Al Ahly vs YangaAl Ahly vs Yanga
  • Baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kupisha mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025), na Kombe la Mapinduzi.
  • Hatimaye ratiba ya ligi ya Kuu Bara (Ligi Kuu NBC), inatarajiwa kurejea wikiendi hii kwa michezo kadhaa ya viporo.
  • Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho hatua ya makundi inarejea. Tayari wawakilishi wa Tanzania Yanga SC wameweka wazi matarajio ya kuvaana na Al Ahly Januari 23 na 30.

Baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kupisha mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), na Kombe la Mapinduzi. Hatimaye ratiba ya ligi ya Kuu Bara (Ligi Kuu NBC) inatarajiwa kurejea wikiendi hii kwa michezo kadhaa ya viporo. Pamoja na ratiba hiyo mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho hatua ya makundi inarejea. Tayari wawakilishi wa Tanzania Yanga SC wameweka wazi matarajio ya kuvaana na Al Ahly Januari 23 na 30. Makala hii inakupitisha kwa ufupi katika ratiba hiyo.

SOMA HII PIA: Ligi Kuu Bara NBC: Yanga SC haikamatiki, Azam yaichakaza Simba SC

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Ratiba ya viporo vya Ligi Kuu Bara NBC

Ratiba ya mechi za Ijumaa na Jumamosi
Ratiba ya mechi za Ijumaa na Jumamosi

Ijumaa Januari 16, 2026

Dodoma Jiji vs Singida Black Stars

Jumamosi Januari 17, 2026

Azam FC vs Coastal Union

Jumapili Januari 18, 2026

Simba SC vs Mtibwa Sugar

Jumatatu Januari 19, 2026

Yanga SC vs Mashujaa                                 

Jumapili hii Saa 10:00 jioni, Simba SC watakuwa dimba la Meja Jenerali Isamuhyo wakiwakaribisha Mtibwa Sugar. Hii ni mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwa Kocha, Steve Barker kuiongonza Simba SC. Swali ni je, ataanza kwa ushindi au itakuwaje?

Wananchi Yanga SC baada ya kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, wanarejea katika NBC Premier League ambapo Jumatatu Januari 19, watakuwa dimba la KMC Complex wakiwakaribisha Mashujaa FC kutoka Kigoma. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 10:00 jioni. Wananchi pia wataendelea walipoishia?

SOMA HII ZAIDI: NBC Premier League table 2025/26

Mambo muhimu kuhusu ratiba ya Ligi Kuu ya NBC

Yanga vs Mtibwa Sugar
Yanga vs Mtibwa Sugar

Ikumbukwe Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), ilitangaza rasmi msimu huu mpya wa 2025/26 kuanza rasmi Septemba 17, 2025 mwaka huu na inatarajiwa kuisha Mei 30, mwaka 2026. Bingwa mtetezi wa ligi hiyo inayodhaminiwa na NBC ni klabu ya Yanga SC. Wananchi wanafurahia msuli wa kifedha, kutoka kwa mdhamini wao mkuu 17 Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Katika ratiba ya awali mchezo wenye uzito mkubwa zaidi kwenye ligi, yaani dabi ya Kariakoo ilipangwa kupigwa Desemba 13, 2025 na April 04, 2026. Lakini ratiba hiyo ina mabadiriko kidogo. Mzunguko wa kwanza Wananchi watakuwa nyumbani, kabla ya ule wa pili ni Simba SC kuwa nyumbani. Michezo hii ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa.

Maboresho ya kanuni

Kama kuna jambo lilitia doa mwenendo wa ligi ya msimu ulopita, ni kuahirishwa pasipo sababu za uwazi mchezo wa Kariakoo Dabi. Hali hii ilileta sintofahamu kubwa kiasi cha baadhi ya watendaji wa Bodi ya Ligi kuachia ngazi. Funzo la kadhia hiyo linaonekana kuleta mabadiliko kadhaa ya kanuni.

Miongoni mwa kanuni zilizofanyiwa maboresho ni ile inayohusu kutofika Uwanjani. Kanuni ya 31, kutofika uwanjani inaeleza yafuatayo; Timu yoyote itakayokosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubalika kwa TPLB, au mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu ya kupoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu.

Lakini pia timu kutozwa faini isiyopungua shilingi milioni hamsini (50,000,000/-), ambapo 50% ya faini itachukuliwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na 50% italipwa kwa timu. Timu Kupokwa alama 3 katika msimamo wa Ligi pamoja na Mwenyekiti, au Rais wa Klabu kufungiwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja hadi mitano.

SOMA HII PIA: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji

Ni Al Ahly vs Yanga, Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Yanga SC
Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Yanga SC

Ikumbukwe Yanga SC na Simba SC wanaiwakilisha Tanzania kwenye hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga SC tayari wamewasilisha ratiba ya michezo yao ijayo ambapo watavaana na Al Ahly back-to-back Januari 23 na 30, mwaka huu.

Hitimisho

Ratiba ya ligi kuu ya NBC na mashindano ya kimataifa zimetoka, sasa ni wajibu wa kila timu kufanya maandalizi yake vizuri. Hii ni ngwe ya lala salama, hesabu kali zinahitajika kwa wanaotaka ubingwa na kupata tiketi za mashindano ya kimataifa. Pia jambo muhimu ni kwa wachezaji na viongozi kukumbuka wito wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kuwa ‘my game is fair play’.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.