- Kinawaka Jumamosi hii ndani ya Ligi Kuu ya England, kuelekea Ni mchezo mkali wa Arsenal vs Manchester United.
- Mchezo huu unatarajiwa kutoa taswira ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England, hasa kwa vikosi hivi vya Michael Carrick na Mikel Arteta.
- Ikumbukwe vijana wa, Arteta wako kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi 7 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Manchester City na Aston Villa.
Ni Jumamosi ya moto ndani ya Ligi Kuu ya England, kuelekea mchezo mkali wa Arsenal vs Manchester United. Mchezo huu unatarajiwa kutoa taswira ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England. Ikumbukwe vijana wa, Mikel Arteta wako kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi 7 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Manchester City na Aston Villa.
SOMA HII PIA: Man United vs Arsenal ‘live’ Old Trafford: Vikosi, Utabiri, Habari za timu.
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Arsenal vs Manchester United

Manchester United wamekuwa na rekodi bora zaidi wanapokutana dhidi ya Arsenal ambapo, katika michezo 243 wameshinda mechi 102. Arsenal wao wameshinda mechi 91 tu, huku mechi 51 zikiisha kwa matokeo ya sare. Hivyo mchezo huu unakuja kuleta taswira mpya ya historia mpya kati ya timu hizi.
Fomu ya timu hizi kwa sasa
Arsenal
WDWWD
Man United
WLDDD
Mechi zilizopita Arsenal vs Manchester United
Man United 0-1 Arsenal (Agosti 17, 2025)
Man United 1-1 Arsenal (Machi 9, 2025)
Arsenal 1-2 Man United *baada ya mikwaju ya penalti (Januari 12, 2025)
Arsenal 2-0 Man United (Desemba 4, 2024)
Arsenal 2-1 Man United (Julai 28, 2024)
SOMA HII ZAIDI: Manchester City vs. Arsenal: A Premier League Showdown
Vikosi vinavyotarajiwa Arsenal vs Manchester United

Arsenal
Kipa: Raya
Walinzi: Timber, Saliba, Gabriel, Hincapie
Viungo: Odegaard, Zubimendi, Rice
Washambuliaji: Saka, Gyokeres, Trossard
Manchester United
Kipa: Lammens
Walinzi: Dalot, Maguire, Martinez, Shaw
Viungo: Mainoo, Casemiro, Diallo, Fernandes, Dorgu
Washambuliaji: Mbeumo
Habari za timu
Arsenal watawakaribisha United kesho Jumapili katika dimba la Emirates, washika bunduki hao wakiwa na lengo la kuzidi kujisimika kileleni mwa msimamo wa ligi. Ikumbukwe huu ni mchezo wa pili kwa timu hizo kuvaana msimu huu, ambapo katika mchezo wa awali Arsenal iliifunga United bao 1-0. Arsenal wapo kwenye mfululizo wa mechi 12 bila kufungwa, ambapo wanaongoza msimamo wa tofauti ya pointi 7.
Arsenal wanaingia katika mchezo huu wakitoka kupata matokeo bora ya ushindi wa mabao 3-1, walioupata dhidi ya Inter Milan katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Rekodi yao huko Emirates inatisha zaidi, kwani hawajafungwa katika mechi 17 zilizopita walipocheza mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.
Manchester United walionekana kuwa timu tofauti chini ya uongozi wa kocha wao mpya, Michael Carrick walipoifunga Man City mabao 2-0. Ni nyota, Bryan Mbeumo na Patrick Dorgu waliopeleka kilio kwa City na nyota hao wanatarajia kuanza wikiendi hii. Man United haijaifunga Arsenal kwenye ligi tangu 2022, na inaonekana ngumu kuibuka na pointi tatu mbele ya Arsenal ambao wanaonekana kuimarika.
SOMA HII PIA: Arsenal FC muhtasari, ratiba, matokeo, habari za usajili, msimamo wa ligi na takwimu
Hali ya majeruhi kwenye vikosi

Arsenal wana kikosi kamili kwa mara ya kwanza msimu huu. Kocha Arteta anatarajiwa kuingiza kikosi chake cha kwanza kwenye mechi hiyo. Gabriel Jesus amekuwa katika hali nzuri tangu aliporejea kutoka kwenye majeraha na Mbrazil huyo anatarajiwa kuanza. Leandro Trossard na Bukayo Saka nao wanatarajia kuongoza mashambulizi ya mawinga, huku Noni Madueke na Gabriel Martinelli wakilazimika kuanzia benchi.
United pia hawatarajiwi kufanya mabadiliko yoyote kwenye kikosi kilichoishinda Man City. Habari nyingine njema kwao ni kurejea kwa staa wa Morocco na mshindi wa pili wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Noussair Mazraoui.
Hitimisho Utabiri wa Arsenal vs Man United

Ni nukta chache kuelekea Arsenal vs Manchester United na msimu huu, Arsenal wameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao, hii ni baada ya kufunga mabao 10 katika mechi zao 5 zilizopita za nyumbani. Hii inawafanya wapewe nafasi kubwa ya kupata bao. Manchester United nao wamefunga angalau bao moja katika mechi zao tisa za ugenini. Hivyo mechi hii inatabiriwa kuwa na angalau mabao 2. Kwa ujumla matokeo ya mchezo huu yanatarajiwa kuwa ushindi, au sare ya Arsenal.

