Everton vs LeicesterLEICESTEREVERTON

Majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye’’ Monday Night Football’’ itashuhudiwa kipute cha kukata na shoka huko King Power Stadium ambapo Leicester City watakuwa wenyeji wa Everton ikiwa ni muendelezo wa hekaheka za timu zote mbili kujinasua na janga la kushuka daraja.

Klabu hizi mbili kwa pamoja zipo kwenye mstari wa hatari wa kuporomoka daraja ambapo Leicester City (The Foxes) wapo kwenye nafasi ya 18 wakiwa na alama 29 huku Everton (The Toffees) wao wapo nafasi ya 19 wakiwa na alama 28.

Tafsiri nyepesi ni kwamba vita ya kwanza katika mchezo huu ni kila mmoja anahitaji kuongeza alama tatu ili kujisogeza juu ya msimamo kwani juu ya vibonde hawa zipo Nottingham Forest waliopo nafasi ya 17 wakiwa na alama 30 wakati Leeds United ipo nafasi ya 16 wakiwa na alama 30 pia.

Iwapo Leicester City itashinda katika mchezo huo watafikisha alama 32 na watazishusha Nottingham Forest na Leeds United  na watachupa hadi nafasi ya 16 huku wakiwatoroka Everton,lakini iwapo The Toffees watashinda watafikisha alama 31 na watawashusha Leicester City walio juu yao kwa tofauti ya alama moja.

Mchezo wa mkondo wa kwanza wa EPL, mabao ya Youri Tielsman na Harvey Barnes yaliwapa ushindi Leicester City dhidi ya Everton waliokuwa kwenye dimba lao la nyumbani la Goodson Park.

Leicester City na Everton zote kwa pamoja zinakutana zikiwa na makocha wapya baada ya wale waliokuwepo awali Frank Lampard na Brendan Rodgers kutimuliwa kufuatia mwenendo mbovu uliopeleka wawe katika nafasi waliyopo hivi sasa.

Lakini licha ya kuwapa kibarua makocha wapya ambao ni Dean Smith kwa Leicester City na Sean Dyche kwa Everton bado timu hizo zimeendelea kuwa kwenye mwenendo wa kudorola na hadi sasa hazijainuka kutoka zilipokuwa zimeachwa na Frank Lampard (Everton) na Brendan Rodgers (Leicester City).

Sean Dyche alijiunga na Everton Januari 30,2023 na ameiongoza katika michezo 13, ameshinda michezo mitatu tu,akitoka sare 4 na amepoteza katika michezo 6 lakini upande wa Dean Smith alijiunga na Leicester City April 13,2023  na kuikuta ikiwa kwenye nafasi ya 19 na ameiongoza The Foxes kwenye michezo mitatu,ameshinda 1,sare 1 na kapoteza mechi 1.

Katika mchezo uliopita,Everton imekutana na kipigo kizito cha bao 4-1 katika dimba lao la nyumbani dhidi ya Newcastle United jambo ambalo lina ashiria wapo katika hali mbaya lakini upande wa Leicester City walipata sare ya bao moja dhidi ya Leeds United.

Michezo mitano ya mwisho ya Leicester City inaonyesha kuwa wamepoteza mara tatu, wameshinda mara moja tu na sare moja wakati upande wa Everton wao wamepoteza mechi tatu na sare mbili.

Kuelekea mchezo wa kesho Kocha wa Leicester City, Dean Smith amesema atamkosa mshambuliaji wake Kelechi Iheanacho atakayekaa nje ya dimba kwa wiki kadhaa zijazo kutokana na majeraha ya misuli. Kwa upande wa Everton Kocha wake Dean Smith amethibitisha upo uwezekano wa kurejea kwa Seamus Coleman baada ya kukosekana kwa majeraha kwenye mechi iliyopita.

Sean Dyche amesema kuwa’’Hata wawe wamekarishwa tama kiasi gani baada ya kipigo cha 4-1 kutoka kwa Newcastle United lakini naamini wataendelea kuiunga mkono timu yao hadi mwisho wa msimu’’.

Kwenye michezo mitano ya mwisho waliyokutana Everton ni wababe kwa kushinda mara 2, Leicester City imeshinda mara 1 na sare mbili huku jumla ya mabao 11 yakifungwa na timu zote mbili.

Jambo la kufutia kuhusu timu hizi ni kwamba zinalingana kwenye rekodi ya uso kwa uso kwani katika michezo 28 waliyokutana,kila timu imeshinda mara 9 na sare 10 ikijitokeza hivyo mshindi katika mchezo huo ina maanisha ataboresha rekodi dhidi ya mpinzani wake.

Takwimu zinaonyesha Leicester City imefunga mabao 44, huku 26 kati ya hayo imeyapata kipindi cha kwanza cha mchezo na 18 ni ya kipindi cha pili,hivyo kuelekea mchezo huu Everton wanapaswa kuwa waangalifu zaidi katika kipindi cha kwanza.

Mbweha hao wamepiga jumla ya mashuti 328,huku yaliyolenga lango ni 125 na yaliyo ota mbawa ni 123,wamepiga jumla ya kona 118 na umiliki wa mchezo ni wastani wa asilimia 48.5.

Vilevile vijana wa Dean Smith wameruhusu mabao 57, kipindi cha kwanza wameruhusu mabao 29 na kipindi cha pili wameruhusu mabao 28 hivyo ni kama wana wastani wa kuruhusu bao katika kila kipindi kwa mujibu wa takwimu.

Wachezaji vinara wa mabao wa Leicester City ni Harvey Barnes mwenye bao 10 ambaye anaongoza kwa kupiga mashuti ya kulenga bao (28), James Maddison mwenye bao 9 mwenye mashuti (25), Kelechi Iheanacho bao 5 (atakosekana), Patson Daka mwenye bao 4 na Youri Tielsmans mwenye mabao matat huku kinara wa pasi za mabao wa The Foxes ni James MaEverton vs Leicesterddison (7) akifuatiwa na Kelechi Iheanacho(4).

Takwimu za Everton zinaonyesha imefunga mabao 25,10 ikiyapata kipindi cha kwanza wakati 15 wameyafunga kiupindi cha pili,tafsiri yake wana wastani mzuri wa kufunga mabao katika kipindi cha pili kuliko kipindi cha kwanza cha mchezo.

 

Everton wamepiga jumla ya mashuti 301 huku kati ya hayo 118 ndiyo yaliyolenga lango na 108 hayo hayakulenga lango,wanao wastani wa asilimia 43 ya kumiliki mchezo.

The Toffees imeruhusu mabao 50, kati ya hayo 20 wameruhusu kipindi cha kwanza wakati wakiruhusu mabao 30 kipindi cha pili,tafsiri yake wapinzani wanapaswa kuwa na mpango kazi ambao utawasaidia kufunga mabao kipindi cha pili.

Wachezaji wanao ongoza kufunga mabao kwa Everton ni Dwight McNeil mwenye mabao 5, akifuatiwa na Damarai Gray mwenye bao 4 huku Anthony Gordon ana mabao 3.

Kinara wa kupiga pasi za mabao ni Alex Iwobi (6) akifuatiwa na Demarai Gray (2) pamoja na Dwight McNail (2).

Damaray Gray ndiye mchezaji aliyepiga mashuti mengi yaliyolenga lango upande wa Everton (23) akifuatiwa na Antony Gordon (15) pia Dwight McNeil (13) hivyo hawa ndio wachezaji wa kuchungwa zaidi na Leicester City.

Swali ni je ni timu ipi kati ya Leicester City na Everton itafanikiwa kujikwamua na hatari ya kushuka daraja? Tuma maoni yako kupitia mitandao yetu ya kijamii Facebook na Twitter.

Mechi ipo tayari katika tovuti yetu sportpesa.co.tz. pia unaweza kupiga *150*87#.

Share this: