Kimbembe cha mechi ya mkondo wa pili ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, kitapigwa Mei 17, 2023 ambapo timu ya Marumo Gallants, watakuwa nyumbani nchini South Africa wakijaribu kupindua matokeo ya kipigo cha mabao 2-0 walichokipata kutoka kwa Yanga kwenye mchezo uliopigwa Tarehe 10 May 2023 kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa leo wa marudiano utachezwa katika dimba la Royal Bafokeng Kaskazini Magharibi mwa kitongoji cha Phoken nchini Afrika Kusini na itachezwa majira ya saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Ugumu wa mchezo huu kwa Yanga unachagizwa na Marumo ambao kwanza wana rekodi nzuri wanapocheza katika ardhi ya nyumbani ambapo kwenye mechi 9 za mwisho za CAF, hawajapoteza hata mechi moja, wameshinda 8 na kutoa sare 1. Hii ni ishara kwamba Yanga watakutana na wakati mgumu katika mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania.
Lakini Yanga nao wanalo la kujivunia kwakuwa nao wanayo rekodi nzuri katika mashindano ya CAF mwaka huu, wamepoteza mechi 2 pekee (Al Hilal na Us Monastir) katika hatua zote,lakini nao wameshinda mechi 3 ugenini(dhidi ya Club Africain,Tp Mazembe na Rivers United) huku wakitokea sare dhidi ya Real Bamako,jambo ambalo linawapa jeuri ya kutunisha msuli katika mchezo huo.
Jambo kubwa ambalo Yanga wanawania kulifanya ni kuhakikisha hawafungwi mabao matatu kwa sifuri, Iwapo watapoteza basi isiwe kwa tofauti ya bao moja. Hapo moja kwa moja watakuwa wamefuzu kucheza hatua ya kimashindano ya kombe la shirikisho Africa kwa kufanikiwa kufainali ya kihistoria,na takwimu zinawabeba hadi sasa kwani hakuna mchezo ambao Yanga wamepoteza kwa mabao zaidi ya mawili.
Rekodi nyingine inayowabeba Yanga na kudhihirisha wapo imara kimbinu, ni kwamba Yanga wamecheza mechi 6 mfululizo bila kuruhusu bao. Hii ni ishara tosha kwamba Marumo wanayo kazi ya ziada ya kufanya iwapo watahitaji kupindua matokeo mbele ya mashabiki wao ambao wamealikwa kushuhudia mchezo huo bila kiingilio.
Je inawezekana Marumo na Yanga watatuonyesha kile walichokifanya kwa Mkapa?
Ukitazama takwimu za mchezo zinaonyesha Marumo walimiliki mchezo kwa asilimia 51 wakati Yanga walikuwa na alimia 49, Marumo walipiga pasi nyingi zaidi (502) wakati Yanga walipiga pasi (490) lakini Yanga ndio waliongoza kwa kupiga mashuti(20) na 8 yalilenga lango wakati Marumo walipiga mashuti (8) na 4 yalilenga lango.
Takwimu hizi zinaonyesha Yanga walikuwa na lengo la kufunga mabao na si vinginevyo, wakawaachia Marumo wakae na mpira jambo lililofanikiwa.
Hata baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza wiki iliyopita, Kocha wa Yanga Nassredine Nabi alisema mechi haijaisha na wanayo kazi ya kufanya kwakuwa Marumo ni wazuri ingawa na yeye anaujua ubora wao na madhaifu na anayafanyia kazi kabla ya kukutana tena hapo kesho.
Nabi alisema Marumo wana viungo bora wenye uwezo wa kukaa na kumiliki mpira huku wakishambulia kwa kasi ama tempo ya juu.
Kwa kudhihirisha hilo, takwimu zinaonyesha hakuna mchezaji aliyepiga pasi nyingi katika mchezo huo kama Olivier Toure (67) ambaye akifuatiwa na Khalid Aucho wa Yanga, aliyepiga pasi (63).
Pamoja na kumiliki na kupiga pasi nyingi, lakini Marumo walijikuta wakimpa kazi kubwa mlinda mlango wao Washington Arubi ambaye aliokoa michomo 6 katika mchezo huo. Tafsiri yake ni kwamba safu yao ya ulinzi ilikua ina madhaifu tofauti na Yanga ambao Djiguir Diarra aliokoa michomo 4 tu katika dakika zote 90.
Dyllan Kerr Kocha wa Marumo amesema ataikabili Yanga kwa namna tofauti na ana imani watapata matokeo mazuri. Mshindi wa mchezo huu wa nusu fainali ya pili atakutana na mshindi kati ya USM Alger na Asec Mimosas ambazo katika mchezo wa mkondo wa kwanza walitoka suluhu ya bila kufungana.
Ni matumaini yetu uchambuzi wa mechi hii umekupa ahueni wewe msomaji wetu.
SportPesa tukiwa kama wadau wa michezo na burudani na pia wadhamini wakuu wa timu ya Yanga tumeshaiweka mechi hii katika tovuti yetu. ili uweze kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

