Senegal bingwa AFCON 2025bINGWA (-)
  • African Cup of Nations Senegal 1-0 Morocco, Januari 18,2026.
  • Senegal bingwa AFCON 2025 kwa kuifunga Morocco goli 1 ikiwa nyumbani
  • Pape Gueye afunga goli la ushindi, Sadio Mane atwaa tuzo ya mchezaji bora AFCON 2025

Senegal bingwa AFCON 2025 kwa kuifunga Morocco goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliokuwa na ushindani mkubwa. Pape Gueye alifunga goli pekee la ushindi dakika ya 90+4 ikiwa ni muda mfupi kabla ya mchezo kuisha. Katika mchezo huo Senegal walitaka kutoka uwanjani kutokana na kugomea maamuzi ya VAR kuwapa penalti Morocco lakini walirejea kuendelea na majukumu yao Uwanja wa Prince Moulay Abdellah.

SOMA HII: AFCON 2025 final Senegal vs Morocco: Ratiba, Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu

Hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Senegal bingwa AFCON 2025 kwa kuifunga Morocco goli 1-0

Senegal bingwa AFCON 2025
Senegal AFCON 2025.

Ulimwengu umeshuhudia Senegal bingwa AFCON kwa kuifunga Morocco goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali.Wenyeji Morocco walikuwa wanapewa nafasi kubwa kushinda. Hii ilitokana na uwepo wa mashabiki wao wengi na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika soka.

Matokeo ya mpira yameamua Senegal kuwa bingwa. Anatwaa taji hili mara ya pili. Katika fainali aliyotwaa mara ya kwanza ilikuwa mbele ya Misri ambapo walishinda kwa penati. 2025, Sadio Mane alikutana na Mo Salah wa Misri hatua ya nusu fainali na kushinda kwa goli 1-0.

Senegal imefanikiwa malengo ya kuwa mabingwa wa mashindano makubwa Afrika 2025. Hivyo bingwa mtetezi kwa sasa ni Senegal huku Morocco wakiwa ni washindi wa pili katika mashindano haya yaliyofanyika nchini Morocco.

Takwimu za mchezo

Senegal Morocco
11Mashuti17
6Lenga lango5
55%Umiliki45%
21Faulo14
0Kadi nyekundu0
5Kadi za njano2
8Kona10
1Magoli0

Sadio Mane mchezaji bora AFCON 2025

Sadio Mane taji
Sadio Mane akiwa na kombe la AFCON 2025.

Nyota wa taifa ya Senegal, Sadio Mane amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa AFCON 2025. Mane ni yeye alifunga goli kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Misri. Anakuwa mchezaji aliyehusika kwenye magoli mengi ndani ya AFCON ikiwa ni magoli 20.

Hitimisho

Senegal bingwa AFCON 2025 kwa kuifunga Morocco goli 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Prince Moulay Abdellah. Baada ya kazi kuwa kubwa 2025 hatimaye mashindano yamefika mwisho 2026. Mwisho wa mashindano haya ni mwanzo wa mashindano mengine.

Share this: