- Ligi Kuu Hispania, La Liga inaendelea tena wikiendi hii.
- Miongoni mwa michezo muhimu ni ule utaowakutanisha Athletic Bilbao vs Barcelona.
- Katika mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa San Mames Wakatalunya watakuwa wanalenga kupata ushindi wa 3 mfululizo wa La Liga.
Ligi Kuu Hispania La Liga inaendelea tena wikiendi hii. Miongoni mwa michezo muhimu ni ule wa Athletic Bilbao vs Barcelona ambapo Wakatalunya watakuwa wanalenga kupata ushindi wa tatu mfululizo katika ligi kuu ya Hispania. Hii itawafanya kuzidi kujisimika kileleni mwa msimamo wa ligi.
SOMA HII PIA: Barcelona FC- Latest news, fixtures, results, table standings, squad players, transfer news and statistics
Hujashinda mamilioni ya SportPesa?

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.
H2h, Athletic Bilbao vs Barcelona

Katika michezo minne mfululizo iliyopita ambayo timu hizo zimekutana. Barcelona wameonyesha utawala mkubwa wakishinda mechi zote. Pia Barcelona imeandikisha mabao 15 ya kufunga dhidi ya moja tu, la kufungwa.
Fomu ya Athletic Bilbao (La Liga)
LDWWWD
Fomu ya Barcelona (La Liga)
WWWLWW
Vikosi vinavyotarajiwa
Athletic Bilbao:
Kipa: Simon
Walinzi: Vivian, Paredes, Laporte, Boiro
Viungo: Rego, Ruiz de Galarreta, I. Williams, Sancet, Washambuliaji: Berenguer; Guruzeta
Barcelona:
Kipa: J Garcia
Walinzi: Cancelo, Cubarsi, E Garcia, Martin
Viungo: Bernal, Pedri, Yamal, Fermin,
Washambuliaji: Raphinha, F Torres
Taarifa za timu
Kikosi cha kocha Hansi Flick kinaongoza msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Real Madrid walio nafasi ya pili. Athletic wao wanakamatia nafasi ya tisa, pointi tano nyuma ya Celta Vigo walio nafasi ya sita. Athletic wanaingia katika mchezo huu baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Real Sociedad katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Copa del Rey Jumatano.
Kikosi cha kocha Ernesto Valverde sasa kinasalia kuzingatia ligi pekee kwa kipindi kilichobaki cha msimu. Wamekusanya pointi 10, katika mechi zao nne za mwisho. Hii ni baada ya kushinda dhidi ya Levante, Real Oviedo na Elche kabla ya kutoka sare na Rayo Vallecano. Matokeo hayo yanawafanya kukusanya pointi 23.
Barcelona hawajafungwa na Athletic tangu walipopoteza 4-2 katika robo fainali ya Copa del Rey Januari 2024. Katika La Liga hawajapoteza dhidi ya Athletic tangu kipigo cha 1-0, katika uwanja wa San Mames Agosti 2019.
Barcelona wameshinda mechi 21 kati ya 26 za ligi msimu huu, na wanaonekana kuwa timu ngumu kuifunga kuelekea hatua za mwisho za msimu. Pia wamekuwa na makali makubwa ya ushambuliaji, wakifunga mabao 71 katika La Liga msimu huu.
Habari za majeruhi

Athletic watamkosa tena Yeray Alvarez (amesimamishwa), Nico Williams (jeraha la paja), Benat Prados (goti), Unai Egiluz (goti) na Maroan Sannadi (goti).
Hata hivyo, kikosi cha Valverde hakikupata majeraha mapya katika kipigo cha 1-0 dhidi ya Real Sociedad. hivyo wachezaji wale wale wanatarajiwa kupatikana kwa mechi hii. Inawezekana kukawa na mabadiliko kidogo kiungo, ambapo Inigo Ruiz de Galarreta anaweza kuanza.
Lakini Inaki Williams, Oihan Sancet na Alex Berenguer wanatarajiwa tena kumsaidia mshambuliaji Gorka Guruzeta katika safu ya ushambuliaji.
Kwa upande wa Barcelona, Robert Lewandowski amerejea mazoezini baada ya jeraha la mfupa karibu na jicho, na anaweza kupatikana.
Hata hivyo, Andreas Christensen (gotI), Jules Kounde (paja), Alejandro Balde (paja), Frenkie de Jong (paja) na Gavi (gotI) hawatacheza.
Kounde na Balde walipata majeraha katika mechi dhidi ya Atletico Madrid, hivyo Joao Cancelo na Gerard Martin wanatarajiwa kuanza kama mabeki wa pembeni dhidi ya Athletic. Marc Bernal amekuwa katika kiwango kizuri hivi karibuni, na kijana huyo wa miaka 18 ana nafasi kubwa ya kuanza tena kiungo, huku Eric Garcia akitarajiwa kucheza katikati ya ulinzi.
Utabiri na hitimisho
Athletic Bilbao vs Barcelona ni zaidi ya mchezo. Hii ni vita a kuamsha matumaini kwa wenyeji Athletic, huku wageni wakitaka kujisimika kileleni mwa msimamo. Athletic wako katika kiwango kizuri kwenye La Liga, na haitashangaza kama timu hizo zitagawana pointi. Hata hivyo, ubora wa safu ya ushambuliaji ya Barcelona unatabiriwa kuwafanya Barcelona kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda.

