Mchezaji wa Yanga Fiston MayeleMicrosoftTeams-image-

Ikiwa leo ndio tamati ya Ligi kuu Tanzania bara, Yaani NBC Premier League msimu wa 2022/23, mchuano mkali upo katika kipengele cha mfungaji bora baina ya Fistona Mayele dhidi ya Saido Ntibanzokiza, ambapo wachezaji hawa wanaowakilisha Yanga na Simba wanawania tuzo ya kiatu cha dhahabu ama mfungaji bora.
Kuna saprise inaweza kutokea kama ambavyo makala yetu ya mwisho kuhusiana na ligi hii ilivyojadili. Kwa wale ambao ni wafuatiliaji katika makala ya wikiendi iliyopita tuliangazia zaidi timu zilizo katika top four, yaani Yanga, Simba, Azam na Singida.
Katika makala ile tuligusia kwa undani takwimu zinazohusu timu mbali mbali kwa kuangalia idadi ya magoli ya kufunga, kufungwa, clean sheets, wanaoongoza kwa kufunga magoli, kutoa assist, kuzuia n.k.
Kama ilivyokuwa kwenye makala hiyo tulijadili mechi za juzi kwa maana ya Tarehe 6 Mwezi huu wa Sita 2023 zinazoweza kuleta mabadiliko katika takwimu za mwisho wa msimu.
Mnyukano huo umekolezwa vilivyo na kiungo mshambuliaji wa wekundu wa Msimbazi, Saido Ntibazonkiza ambaye katika mchezo wa juzi Tarehe sita, dhidi ya Polisi Tanzania aliweka kambani mabao 5 peke yake na sasa amefikisha jumla ya magooli 15 akimsogelea kinara Fiston Kalala Mayele wa Yanga mwenye bao 16.
Saido ambaye amewahi kuichezea Yanga akiwa na Mayele, alitupia kambani mabao hayo na sasa amefanya mechi za kesho kusubiriwa kwa hamu na kuona ni nani kati yao ataondoka na kiatu cha dhahabu kama mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC Premier League, msimu wa 2022/23
Nyota huyo wa kimataifa wa Burundi alikuwa na mabao 10 kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Polisi Tanzania hapo juzi.
Shinikizo linakuwa kubwa kwa Fiston Mayele ambaye kwa siku za karibuni hajawa katika nafasi ya kufunga katika Ligi Kuu na hii pengine ilichagizwa na fikra nyingi kuwa alizielekeza kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Fiston Kalala Mayele raia wa Congo,alikuwa akitumika kimkakati katika baadhi ya mechi za hivi karibuni ili kumpa nafasi ya kupumzika na kiuhalisia maamuzi ya benchi la ufundi yalililipa,ambapo mshambuliaji huyo alifunga mabao muhimu yaliyoipeleka timu hiyo fainali ya Kombe la Shirikisho na pia akaibuka mfungaji bora wa mashindano akiwa na bao 7 ,akimpiku Ranga Chivaviro wa Marumo Gallants aliyemaliza na bao 6.
Kinyang’anyiro hiki kinarudisha nyuma kumbukumbu ya msimu uliopita ambapo Fiston Mayele alikosa tuzo ya mfungaji bora licha ya kuongoza kwa tofauti ya bao 5 dhidi ya George Mpole aliyekuwa akikipiga na Geita Gold ambaye aliibuka kidedea kwa kupachika bao 17.
Stori ni kama inataka kujirudia kwani George Mpole alifunga bao katika mchezo wa mwisho dhidi ya Coastal Union ya Tanga,na safari hii Saido Ntibazonkiza anahitaji bao mbili ili kufikisha bao ili kumpiku Mayele,ikumbukwe Simba katika mchezo wa mwisho watakabiliana na Coastal Union.

Mchezaji Saido Ntibazonkiza,Simba
Wakati Saido Ntibazonkiza atakuwa na kibarua dhidi ya Coastal Union,stori ni tofauti kwa Fiston Mayele ambaye baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger,alipumzishwa na hata katika mchezo uliopita wa Yanga waliotoka sare ya bao tatu raia huyo wa Congo DR hakujumuishwa kwa lengo la kumpa nafasi ya kujiweka sawa kabla ya fainali ya michuano ya ASFC ambayo itapigwa Juni 12 huko Tanga.
Swali ni je, Kocha Nassredine Nabi atalazimika kumpanga katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu baina yao na Tanzania Prisons ili kumpa nafasi pengine ya kujitengenezea mazingira ya Mayele kufunga mabao ambayo yanaweza kumfanya awe mfungaji bora msimu huu?
Je ni kwa kiasi gani Mayele ataweza kuhimili shinikizo hilo pasipo kuathiri aina ya uchezaji wake ili isije kupoteza saikolojia yake iwapo lolote litatokea kabla ya fainali ya ASFC?
Swali jingine ni je,Saido Ntibazonkiza anaweza kuendeleza moto aliouwasha dhidi ya Polisi Tanzania?nyota huyu amekuwa na tabia ya kufunga bao nyingi katika michezo na msimu huu amepiga Hat Trick mbili, hili ni jambo ambalo linaweza likawa kikwazo kwa Mayele ambaye pia ndani ya msimu huu amefunga Hat Trick moja.
Ukitazama Saidi Ntibazonkiza yupo kwenye nafasi bora zaidi ikilinganishwa na Mayele ambaye atakuwa na tahadhali kubwa ili asiumie kwenye mchezo wa Tanzania Prisons kabla ya kuivaa Azam katika mchezo muhimu utakaopigwa siku mbili baada ya mchezo wa Ligi Kuu.
Ukiachana na kiatu cha ufungaji bora,Saido Ntibazonkiza na Fiston Kalala Mayele wote wapo katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu.
Mastaa hawa wa kimataifa wanazo takwimu bora sana, Saido Ntibazonkiza ndiye kinara wa kuhusika kwa mabo mengi ndani ya msimu huu ambapo amefunga bao 15 na kutengeneza nafasi za mabao 12 hivyo kahusika katika jumla ya mabao 27 katika michezo 22.
Fiston Kalala Mayele yeye amehusika katika mabao 21 katika Ligi hiyo, amefunga bao 16 na katengeneza nafasi 4 za mabao.
Huenda takwimu hizi nazo zikaongeza kitu kwenye maamuzi ya ni yupi anaweza kutangazwa kuwa mchezaji bora japokuwa namba pekee hazitoshi kuamua hilo.
Maswali ni je,nani kati ya mafahali hawa wawili atakayetumia nafasi kati mechi za mwisho za kufunga pazia la Ligi Kuu ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwa mfungaji bora na hata mchezaji bora.
Tayari SportPesa tumeshakuwekea mechi ya Tanzania Prisons VS Yanga, Simba VS Coastal Union, Azam VS Polisi Tanzania, Mtibwa VS Geita Gold, Mbeya City VS KMC, Ihefu VS Kagera Sugar, Ruvu VS Dodoma FC, Namungo VS singida kwenye tovuti yetu. Kubashiri mechi hii na zinginezo tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

Share this: