Belgium U 21Belgium-U

Jumatano ya kesho, yaani Juni 21,2023, mabingwa mara mbili wa michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 Uholanzi (Netherlands U21),  wataianza kampeni yao ya kuwania ubabe katika bara la Ulaya, watakapoumana na timu ya Ubelgiji (BelgiumU21) katika michuano ya U21 European Championship

Mchezo huu wa kundi A utapigwa katika uwanja wa Mikheil Meskhi huko Tbilisi,  ambapo Uholanzi ambao walitwaa Ubingwa miaka ya 2006/7 watawakabili Ubelgiji ambao wao wanaisaka nafasi ya kucheza angalau fainali ya michuano hii ya Vijana.

Inafahamika kwamba kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji kinaondoka huku kikiwa kimeshindwa kutwaa ubingwa, hivyo The Young Devils wanatazamiwa kuvaa viatu vya kaka zao na kubadilisha mtazamo juu ya kile ambacho wameshindwa kukamilisha kaka zao kama Eden Hazard, Kevin De Bruyne, Romelu Lukaku, Dries Mertens na wengineo.

Tangu wafuzu nusu fainali za michuano hii ya Ulaya ya vijana wenye umri chini miaka 21 mwaka 2007 ambao ndio ulikuwa ndio ushiriki wao kwa mara ya pili katika michuano hii.

Ubelgiji wamefuzu mara mbili pekee kati ya mara nane ikiwemo mwaka 2023 na walitupwa nje katika hatua ya makundi bila ya alama kwenye hatua ya makundi ya michuano ya mwaka 2019.

Jacky Mathijssen ambaye alikuwa ndiye Kocha wa Ubelgiji iliyoshindwa kufuzu fainali hizi 2021, ndiye aliyeiongoza timu hiyo kutopoteza mchezo dhidi ya Romania pamoja na Georgia na sasa wameshinda mechi sita, wametoa sare mechi mbili kwenye michezo ya kufuzu huku wakiongoza kundi lililokuwa na timu za Denmark, Uturuki, Kazakhstan na Scotland.

Ubelgiji wamekuwa na michezo kadhaa ya kirafiki na hivi karibuni waliibuka na ushindi dhidi ya Japan na Israel, huku wakifunga mabao matano ndani ya michezo hiyo miwili.

Matokeo hayo  yamewapa imani kuwa wanaelekea kwenye mashindano wakiwa kwenye kiwango kilicho bora na cha uhakika.

Wakati The Young Devils walimaliza kwenye nafasi nne za juu miaka kumi na sita iliyopita, Uholanzi walitwaa mara mbili mfululizo mataji miaka ya 2006/7 na kuchukua utawala wa soka la vijana katika kipindi hicho.

Tangu mwaka 2009, The Jong Orange wamekuwa na wakati mzuri ndani ya miaka saba iliyopita na kama ni kutolewa basi wamekuwa wakiishia kwenye hatua ya nusu fainali ambapo walifanya hivyo mwaka 2013 na 2021.

Ni timu chache sana ambazo katika msimu huu zilifanikiwa kuuvunja ukuta wa Kocha Erwin van de Looi ambaye anakinoa kikosi hicho.

De Looi ameiongoza The Jong Orange kufuzu wakiwa vinara tena bila ya kupoteza wakiwafanya Switzerland,Moldova,Wales, Bulgaria na Gibralter wakiwa chini yao.

wachezaji wa Netherlands U21 vs BelgiumKatika mechi kumi walizocheza vijana wa Uholanzi wameruhusu bao tatu pekee kitu ambacho kinawafanya wawe ni miongoni mwa timu tatu zilizo na safu bora ya ulinzi ikiwemo Ureno.

Ushahidi juu ya uimara wa safu ya ulinzi ya The Jong Orange unathibitishwa kupitia michezoya hivi karibuni ya kirafiki ambapo wamecheza michezo mitano huku mitatu kati ya hiyo hawajaruhusu bao na wameendeleza rekodi ya kutopoteza katika michezo kumi na tano waliyocheza kwenye mashindano yote.

Mara ya mwisho kwa Uholanzi kupoteza ilikuwa ni dhidi ya Ujerumani kwenye nusu fainali ya michuano ya mwaka 2021,lakini mechi nyingine ambazo walitoka sare ni dhidi ya Jamhuri ya Czech na Japan.

Timu hizi mbili zinakutana zikiwa na matokeo yanayoshabihiana pindi walipokutana ambapo kila timu imeshinda mechi tatu na mara ya mwisho walipokutana kwenye mchezo wa kirafiki mwezi septemba mwaka jana, Uholanzi iliibuka na ushindi dhidi ya Ubelgiji wa bao 2-1.

Hakuna upungufu wa wachezaji wenye uzoefu kwenye kikosi cha Ubelgiji ambapo Kocha Mathijssen atamjumuisha Lois Openda kuiongoza safu ya ushambuliaji akiwa na takwimu bora akiwa na Lens ya Ufaransa akiwa amepachika bao 21 msimu uliomalizika.

Ikumbukwe mshambuliaji huyo ameisaidia Lens kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Ufaransa ambayo bingwa wake ni PSG.

Openda alijumuishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Ubelgiji kinachowania kufuzu Euro 2024, lakini ameachwa makusudi kwa ajili ya michuano hii ya vijana sawa na Ameen Al-Dakhil, na Olivier Deam .

Licha ya kuanza kwa kusuwasuwa tangu ajiunge na AC Milan, Charles Deketelaere, bado amekuwa namba 10 bora ya kuchungwa sambamba na nyota wa Rangers Nicolas Raskin ambaye alifunga bao kwenye ushindi wa Uholanzi wa bao 2-0 dhidi ya Israel wote wanatarajiwa kuanza katika eneo lakiungo.

Bahati mbaya kwa kinda anayekipiga kwa Liverpool , Sepp van de Berg  amepata maumivu ya mgongo na amejiondoa kwenye kikosi na nafasi yake imechukuliwa na Shurandy Sambo wa Sparta Rotterdam .

Nyota watatu wa timu ya wakubwa Ryan Gravenberch, Devyne Rensch na Kenneth Taylor wameachwa na Kocha Ronald Koeman ili waendelee na maandalizi na timu ya Vijana, huku beki wa pembeni wa Bayer 04 Leverkusen, Jeremie Frimpong  ameachwa kwenye kikosi hicho.

Mechi hii ipo tayari kwenye tovuti yetu. Kucheza tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

 

Share this: