Singida Black Stars vs Azam FC NBC Premier League ni mechi kali inayofuata. Aprili Mosi, mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Airtel. Saa 10:00 jioni Singida.
SOMA HII: Mashujaa FC yaibana Azam FC NBC Premier League/ Highlights, statics, standings

Singida Black Stars vs Azam FC NBC Premier League utabiri upoje?

Ni Singida Black Stars vs Azam FC NBC Premier League wanakutana kusaka pointi tatu. Katika mechi mbili kubwa wakiwa nyumbani chui walipoteza zote. Ilikuwa Singida Black Stars 0-3 Yanga SC na Singida Black Stars 1-2 Simba SC.
Huu ni mchezo mwingine mkubwa katika ligi namba 6 kwa ubora. Wenyeji wanapewa nafasi kubwa kupata ushindi kutokana na mwendo walionao Machi. Licha yakushindwa kushinda nyumbani wamepata ushindi katika mechi 3 walizocheza tofauti na wapinzani wao Azam FC.
Licha ya Singida Black Stars kupewa nafasi kubwa kushinda, Azam FC ipo katika ubora. Mbinu za Florent Ibenge zimekuwa hazitabiriki hivyo lolote linaweza kutokea. Majibu yatakuwa wazi mara baada ya dakika 90.
H2H Singida Black Stars vs Azam FC NBC Premier League

03/12/2025, Azam FC 0-0 Singida Black Stars
06/04/2025, Singida Black Stars 1-0 Azam FC
28/11/2024, Azam FC 2-1 Singida Black Stars
21/04/2024, Azam FC 1-0 Singida Black Stars
04/11/2023, Singida Black Stars 1-3 Azam FC
13/03/2023, Singida Black Stars 1-0 Azam FC
31/10/2022, Azam FC 1-0 Singida Black Stars
11/03/2021, Azam FC 3-0 Singida Black Stars
20/10/2020, Singida Black Stars 0-2 Azam FC
SOMA HII: NBC Premier League wiki ya moto/ Singida Black Stars vs Simba SC/ Tanzania Prisons vs Yanga SC

Matokeo ya mechi za Singida Black Stars
Machi 2, 2026 Singida Black Stars 1-0 Coastal Union
Machi 5, 2026, Singida Black Stars 0-3 Yanga SC
Machi 11,2026, Singida Black Stars 1-2 Simba SC
Machi 15,2026, Mbeya City 1-4 Singida Black Stars
Machi 18,2026, Tanzania Prisons 1-2 Singida Black Stars
Matokeo ya mechi za Azam FC

Machi 2, 2026, Pamba Jiji FC 2-2 Azam FC
Machi 5, 2926, Tanzania Prisons 0-0 Azam FC
Machi 11,2026, Dodoma Jiji FC 0-3 Azam FC
Machi 15, 2026, Azam FC 0-0 Yanga SC
Machi 19,2026, Mashujaa FC 0-0 Azam FC
Msimamo Singida Black Stars vs Azam FC
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 3. Azam FC | 15 | 7 | 8 | 0 | 29 |
| 6. Singida Black Stars | 15 | 7 | 7 | 4 | 25 |
Kwenye msimamo Azam FC baada ya kucheza mechi 15, (MP) ipo nafasi ya 3, (POS). Ushindi, (W) mechi 7, imetoa sare, (D) mechi 8. Matajiri wa Dar hawajapoteza (L) mchezo.
Singida Black Stars ipo nafasi ya 6 baada ya mechi 15. Imeshinda mechi 7 na imetoa sare mechi 7. Singida Black Stars imepoteza jumla ya mechi 4 ikikusanya pointi 25.
SOMA HII:Azam FC 0-0 Yanga SC Dar Derby/ Highlights, standings, statics

Hitimisho
Singida Black Stars vs Azam FC NBC Premier League haijawahi kuwa mechi nyepesi. Ndani ya Machi, Singida Black Stars imecheza mechi 5, ushindi mechi 3 ikipoteza 2. Matajiri wa Dar ni mechi moja imeshinda na sare 4.

