- Joto lipo juu kuelekea mechi ya Yanga SC vs Simba SC Uwanja wa New Amaan Complex, NBC Premier League 2025/26.
- Huku tetesi za Simba SC kugomea, kule jeshi la Yanga SC limetua Zanziba.
- Pacome ashtua! Licha ya taarifa za awali kueleza kuwa, Pacome Zouzoua alikuwa na majeraha ameonekana fitI Zanzibar.
‘Damaro Day’ ndiyo Habari ya mjini. Hii ni jina ambalo umepewa mchezo mkubwa wa dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC utakaopigwa Machi 1, mwaka huu. Mchezo huo ni wa mkondo wa 1 kwa timu hizo msimu huu, na tayari joto limezidi kuwa juu na tambo kutoka pande zote mbili.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC joto linazidi kupanda/ Ratiba, msimamo
Je, unataka kushinda mamilioni ya SportPesa?
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Yanga SC vs Simba SC, mechi yahamia Zanzibar
Mchezo huu ambao hapo awali ulipangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa sasa umehamishiwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar. Hili lilithibitishwa na Taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi Februari 16, mwaka huu. Ikumbukwe kuwa mapema tayari Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe aligusia mabadiliko hayo kabla ya taarifa ya bodi ya ligi, hali ambayo inaelezwa ilianzisha malalamiko kutoka upande wa pili.
Simba wathibitisha kuandika barua

Kutokana na tetesi hizo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amekiri kuwa uongozi umeandika barua kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB). Ambapo pia alisisitiza kuwa mchezo wa Yanga SC vs Simba SC ni mchezo mkubwa hivyo taratibu lazima zifuatwe.
“Nakiri ukweli kuwa tumeandika barua kwenda bodi ya ligi na siyo barua ya kulalamika. Ni barua ya kutaka kupata ufafanuzi zaidi. Mkubwa halalamiki. Barua yetu sio ya kulalamika yaani sisi Simba SC tumlalamikie nani? Kwa sababu kulalamika umeonewa halafu unalalamika. Sisi Simba SC nani wakutuonea nchi hii?
“Tumeandika barua yakutaka kupata ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo, kuelekea mchezo wetu wa Machi Mosi. Hatutapenda kuweka wazi ni mambo gani ambayo tunataka kupatiwa ufafanuzi. Tunafanya hivyo ili kuepusha taharuki. Kwa sababu mechi ya Simba SC na Yanga SC ni mechi kubwa. Tumeandika hiyo barua imekwenda bodi ya ligi na mambo yanakwenda vizuri kwelikweli, tumeshapata majibu na mambo mengine yataendelea.
“Haijawahi kutokea mabadiliko ya uwanja yanatolewa na klabu kabla ya bodi ya ligi. Hapo ndipo tulipopata mashaka, tunavyofahamu sisi mabadiliko yoyote yanatolewa na bodi ya ligi na sio klabu ama ofisa habari wa klabu husika,” alisema Ahmed Ally.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC Uwanja wa New Amaan Complex/ Matokeo ya CAF Champions League
Yanga SC vs Simba SC msimamo unasemaje?

Kwenye muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Bara yaani NBC Premier League 2025/26 mpaka sasa Yanga SC ipo kileleni ikiwa imekusanya pointi 28. Simba wao wanaiendea dabi wakiwa katika nafasi ya tatu, baada ya kukusanya pointi 25. Hii inafanya pengo la pointi kati ya timu hizo mbili kuwa 5.
Jeshi la Yanga latua ‘Guantanamo bay’
Kuelekea mchezo huo muhimu, kikosi cha Yanga SC leo Alhamisi kimewasili rasmi visiwani Zanzibar. Yanga SC mara baada ya kutua Zanzibar, moja kwa moja wameanza maandalizi yao katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Wachezaji wote walionekana kushiriki mazoezi hayo wakiwa na ari kubwa ya kufanya vizuri.

Pacome ashtua!

Licha ya taarifa za awali kueleza kuwa Nyota wa Yanga SC, Pacome Zouzoua alikuwa na majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya JS Kabylie ameonekana akishiriki mazoezi hayo. Ikumbukwe Pacome ndiye aliizamisha Simba SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa Septemba 16, mwaka huu. Nyota huyo amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipojiunga na Wananchi na anatajwa kuwa Nyota hatari zaidi.
SOMA HII PIA: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highlights, magoli yote, h2h – Ngao ya jamii 2025
Hitimisho

Mchezo wa Kariakoo dabi kati ya Yanga SC vs Simba SC mara zote umekuwa na mivutano mikubwa kutokana na uzito wake. Katika miaka ya karibuni Simba SC wamekuwa kwenye nyakati ngumu wakipoteza michezo 6 mfululizo. Hii imesababisha maumivu makubwa kwa mashabiki wao, huku Wananchi wakionekana kuwa na jeuri zaidi. Swali ni Je, mnyama atakubali kuendelea kuwa mteja, au atarudisha heshima.

