kama kipa Yehia Elderaa, kiungo Ibrahim Adel anayekipiga Pyramids, Mohamed Mahmoud, Mostafa Saad Abdallah Sayed, huyu ni winga anayekipiga Smouha, Abdel Rahman Atef Yousef huyu ni mshambuliaji wa Ghazl El Mahalla.

Kwa upande wa Gabon U23 nao wataingia uwanjani wakiwategemea wachezaji kama Emmanuel Ovono, huyu ni mshambuliaji wat imu ya Torpedo, watakuwa pia wakimtegemea beki kisiki Jeremy onyodo, Jhovany Mayoulou Ikangui, Moussango Jeremie Obounet.

Hawa ni baadhi ya nyota wat imu zote mbili ambao wanategemewa kukipiga siku ya leo.

Mchezo huu tayari upo katika tovuti yetu. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

 

Share this: