PortugalU21Portugal-U-

Patashika ya michuano ya Ulaya ya U21 ya European Championship kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21 inaendelea kuchanja mbunga ambapo siku ya keso Jumanne ya Juni 27,2023 katika dimba la Mikheil Meskhis Sakhelobis, utapigwa mchezo wa mwisho wa kundi A ukizikutanisha timu ya Portugal U21 dhidi ya Belgium U21.

Timu ya taifa ya Portugal U21 watahitaji kushinda dhidi ya timu ya Belgium U21 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi A ili kuweka hai matumaini ya  kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya kwa Vijana wenye umri wa miaka 21.

Kikoci hicho kinachonolewa na Kocha Rui Jorge wapo mkiani mwa kundi A, wakiwa na alama moja pekee wakati timu ya Belgium U21 wapo nafasi ya pili wakiwa na alama mbili baada ya mechi mbili walizocheza za awali.

Ureno haijawahi kushinda taji la mashindano ya Ulaya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21  ingawa walifanikiwa kutinga fainali mara tatu na mara ya mwisho ni mwaka 2021 walipopoteza mbele ya timu ya Germany U21.

Licha ya kufanya vizuri mwaka 2021, kwa sasa hali ni tofauti kwani wanapambania nafasi ya kufuzu robo fainali na wana alama moja pekee katika michezo miwili ya awali, walipoteza bao 2-1 dhidi ya Georgia kabla ya kutoka sare ya bao moja dhidi ya timu ya Ntherlands U21.

Katika mchezo uliochezwa siku ya Jumamosi, timu ya Portugal U21 waliandika bao kupitia kinara wao wa kupachika mabao Andre Almeida lakini Uholanzi walisawazisha kupitia Brian Brobbey.

Ushindi kwa timu ya Portugal U21 utawafanya wafikishe alama 4 sawa na Georgia, lakini vinara watasalia kileleni mwa kundi A kutokana na matokeo ya timu hizi zilipokutana.

Kutokana na matokeo haya, timu ya Portugal U21 inahitaji kushinda mchezo wao huku wakiiombea timu ya Georgia U21 kuizuia timu ya Netherlands U21 kupata ushindi ili wao wafanikishe mpango wa kumaliza nafasi ya pili na hatimaye wafuzu kucheza robo fainali.

Timu ya Belgium U21 kwa sasa wapo nafasi ya pili baada ya suluhu dhidi ya Netherlands U21 na sare ya bao mbili dhidi ya Georgia.

 

Belgium U 21 vs Portugal U21Kikosi hicho kinachonolewa na Jacky Mathijssen kiliongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Georgia U21, shukrani kwa mabao ya wachezaji Maxim De Cuyper na Largie Ramazani, lakini vinara wa kundi walisawazisha na kukamata usukani.

Timu ya Belgium U21 watafuzu katika hatua ya mtoano iwapo watashinda leo usiku dhidi ya timu ya Portugal U21 vilevile sare itatosha kwao iwapo Netherlands U21 watashindwa kuifunga timu ya Georgia U21.

Kwa mara ya mwisho timu ya Belgium U21 kufanya vizuri katika mashindano haya ni mwaka 2007 ambapo walitinga nusu fainali lakini cha kushangaza walishindwa kufuzu katika mashindano hayo 2021.

Kikosi cha timu ya Portugal U21, kipo kamili kikiwa na nyota bora na wenye uzoefu  kama Nuno Tavares, Andre Almeida, Pedro Neto na Fabio Silva ambao wamecheza kwenye mechi mbili za makundi.

Kocha Mkuu wa timu ya Portugal U21 Jogre ana wakati mgumu wa kufanya maamuzi na upo uwezekano akamuweka benchi Fabio Silva katika kikosi cha kwanza huku nafasi yake ikitarajiwa kukabidhiwa kwa Henrique Araujo.

Diego Moreira na Francisco Conceicao nao wapo kwenye hekaheka za kujumuishwa kwenye dakika tisini za mchezo na huenda benchi likawahusu katika mchezo wa mwisho dhidi ya timu ya Belgium U21.

Upande wa timu ya Belgium U 21 utaendelea kumtegemea mchezaji Lois Openda katika safu ya ushambuliaji, huku nyota huyo kutoka Lens ya Ufaransa akiwa ametupia mabao 13 katika mechi 17 alizocheza katika ligi kuu Ufaransa Ligue 1.

Ramazani alifunga bao katika mchezo dhidi ya Georgia U21 na huenda akaendelea kusalia kikosini katika mchezo wa mwisho, vilevile inatarajiwa kumshuhudia mshambuliaji anayekipiga  katika timu ya ligi kuu Italia AC Milan, Charles De Ketelaere kuanza katika kikosi cha timu ya Belgium U21.

Mchezaji Hugo Siquet kwa mara nyingine atacheza nafasi ya beki wa kulia naye Mandela Keita akitarajiwa kucheza katika eneo la kiungo licha ya uwepo wa ushindani wa nafasi katika safu hiyo.

Tayari mechi hii ipo katika tovuti yetu. kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

 

 

Share this: