Leo Simba SC wakishinda hakuna mahala wanakwenda hilo lipo wazi. Ni karata ya mwisho inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, CAF Champions League 2025/26. Sababu kubwa ni pointi chache walizovuna kwenye mechi za makundi.
SOMA HII: Kamata matokeo ya Simba SC CAF Champions League/ Fixture, standings
Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

Simba SC wakishinda hakuna mahala wanakwenda watapambana na nani?

Mchezo wa leo Simba SC wakishinda hakuna mahala wanakwenda wanatarajiwa kupambana na kinara wa kundi. Saa 1:00 usiku ni Simba SC vs Stade Malien. Hawa wana uhakika wakutinga hatua ya robo fainali.
Neno la Semaji Ahmed Ally kwa mashabiki
“Ombi langu ni moja kwa Wanasimba, tunafahamu kwamba mechi hii hata tukishinda hakuna mahala tunakwenda lakini kushinda ni muhimu sababu unatengeneza kujiamini kwa wachezaji kuelekea mechi iliyopo huko mbele. Bado tuna vita kubwa kwenye Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho. Ili tujiamini huko mbele lazima tushinde mechi hii. Tumewafunga Mashujaa, tumewafunga KMC lakini watu bado hawajaridhika, sasa mechi hii ni muhimu kushinda ili kuonyesha kwamba tumeimarika.
“Mimi niwape pole mashabiki wa Simba, tumezoea kwenda robo fainali lakini mwaka huu tumeshindwa na hilo ni kawaida kwenye maisha kuna muda unafanya vizuri na kuna muda unafanya arijojo. Sasa asitokee mtu akajifanya ndio ana uchungu sana na Simba akaanza kuwatukana viongozi wetu, hii ni hali ya kawaida, ukishindwa unakaa chini na kujipanga kwa msimu ujao.”
Viingilio vya mechi leo

Mzunguko – Tsh. 3,000
VIP C – Tsh. 5,000
VIP B – Tsh. 10,000
VIP A – Tsh. 20,000
Platinum – Tsh. 100,000.
SOMA HII: Simba SC vs Stade de Malien CAF Champions League/ H2H, live score, predictions

Matokeo ya Simba SC Caf Champions League
| 23/11/2025 | Simba SC | 0 | 1 | Petro de Luanda |
| 30/11/2025 | Stade de Malien | 2 | 1 | Simba SC |
| 24/01/2026 | Es Tunis | 1 | 0 | Simba SC |
| 01/02/2026 | Simba SC | 2 | 2 | Esperance de Tunis |
| 7/2/2026 | Petro de Luanda | 1 | 1 | Simba SC |
Mechi ya mwisho kwa Simba SC CAF
| Tarehe | Mwenyeji | Mgeni | |
| 13/02/2026 | Simba SC | vs | Stade de Malien |
Msimamo wa kundi D

| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Stade Malien | 5 | 3 | 2 | 0 | 11 |
| 2. Esperance de Tunis | 5 | 1 | 3 | 1 | 6 |
| 3. Petro de Luanda | 5 | 1 | 3 | 1 | 6 |
| 4.Simba SC | 5 | 0 | 2 | 3 | 2 |
Hitimisho
Simba SC wakishinda hakuna mahala wanakwenda kwa kuwa pointi zake ni ndogo. Stade de Malien amefuzu hatua ya robo fainali. Matokeo ya mechi ya ES Tunis vs Petro de Luanda yataamua nani ataungana na Stade de Malien hatua ya robo fainali.

