Leo Juni 3,2023 katika dimba la Wembley jijini London utapigwa mchezo wa Fainali ya Kombe la FA ikizikutanisha timu za Manchester City na Manchester United.
Hii ni Fainali ya ya watani wa jadi ambao wanakutana katika hatua katika hatua kama hii kwa mara ya kwanza jambo linaloleta mvuto wa aina yake.
Kinachoongeza utamu na ushindani katika fainali hii ni kwamba, Manchester City wapo katika safari ya matumaini ya kuifikia rekodi iliyowekwa na Manchester United mwaka 1999 iliyokuwa ikinolewa na Kocha Sir Alex Ferguson ambapo walitwaa (Treble) mataji matatu makubwa yaani Ligi Kuu EPL, FA Cup na Klabu bingwa Ulaya hivyo timu ya kwanza kuzuia rekodi hiyo kufikiwa ipo mikononi mwa The Red Devil’s wenyewe.
Inafahamika tayari Manchester City wameshatwaa EPL na iwapo watatwaa FA tafsiri yake watahitaji kuifunga Inter Milan katika fainali ya Klabu bingwa itakayopigwa wiki moja baadae katika Jiji la Instabul nchini Uturuki ili wakamilishe ndoto yao ya kuwa Klabu ya pili ya England kutwaa Treble.
Kwa kuzingatia kuwa wenye uwezo wa kuizuia rekodi hiyo iliyodumu kwa miaka 24, ipo mikononi mwa Manchester United, beki wa The Citizen, Nathan Ake amewaonya wachezaji wenzake kuwa makini.
Anasema kuwa anafahamu fika kuwa The Red Devil’s wanauwezo wa kuwashangaza kama ambavyo walifanya katika mchezo wa mwisho, walipookutana nao Mwezi Januari 2023 na kuwafunga mabao 2-1.
Inakumbukwa licha ya Man City kuongoza hadi dakika za mwisho, Bruno Fernandes alifunga bao ambalo lilizua utata kabla ya Marcus Rashford kupigilia msumari wa moto muda mchache baadae na kuwafunga Manchester City.
Kocha wa Manchester United Eric Ten Haag,’ yeye amesema watahitaji kucheza kwa usahihi (Perfect game) iwapo watahitaji kuwafunga vijana wa Pep Guardiola na amesisitiza kwamba wapo tayari kujitoa zaidi katika mchezo huo.
Ifahamike kwamba Ten Haag ameuanza vyema msimu wake wa kwanza ndani ya Man United akiwa amekamilisha mpango wa kuirejesha Klabu hiyo kwenye michuano ya Klabu bingwa Ulaya,ametwaa taji la EFL hivyo iwapo ataifunga Manchester City Jumamosi atakuwa ametwaa mataji mawili muhimu ndani ya msimu wake wa kwanza,na itakuwa ishara bora katika kazi yake na kurejesha imani kwa mashabiki.
Ikumbukwe Man United iliifunga Newcastle United kwenye mchezo wa Fainali ya EFL kwa kuitandika bao 3-0.
Safari ya Man United katika michuano ya FA Cup ilianza kwa kuzitandika Everton, Reading na West Ham kwa bao 3-1 Kila timu kabla ya kuiondoa Fulham kwenye robo fainali kwa kuwanyuka 3-1 kisha wakamalizia kazi dhidi ya Brighton & Hove Albion kwa kuwafunga kwa penati baada ya muda wa ziada.
Manchester United yenyewe ilianza kwa kuviangusha vigogo ambavyo ni Chelsea waliyoipa kipigo cha 4-0, Arsenal 1-0, kisha ikazitupa nje Bristol City kwa kipigo cha 3-0, ikaisambaratisha Burnley kwa 6-0 na nusu fainali wakawanyoa Sheffield kwa bao 3-0.
Timu hizi zinakutana zikiwa katika ubora ambao haujatofautiana sana kupitia mechi za hivi karibuni ambapo Man City imeshinda mechi 3 kati ya 5 za mwisho, wakipoteza moja dhidi ya Brentford na sare dhidi ya Brighton lakini kwa Manchester United ipo kwenye kiwango cha lami kwani katika mechi 5 za mwisho wameshinda 4 na kupoteza moja dhidi ya West Ham United.
Katika mechi hizo 5 za mwisho,Manchester United imefunga bao 9 na kuruhusu bao 3, imefunga bao zaidi ya mawili katika mechi 2 kati ya tano,na imeruhusu bao 2 kati ya mechi hizo 5.
Manchester City wao wamefunga bao 9 na kuruhusu mawili, wamefunga bao zaidi ya 2 na kuendelea katika mechi 2 kati ya 5 na pia katika mechi hizo 5 ni mbili ambazo timu zote ziliruhusu bao.
Rekodi zinaonyesha kwamba katika mechi 20 za mwisho timu hizi kukutana kila timu imeshinda mara 9, sare 2.
Katika mechi 5 za mwisho walizokutana, Manchester City imeshinda mara 3 na Manchester United imeshinda mara 2 hakuna sare.
Mnamo Machi 7, 2021, Man City ilinyukwa bao 2-0 katika dimba la Etihad, Novemba 6,2021, Man City ikalipa kisadi kwa kuwafunga Man United pale Old Trafford bao 2-0.
Machi 6, 2021, Manchester City ilitoa kipigo kizito cha bao 4-1 kwa Man United kabla ya kurejea tena kwa staili hiyo hiyo mnamo Oktoba 2,2022 walipoizaba Man United bao 6-3 katika dimba la Etihad.
Ten Haag alizinduka mnamo Januari 14,2023 mapema mwaka huu wakiifunga Man City bao 2-1 katika dimba la Old Trafford.
Katika mechi hizi, Manchester City imefunga bao 13 wakati Man United imefunga bao 8, mechi 3 kati ya 5 zilizalisha mabao zaidi ya mawili na jumla ya michezo mitatu kati ya mitano ilishuhudiwa timu hizo zikifungana mabao.
Kwa mujibu wa mtandao wa Sports Mole unaohusika na kuchakata takwimu umearifu kwamba Manchester City ina nafasi kubwa ya kushinda mechi hii.
Takwimu hizi zinatokana na kiwango cha timu,matokeo ya karibu na Viwango vya wachezaji.
The Citizen wamepewa 48.64%, Red Devil’s wamepewa 27.75% huku sare ikipewa 23.6 %.
Utabiri umeendelea kufafanua ushindi wa 2-1 kwa Man City unapewa 9.5%, ushindi wa The Citizen wa 1-0 umepewa 8.73% na ushindi wa 2-0 una 7.57%.
Kwa Manchester United kushinda bao 2-1 una 6.88%, kutoka sare ya 1-1 wamepewa 10.95%.
Timu zote kufungana imepewa 58.87%, mchezo huo kutoa bao zaidi ya mawili (over 2.5) imepewa 57.43% wakati mabao chini ya mawili (under 2.4) imepewa 42.57%.
Takwimu hizi zitakusaidia kuamua utabiri vipi kupitia Sportpesa kwakuwa machaguo yapo mengi na unaweza jishindia donge nono, tabiri sasa kwa kutembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

