Dodoma Jiji FC vs Simba SCAbdi Banda
  • Yanga SC vs Simba SC kituo kinachofuata Machi Mosi, New Amaan Complex
  • Dodoma Jiji FC vs Simba SC ni leo NBC Premier League Februari 25,2026 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma
  • Steve Barker Kocha Mkuu wa Simba SC akiri ugumu wa mchezo

Dodoma Jiji FC vs Simba SC ni ratiba ya leo NBC Premier League 2025/26. Mnyama anakuwa ugenini Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 1:15 usiku. Baada ya mchezo wa leo kituo kinachofuata itakuwa Yanga SC vs Simba SC, Machi Mosi 2026, Uwanja wa New Amaan Complex.

SOMA HII: Tanzania Prisons 0-2 Simba SC NBC Premier League/ Highlights, statistics, standings

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

aviator

Dodoma Jiji FC vs Simba SC utabiri unasemaje?

Dodoma Jiji FC vs Simba SC
Wachezaji wa Simba SC kwenye moja ya mchezo wa ushindani. Source: Simba SC.

Kuelekea mchezo wa Dodoma Jiji FC vs Simba SC utabiri unamuangikia mnyama kwa ushindi. Hii inatokana na rekodi ya mechi za ugenini kupata ushindi asilimia 100. Licha ya Simba SC kupewa asilimia kubwa kushinda bado Dodoma Jiji FC sio timu ya kubeza.

SOMA HII: Timu tano zilikuwa na maajabu ya sabasaba | Yanga SC na Simba SC zatuma ujumbe maalumu

aviator

Msimamo Dodoma Jiji FC vs Simba SC

 MPWDLPTS
4. Simba SC971122
6.Dodoma Jiji FC1555520

Matokeo yaliyopita kwa Simba SC

Februari 22,2026 Tanzania Prisons 0-2 Simba SC

Matokeo yaliyopita kwa Dodoma Jiji FC

Ambudo
Ambudo Dickson nyota wa kikosi cha Dodoma Jiji FC.

Februari 12,2026 Dodoma Jiji FC 3-0 TRA United

Maoni ya kocha wa Dodoma Jiji

Amani Josiah, kocha wa Dodoma Jiji FC amebainisha wamefanya maandalizi vizuri. Kocha huyo ameongeza kuwa wanawaheshimu wapinzani wao watawakabili kwa nidhamu.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu Simba SC tutawakabili kwa nidhamu kubwa. Tumefanya maandalizi mazuri kimwili, kiakili, kimbinu na hasa kisaikolojia,” alisema Josiah.

Rekodi zinaonyesha Dodoma Jiji FC wamecheza mechi 7 wakiwa nyumbani, ushindi mechi 4, sare 2 ikipoteza mchezo nmoja.

SOMA HII: Yanga SC vs JKT Tanzania NBC Premier League/ Ahmed Ally, Pedro watambiana/ Ratiba, msimamo

aviator

Maoni ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker

Kocha wa Mkuu wa Simba SC, Steve Barker amebainisha kuwa watajithidi kucheza kwa umakini mbele ya wapinzani. Amebainisha kuwa anatambua watakutana na ugumu.

 “Tumejiandaa na ugumu tutakaokutana nao kwenye mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji FC. Tutajitahidi kucheza kwa malengo ili kupata matokeo mazuri,” alisema Barker.

Simba SC ikiwa ugenini NBC Premier League 2025/26 imecheza mechi 3, ilipata ushindi mechi zote 3 ikivuna pointi 9.

C-Chama
Clatous Chama kiungo wa Simba SC. Source: Simba SC

H2H

14/03/2025, Simba SC 6-0 Dodoma Jiji FC
29/09/2024, Dodoma Jiji FC 0-1 Simba SC
17/05/2024, Dodoma Jiji FC 0-1 Simba SC
01/10/2021, Dodoma Jiji FC 0-1 Simba SC

Ligi
Ligi Kuu Bara msimamo.

Hitimisho

Dodoma Jiji FC vs Simba SC ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili uwanjani. Mara baada ya ratiba ya leo kukamilika kituo kinachofuata kwa mnyama ni Kariakoo Dabi.Yanga SC vs Simba SC inatarajiwa kuchezwa Machi Mosi, 2026, Zanzibar.





Share this: